image

Njia za kuzuia ugonjwa wa kisonono

Posti hii inahusu zaidi njia ambazo utumiwa Ili kuweza kuzuia kuwepo ugonjwa wa kisonono, kwa kufuata njia hizi ugonjwa huu wa kisonono unaweza kupungua kwa kiasi au kuisha kabisa.

Njia za kuzuia ugonjwa wa kisonono.

1. Ili kuweza kuzuia ugonjwa wa kisonono ni vizuri kabisa kujua njia za kusambaa kwa ugonjwa huu ambapo utokea pale mtu mmoja anapojamiiana na mwingine ambaye ana ugonjwa huo bila kutumia kinga kwa hiyo ugonjwa huo utoka kwa mto mmoja kwenda kwa mwingine.

 

 

2. Na pia uweza kusambaa wakati mtoto anapozaliwa.

Pale mtoto akitaka kupita kwenye via vya uzazi vya Mama kabla hajatoka nje anaweza kupata ugonjwa huu ikiwa Mama ana ugonjwa wa kisonono, kwa hiyo baada ya kujua njia za kusambaa kwa ugonjwa huu ni vizuri kujua njia za kutibu kama ifuatavyo.

 

 

3. Kutumia kondom wakati wa kujamiiana.

Kama una wasiwasi na mpenzi unayejamiiana naye ni vizuri kabisa kutumia kondom, kwa sababu katika matumizi ya kinga wadudu hawawezi kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine wakati wa kujamiiana.

 

 

4. Matumizi ya gloves kwa wahudumu wa afya ni muhimu sana.

Kwa Sababu ugonjwa huu kwa wakati mwingine unaweza kutokea kwa kupitia kwenye maji maji, kwa hiyo Mama kama anafanyiwa uchunguzi wa kwenye via vya uzazi Ili kuangalia njia na mambo mengine wakati wa uchungu ni vizuri kutumia gloves Ili kuepuka kuenea kwa ugonjwa huu.

 

 

5. Kitu kikubwa na cha maana zaidi ni kiwapima wanawake wajawazito.

Kwa kufanya hivyo ni rahisi kumtambua ni nani mgonjwa na kumwanzishia matibabu au ni nani ambaye sio mgonjwa na kuweza kujikinga zaidi, kwa hiyo ikitokea Mama anaumwa ni vizuri kabisa kumtibu na mwenza wake na wakati wa matibabu waache kujamiiana kwa mda mpaka matibabu yatakapoisha,

 

 

6. Kuachana na tabia ya kuchangiana nguo.

Kuna tabia ya watu kuchangiana nguo kama vile chupi na taulo, tabia hii kwa wingi utaikuta kwa wanafunzi wa secondary hasa wasichana wanaoishi kwenye shule za bweni, ni vibaya kwa sababu kama Kuna mwenye ugonjwa huu anaweza akasambaza kwa wengine.

 

 

7. Na pia kuachana na tabia ya kutumia via vya uzazi vya bandia, kwa mfano unaweza kukuta mtoto wa kike ana uboo uliotengenezwa kwa bandia akisikia hamu ya kuwa na mwanaume anautumia huo na pia Kuna kipindi anawapatia wengine nao wanaotumia kama Kuna mmoja wapo ana ugonjwa wa kisonono unaweza kukuta wanafunzi wengi Wana ugonjwa huu hata kama wako bweni na hawatoki nje.

 

 

8 . Vile vile elimu inapaswa kutolewa kwa wingi kuhusu ugonjwa huu kwa sababu Kuna ambao hawana taarifa kabisa kuhusu kuwepo kwa magonjwa haya, na kwamba yanatibika ni vizuri kabisa kutoa elimu kwa jamii Ili kujua yafuatayo. Njia zinasababisha kuwepo kwa ugonjwa huu, matibabu yake, madhara ya ugonjwa huu na pia namna ya kuepuka ugonjwa huu.

