Njia za kuzuia upele

Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali za kuzuia upele, ni njia ambazo utumiwa Ili kupunguza tatizo la upele kwenye jamii, kwa hiyo jamii inapaswa kutumia njia hizi Ili kuweza kupambana na ugonjwa huu ambao unatibika.

Njia za kutibu ugonjwa wa upele.

1. Kwanza kabisa tunapaswa kuoga mara kwa mara walau mara mbili kwa siku kwa wale ambao hawajapata ila kwa waliopata wanapaswa kuoga zaidi ya mara mbili au wakioga hata mara tatu sio mbaya na pia kila wanapooga wanapaswa kubadilisha nguo chafu na kuvaa nguo safi Ili kuweza kuepuka kuendelea kuwepo kwa maambukizi.

 

2. Pia tunapaswa kuwatafuta watu ambao Wana dalili za ugonjwa huu na kuwapatia matibabu muhimu Ili waweze kuwa vizuri Pia kuzunguka kwenye vijiji mbalimbali Ili kuwatafuta wagonjwa wote hasa hasa wale wasiopenda kwenda hospital wapewe elimu Ili waone umuhimu wa kwenda hospital.

 

3. Watu wanapaswa kupewa elimu kuhusu namna ya kufanya usafi kwa sababu kwa wale wanaozingatia usafi ni vigumu sana kupata ugonjwa huu kwa hiyo ni vizuri kuwajulisha njia na namna ugonjwa huu unavyosambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine na jinsi ya kutibu ugonjwa huu.

 

4. Vile vile na mifumo ya maji inapaswa kuboreshwa Ili watu waweze kupata maji ya kutosha kwenye familia na nyumba baada ya nyumba kwa kufanya hivyo watu wataweza kufua na kuoga na maambukizi yataisha au kupunguza kwa kiasi.

 

5. Pia wahudumu wa afya na viongozi wanapaswa kwenda mashuleni kutoa elimu kwa watoto kuhusu namna ya kujikuna kwa sababu watoto wengi wanapata kwa kuambukizana kutoka kwa mtoto mmoja kwenda kwa mwingine na tatizo kama lipo watibiwe kwa wale walioambukizwa Ili kuepuka maambukizi kuendelea.

 

6. Vile vile wahudumu wa afya wanapaswa kuzunguka kutoka kwenye nyumba Moja na nyingine Ili kutibu wale wenye ugonjwa tayari.kwa hiyo jamii inapaswa kuelekezwa kuwa chanzo kikubwa cha ugonjwa huu ni uchafu na dawa kuu ni usafi kwa kujua hivyo hali itaweza kutulia na watu watapona.

 

 Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/04/23/Saturday - 05:38:05 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1161

Post zifazofanana:-