picha

Njia za kuzuia uwepo wa ugonjwa wa Bawasili.

Posti hii inahusu zaidi njia au mbinu ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kuepuka kuwepo kwa ugonjwa wa Bawasili kwenye jamii, hizi ni njia za awali za kupambana na kuwepo kwa Ugonjwa wa Bawasili.

Njia za kuzuia kuwepo kwa ugonjwa wa Bawasili.

1. Njia ya kwanza ni kuhakikisha kuwa ukipata haja kubwa fanya haraka kuitoa na usisubiri mda na pia kama kuna tatizo la choo kuwa ngumu ni vizuri kutafuta matibabu ili kuweza kuepuka madhara ya uwepo wa Bawasili.

 

2. Kuachana na tabia ya kufanya mapenzi kinyume cha maumbile.

Hii ni tabia ambayo imeingia na inatumiwa na watu wengi sana hasa kwa vijana hali inayopelekea kuwepo kwa ugonjwa wa Bawasili na pia kuwepo kwa Maambukizi mbalimbali kwa sababu ya kulegea kwa mishipa ya haja kubwa hali inayosababisha kuwepo kwa Bawasili.

 

3. Kutibu magonjwa ya kuharisha endapo yametokea.

Kwa kawaida kuharisha kwa mda mrefu usababisha kuwepo kwa Ugonjwa wa Bawasili kwa kufanya hivyo tutaweza kuepuka kuwepo kwa Ugonjwa huu.

 

4. Kupunguza matumizi ya vyoo vya kukalia.

Kwa wale wanaotumia sana vyoo vya kukalia wanapaswa kupunguza au kutumia njia nyingine ili kuepuka kuwepo kwa Ugonjwa wa Bawasili.

 

5. Kupunguza tabia ya kunyanyua vitu vizito.

Kwa wale ambao kazi zao mara nyingi ni kunyanyua vitu vizito wanapaswa kupunguza ili kuepuka matatizo ya gonjwa la Bawasili.

 

6. Kupunguza uzito na unene wa kupitiliza.

Kwa kawaida watu wanene na wenye uzito wa kupitiliza wako kwenye hatari kubwa ya kupata ugonjwa huu.

 

7. Kuachana na msongo wa mawazo.

Kuna watu ambao wanaweza kila siku kwa sababu ya kuwepo kwa matatizo kwenye maisha yao kwa hiyo tunapaswa kuwakwaza na kutafuta kitu chochote cha kuwafanya waachane na kukaa kwenye mawazo mda wote.

 

8. Kutoa elimu kwa watu kuhusu Ugonjwa huu. Maana yake, jinsi unavotokea, madhara yake na njia za kufanya ili kuweza kutokomeza kabisa ugonjwa huu kwenye jamii.

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2022/07/09/Saturday - 03:31:35 pm Topic: magonjwa Main: Afya File: Download PDF Views 1595

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉2 Simulizi za Hadithi Audio    👉3 kitabu cha Simulizi    👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉5 Dua za Mitume na Manabii    👉6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana:

Fahamu Ugonjwa unaosababisha madhara kwenye mapafu

Posti hii inaelezea kuhusiana na Magonjwa yanayosababisha madhara kwenye mapafu na kitaalamu hujulikana Ugonjwa wa Acute Respiratory Distress Syndrome (ARDS) hutokea wakati Majimaji yanapojaa kwenye vifuko vidogo vya hewa nyororo (alveoli) kwenye mapafu

Soma Zaidi...
Fahamu ugonjwa wa Varicose vein

Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa vericose veini, hili ni tatizo ambalo utokea katika mzunguko wa damu hasa kwenye miguu.

Soma Zaidi...
Je ugonjwa wa pumu uneweza kusababisha kifo, na nini kifanyike kupunguza madhara?

Ugojwa wa pumu ni hatari na unaweza kutokea ghafla. Lakini je unaweza kusababisha kifo, makalahii itakwend akujibu swali hili

Soma Zaidi...
Sasa UKIMWI unatokeaje?

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia ambazo UKIMWI hutokea

Soma Zaidi...
Dalili kuu 7 za vidonda vya tumbo

Zijuwe dalili kuu 7 za vidonda vya tumbo, kama kiungulia, tumbo kujaa, maumivu ya umbo..

Soma Zaidi...
Fahamu kuhusu Ugonjwa wa Bawasili

Posti hii inahusu zaidi juu ya ugonjwa wa Bawasili, ni ugonjwa unaotokea kwenye njia ya haja kubwa hali ambayo upelekea kuwepo kwa uvimbe au nyama ambazo uonekana hadi nje, kwa lugha ya kitaalamu ujulikana kama haemorrhoid au pokea.

Soma Zaidi...
Dalili za maambukizi ya sikio kwa watoto

Posti hii inazungumzia kuhusiana na dalili za maambukizi ya sikio kwa watoto.

Soma Zaidi...
Dalili za saratani (cancer)

Posti hii inahusu zaidi dalili za kansa, ni dalili ambazo utokea kwa mtu Mwenye tatizo la ugonjwa wa Kansa ingawa sio lazima dalili hizi kutokea tukadhani kuwa ni Kansa Ila zilizonyingi huwa ni kweli dalili za kansa.

Soma Zaidi...
Je mtu anaweza kushiriki mapenzi na mtu mwenye maambukizi ya ukimwi pasipo kuambukizwa?

Naomba kuuliza swaliJe mtu anaweza kushiriki mapenzi na mtu mwenye maambukizi ya ukimwi pasipo kuambukizwa?

Soma Zaidi...