Njia za kuzuia mimba zisiharibike.
Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kuzuia mimba zisiharibike, kwa sababu kila mama anayebeba mimba anategemea kupata mtoto kwa hiyo na sisi hamu yetu ni kuhakikisha kwamba mtoto anazaliwa kwa kuzuia mimba kuharibik
Njia za kuzuia mimba zisiharibike
1. Njia ya kwanza ni kuepuka matumizi ya pombe, dawa za kulevya na kuvuta sigara.
Hizi ndizo njia ambazo Usababisha mimba kutoka kwa sababu baadhi ya vilevi ni vikali na kuwepo kwa nicotine usababisha kuharibika kwa mimba.
2. Fanya mazoezi mepesi mepesi.
Kwa kufanya mazoezi hayo usababisha ukuaji mzuri wa kichanga ila mazoezi makubwa makubwa achana nayo hasa kufanyanya kazi nzito ambazo Usababisha mimba kutoka unapaswa kuepukana nayo ili kuweza kuepuka na matatizo ya kutoka mimba.
3. Jikinge na Maambukizi mbalimbali hasa kwenye via vya uzazi.
Wakati wa ujauzito ni vizuri kabisa kujikinga na kuwepo kwa magonjwa kwenye via vya uzazi kwa sababu yanaweza kusababisha maambukizi.na kusababisha mimba kutoka kwa hiyo na siku zote epuka kujamiiana na wanaume wengi au mbalimbali wakati wa ujauzito ili kupunguza magonjwa.
4. Na pia wakati wa ujauzito ni vizuri kuepuka kutumia sabuni za kunukia kusafisha uke daima tumia sabuni ya kawaida kwa sababu kuna hatari ya kuua bakteria wazuri wa kulinda uke na kusababisha Maambukizi kwenye via vya uzazi na kusababisha mimba kutoka.
5. Punguza matumizi ya vyakula visivyofaa.
Kwa kawaida kuna vyakula ambavyo havifai wakati wa ujauzito ni pamoja na vyakula vyenye kiwango kikubwa cha caffeine kwa mfano kahawa na matumizi ya mara kwa mara ya soda .
6. Tumia mlo kamili wakati wa ujauzito.
Kwa kawaida mlo kamili unatakiwa wakati wa ujauzito ni pamoja na vyakula na mboga mboga za majani na pia matumizi ya vyakula vyenye madini ya chuma kwa wingi kwa kufanya hivyo tunaweza kupunguza kiwango cha mimba kuharibika.fs
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 ai web app π2 Bongolite - Game zone - Play free game π3 Madrasa kiganjani π4 kitabu cha Simulizi π5 Dua za Mitume na Manabii π6 Kitau cha Fiqh
Post zinazofanana:
Unaweza kuhisi chochote ktk tumbo ukiwa na wiki mbili? Na je ukibonyeza tumbo utahisi chochote ukiwa ns wiki
Ni mida gani njamzito ananza kuhisi kuwa tumboni anebeba mtoto.
Soma Zaidi...TATIZO LA KUVIMBA KWA USO NA MIGUU KWA WAJAWAZITO
KUVIMBA VYA MIGUU KWA WAJAWAZITO Kuvimba kwa miguu ni hali inayowapara wengi katika wajawazito.
Soma Zaidi...Wajibu wa mjamzito katika utaratibu wa uleaji wa mimba
Posti hii inahusu zaidi wajibu wa Mama mjamzito katika kileo mimba sio yeye tu Bali na wote waliomzunguka wanapaswa kuhakikisha kuwa mama mjamzito anapaswa kufanyiwa huduma zote Ili kuweza kujifungua salama na bila shida yoyote.
Soma Zaidi...Zijuwe Dalili za minyoo na dalili kuu 9 za minyoo
Utajifunza dalili za minyoo, sababu za minyoo na namna ya kujiepusha na minyoo. Dalili kuu 5 za minyoo mwilini
Soma Zaidi...Jinsi mimba inavyotungwa na namna ambavyo jinsia ya mtoto inavyotokea
Posti hii hasa inahusu kasoro ,utatuzi,na jinsi ya kutunga mimba kwa upande wa mwanamke na mwanaumeΒ .itatupelekea jinsi ya kuangalia kasoro na jinsi ya kutatua hizo kasoro katika jamii zetu.
Soma Zaidi...Dalili za PID
Posti hii inahusu zaidi dalili za PID maana yake ni maambukizi kwenye pelvic kwa kitaalamu huitwa pelvic infection disease, ni ugonjwa unaoshambulia sana wanawake na wasichana
Soma Zaidi...