 

 

9. Kwa kufanya hivyo jamii itaweza kushutuka na kufuata utaratibu unaofaa Ili kuhakikisha kuwa wanakuwa salama na pia wanawasaidia watoto wadogo kuepukana na kuzaliwa na ugonjwa huu ambapo usababisha magonjwa ya macho kama mtoto amezaliwa nao hata pengine kuwepo kwa upofu kama matibabu hayajafanyika mapema





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1267


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

ATHARI ZA KUTOTIBIWA VIDONDA VYA TUMBO
ATHARI ZA KUTOTIBIWA VIDONDA VYA TUMBO Kuachwa kwa vidonda vya tumbo bila kutibiwa, vinaweza kusababisha: Kutokwa na damu kwa ndani. Soma Zaidi...

ugonjwa wa Malaria dalili zake na chanzo chake.
Malaria ni moja ya magonjwa hatari yanayoongoza katika vifo vya watoto wengi duniani walio chni ya umri wa miaka 5. Katika post hii utakwend akujifunza kuhusuugonjwa huu jinsi unavyotokea, hatuwa zake na dalili zake. Soma Zaidi...

JITIBU KWA MUAROBAINI: faida za kiafya za muarobaini
1. Soma Zaidi...

Makundi yaliyo katika hatari ya kupata Ugonjwa wa ngiri.
Posti hii inahusu zaidi makundi ambayo yapo katika hatari ya kupata ugonjwa wa ngiri, ni hatari kwa sababu tunajua kuwa ngiri utokea kwa sababu ya kuta au tishu zinazoshikilia viungo fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwepo kwa uwazi na kufanya viun Soma Zaidi...

Ugonjwa wa upungufu wa maji mwilini.
Upungufu wa maji mwilini hutokea unapotumia au kupoteza Majimaji mengi zaidi ya unayonywa, na mwili wako hauna maji ya kutosha na Majimaji mengine ya kufanya kazi zake za kawaida. Usipochukua nafasi ya Vimiminika vilivyopotea, utapungukiwa na maji. Soma Zaidi...

Maambukizi kwenye mrija wa mkojo(urethritis )
Posti hii inahusu zaidi maambukizi kwenye mrija wa mkojo, maambukizi haya usababishwa na virusi na bakteria. Soma Zaidi...

Sababu za maumivu ya tumbo kitovuni na dalili zake
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya tumbo kitovuni na dalili zake Soma Zaidi...

Ugonjwa wa kisonono
Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa kisonono, ni ugonjwa unaosababishwa na mdudu ambaye kwa kitaalamu huitwa Neisseria gonococcal. Soma Zaidi...

Dalili za fangasi ukeni
Post hii inakwenda kukujulisha dalili za kuwa huwenda una fangasi sehemu zako za siri. Soma Zaidi...

Mbinu za kupunguza Magonjwa ya kuambukiza.
Posti hii inahusu zaidi mbinu mbalimbali ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kupunguza kiwango cha kuwepo kwa magonjwa ya kuambukiza, kwa hiyo zifuatazo ni mbinu ambazo zinapaswa kutumika ili kupunguza kiwango cha magonjwa ya kuambukiza. Soma Zaidi...

Tatizo la ngozi kuwasha (ugonjwa wa kuwashwa kwa ngozi
Dermatitis ni hali inayofanya ngozi yako kuwa nyekundu na kuwasha. Ni kawaida kwa watoto, lakini inaweza kutokea katika umri wowote. Hakuna tiba iliyopatikana ya ugonjwa wa Dermatitis Soma Zaidi...

Vitu vinavyochochea kuwepo kwa Ugonjwa wa ukimwi.
Posti hii inahusu zaidi vitu ambavyo vinasababisha kuongezeka kwa Ukimwi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine na baada ya watu kujua Ugonjwa huu na matokeo ila bado ugonjwa unazidi kuongezeka. Soma Zaidi...