image

Njia za kuzuia Malaria kwa wajawazito

Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali za kuzuia Malaria kwa wajawazito na watoto wao wakiwa bado tumboni, tunajuwa wazi kuwa wajawazito wakipata Malaria inaweza kupelekea mimba kutoka kwa hiyo ili kuzuia tatizo hili zifuatazo ni njia zilizowekwa ili kuz

Njia za kuzuia Malaria kwa wajawazito.

1.Kuwapatia wajawazito neti pindi wanapoanza mahudhurio ya kliniki.

Hii ni mojawapo ya njia ambayo inafanya kila mahali nchini ambapo kila mwanamke mwenye mimba akija kuanza mahudhurio ya kliniki anapewa neti ili aweze kulala ndani yake wakati wa usiku na kuzuia mbu wanaoeneza Malaria wasimpate akilala ndani ya neti, kw hiyo akina Mama wale wazembe wa kuhudhuria kliniki mnapaswa kwenda ili kuepukana na Ugonjwa wa Malaria.

 

2.Pia kuna watu wenye mila potofu wakipewa neti badala ya kuitumia wakati wa kulala wanaitumia kufugia kuku na kufunika mazao ili yasiliwe na wadudu kwa hiyo elimu ni ya msingi kwa jamii ili kuepuka vitu vya namna hivyo na wanaofanya mambo kama haya wanapaswa kuchukuliwa na sheria kwa sababu hizi neti ni bajeti ya serikali.

 

3.Na njia nyingine ni kutoa dawa za SP kila mwezi pale ambapo Mama anakuja kwenye mahudhurio ya kliniki. Kila mwezi kwenye vituo vyote akina Mama upewa dawa za SP lengo ni kuzuia wadudu wanasababisha malaria kutofikia mtoto, maana dawa hizi ukaa karibu na plasenta ikitokea mdudu amefika uweza kuuawa na hawezi kupata Malaria, kwa hiyo akina Mama wanaoanza kliniki wakiwa na miezi sita hawapati dawa hizi kwa wakati kwa hiyo wanaweza kuwa katika hatari ya kupata Maambukizi.

 

4.Kuna baadhi ya mila na desturi za watu wakipewa dawa hizo uleta visingizio wakidai watatumia wakiwa njiani eti zinawasumbua na wakienda nyumbani hawatumii wanatumia madawa ya kienyeji hali hii usababisha mama kujifungua mtoto mfu au mimba kutoka, kwa hiyo hakina Mama jaribu kujali maisha yenu na watoto pia nenda kliniki kwa wakati, tumia kila dawa ipasavyo na nakuhakikishia utajifungua salama achana na mila na desturi za zamani maisha yamebadilika kuna magonjwa mengi na vitu vingi kwa hiyo okoa maisha yako na mtoto wako.

 

5.Njia nyingine ni kupima Malaria kwa wajawazito pindi tu wanapoanza mahudhurio ya kliniki, hii inatumika kila sehemu ambapo wanawake wanapoanza kliniki kati ya vipimo vinavyopikwa na Malaria nayo imo kwa kuft hivyo ni kutafuta njia ili kutokomeza ugonjwa huu. Kwa hiyo akina Mama wale wazembe wa kuhudhuria kliniki Malaria ipo na inaweza kumshika mjamzito na kusababisha madhara makubwa kama vile mimba kutoka na kuzaa mtoto mfu, kwa hiyo acha uvivu nenda kliniki



           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/02/08/Tuesday - 09:59:27 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 663


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

SABABU ZA KUKOSA NGUVU ZA KIUME AMA KUWA NA UWEZO MDOGO WA KUHIMILI TENDO LA NDOA
Hii ni hali inayowapata wanaume kushindwa kuhimili tendo la ndoa. Soma Zaidi...

Hivi kipimo cha mimba cha mkojo baada ya kutumika Mara 1 ,hakiruhusiw tena kutumika au
Je ni kweli kupima kimoja cha mloka kinaweza kupima mimba zaidi ya mara moka? Soma Zaidi...

SABABU ZA KUTOKA KWA MIMBA (sababu za kuharibika kwa ujauzito)
Tafiti zinaonesha kuwa karibia asilimia 10% mpaka 25% ya wanawake wanaopata ujauzito, mimba zao hutoka. Soma Zaidi...

Siku za kupata mimba
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu siku za kupata mimba Soma Zaidi...

Sifa za siku za kupata mimba
Somo hili linakwenda kukueleza baadhi ya sifa za siku za kupata mimba Soma Zaidi...

Je bado unasumbuliwa na nguvu za kiume?
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kuondoa tatizo la nguvu za kiume Soma Zaidi...

Samahani nauliza mjamzito akiwa na presha140/90 Kuna madhara?
Presha ya kupanda hypertension huweza kuzumbuwa watu kwa jinsia zote, na umri wote. Wajawazito pia wamekuwa wakisumbuliwa na presha hii mara kwa mara. Soma Zaidi...

Kuwepo kwa maziwa wakati wa ujauzito.
Posti hii inahusu zaidi kuwepo kwa maziwa kwa akina Mama wakati wa ujauzito ni kawaida kwa sababu ya kuzaliwa kwa homoni ambayo usaidia kutoa maziwa. Soma Zaidi...

Maumivu ya tumbo kabla ya kupata hedhi
Je unasumbuliwa na maumivu ya tumbo. Unadhani ni dalili za mimba na ukapima hakuna mimba. Soma Zaidi...

Fahamu kuhusiana na kubalehe kwa msichana na mvulana.
Kubalehe ni wakati mwili wa mtoto unapoanza kubadilika na kuwa wa mtu mzima (balehe) hivi karibuni. Kubalehe ambao huanza kabla ya umri wa miaka 8 kwa wasichana na kabla ya umri wa miaka 9 kwa wavulana. Soma Zaidi...

Dalili za kujifungua hatua kwa hatua
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za kujifungua hatua kwa hatua Soma Zaidi...

Sorry kunamchumba wangu katokwa na majimaji meupe na tumbo linamuuma BAADA mda likaacha nidalili za Nini au.nikawaida tu
Majimaji msule sehemu za siriyanaweza kuashiria mambo mengi ka mwanamke. Ikiwemo ujauzitina maradhi. Pia yanaweza kuashiria kuwa mwanamke unaweza kuoatavujauzito amalaa. Soma Zaidi...