NJIA ZA KUTIBU SARATANI


image


Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali za matibabu ya ugonjwa wa saratani,ni ugonjwa ambao unaweza kupona ikiwa umegundulika mapema katika hatua za mwanzo na kama ugonjwa huu umefikia hatua za mwisho Tiba yake huwa ni kupunguza makali ya ugonjwa.


Njia za kutibu ugonjwa wa saratani.

1.Saratani inaweza kutibiwa kwa kutumia njia mojawapo ambayo huitwa Tiba homoni.

Njia hii dawa mbalimbali utumika Ili kuweza  kusimamisha homoni ambazo uzalisha saratani, tukumbuke kuwa Kuna homoni ambazo zikiwa mwilini huwa zinazalisha saratani kwa hiyo hizi homoni kama hazijazuiliwa uendelea kuongezeka na kusababisha madhara kwa mgonjwa , kwa hiyo dawa hizi zimetengenezwa iili kuweza kuzuia kuongezeka kwa homoni hizi ambazo usababisha saratani.

 

2. Aina nyingine ya kutibu saratani ni Tiba mionzi.

Hii ni njia ambayo utumia mionzi yenye nguvu kuua seli za saratani, tukumbuke kuwa saratani usababishwa na kuwepo kwa seli zisizotarajiwa katika mwili wa binadamu ambapo kwa kitaalamu huitwa Abnormal cell, kwa hiyo Ili kuweza kupunguza maambukizi mionzi yenye nguvu utumika Ili kuweza kuua hizi seli ambazo usababisha saratani. Kwa hiyo kiasi kikubwa Cha seli hizi zikifa na Maambukizi upungua.

 

3.Aina nyingine ya tiba ni Tiba kemikali.

Hii ni mojawapo ya tiba ya saratani ambapo  dawa utumika Ili kuweza kuua seli zinazosababisha saratani kwa hiyo dawa hizi zinaweza kuwa kwenye mfumo wa vidonge au wakati mwingine zinakuwa kwenye muuundo wa Maji maji ambayo ni drip, kwa hiyo upewa mgonjwa na hizi dawa huua seli ambazo usababisha saratani.

 

4. Njia nyingine bambayo utumika ni upasuaji.

Ni Aina ya njia ambayo utumika kuondoa seli ambazo usababisha saratani, tukumbuke kuwa saratani inaweza kuwa kwenye sehemu yoyote kwenye mwili kwa hiyo kwa kutumia njia hii ya upasuaji kama sehemu fulani imeshambuliwa sana na saratani hiyo sehemu utolewa Ili kuepuka seli hizi kusambaa kwenye sehemu mbalimbali za mwili wa binadamu.

 

5. Njia nyingine ni kutumia dawa mbadala za miti shamba ambazo utumiwa na watu wengi na wengine wamesshuhudia kupona na pia Kuna kutumia ushauri yaani cancelling kwa wagonjwa wa saratani na watu upunguza mawazo na kuendelea na maisha Yao ya kila siku na wengine wanaotumia masage yaani kunyoosha sehemu iliyoathiriwa na damu inaweza kutembea kwenye sehemu husika na wengine wanaotumia Mazoezi Ili kuweza kutibu sehemu iliyolegea.



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    2 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    3 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    4 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    5 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    6 Mafunzo ya php    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Ratiba ya chanjo ya kuzuia kuharisha
Posti hii inahusu zaidi ratiba ya chanjo ya kuzuia kuharisha hii ni chanjo wanayopewa watoto wadogo chini ya miaka mitano kwa lengo la kuzuia kuharisha chanjo hiyo kwa kitaalamu huitwa Rotarix. Soma Zaidi...

image Imani potofu kuhusu kifua kikuu
Posti hii inahusu zaidi imani potofu waliyonayo Watu kuhusu ugonjwa wa kifua kikuu, hizi ni imani ambazo uwepo kwenye jamii na pengine uweza kuaminika lakini si za ukweli. Soma Zaidi...

image Maradhi yatokanayo na fangasi
Somo hili linakwenda kukuletea baadhi ya maradhi yatokanayo na fangasi Soma Zaidi...

image Zijue kazi za ini
Post hii inahusu zaidi kazi za ini, ni kiungo muhimu kwenye mwili ambacho Kina umuhimu sana, bila ini maisha ya mwanadamu yanaweza kuishia pabaya Soma Zaidi...

image Ugonjwa wa Saratani ya ini.
Saratani ya ini ni Saratani inayoanzia kwenye seli za ini lako. Soma Zaidi...

image Magonjwa madogo madogo kwa Mama wajawazito.
Posti hii inahusu zaidi magonjwa madogo madogo kwa akina Mama wajawazito, ni magonjwa ambayo hayawezi kupelekea kupoteza maisha kwa Mama mjamzito, magonjwa haya upotea ikiwa Mama atajifungua. Soma Zaidi...

image Minyoo Ni nini
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maana ya minyoo Soma Zaidi...

image Dalili za mtoto Mwenye UTI
Posti hii inahusu zaidi dalili za mtoto Mwenye UTI,ni dalili ambazo uwapata watoto wadogo chini ya umri wa miaka mitano. Soma Zaidi...

image mkewang alikuwa anasumbuliwa na tumbo kama siku tatu lika tuliya saivi analalamika kiuno na mgongo vina muuma nini tatizo tockt
Maumivu ya tumbo nakiuno kwa mwanamke yanahitaji uangalizi wakina. Kwani kuna sababu nyingi ambazo zinawezakuwa ni chanzo. Soma Zaidi...

image Namna ya kumsaidia mtoto mwenye UTI
Post hii inahusu zaidi namna ya kuwasaidia mtoto akiwa na ugonjwa wa UTI. Soma Zaidi...