Njia za maambukizi ya Homa ya inni

Njia za maambukizi ya Homa ya inni

Posti hii inahusu zaidi njia za maambukizi ya Homa ya inni, Homa ya inni usababishwa na virusi viitwavyo Hepatitis B, huwapata watu wote hasa wale wenye umri chini ya miaka mitano.

Njia za maambukizi ya Virusi vya Hepatitis B.

1. Njia ambazo virusi vya Hepatitis B uenea ni kama zinafanana na njia za virus vya Ukimwi kwa hiyo tujitahidi kujua namna Homa ya inni inavyoambukizwa tunaweza pia kuepuka ugonjwa huu na kuweza kuishi kawaida pasipo Ugonjwa huu .

 

Kwa hiyo Tunapaswa kushika masharti katika kupambana na Homa ya inni hasahasa kupata chanjo ya Homa ya inni kwa sababu unatolewa bure kwa watoto Ila watu waziy ni malipo. Kwa hiyo tunapaswa kujua njia za maambukizi kama vile.

 

2. Kumwongezea mtu damu, kutoka kwa mwenye virusi vya ugonjwa huu kwenda kwa yule ambaye Hana.

 

Kwa hiyo kabla ya kumwongezea mtu damu kitu Cha kwanza anapaswa kupima Ili kuangalia kama Kuna maambukizi kwenye damu, baada ya kuona kama kuna maambukizi kwenye damu , mtu hasipewa damu hiyo, 

 

3. Mama kwenda kwa mtoto wakati wa kujifungua au mtoto akiwa tumboni kwa mama.

 

Ugonjwa huu wa inni unaweza kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kupitia kwa Mama kwenda kwa mtoto wakati wa kujifungua au wakati mtoto akiwa tumboni kwa mama  kwa hiyo mama akiwa anna mimba anashauliwa kupima ugonjwa wa inni Ili kuhakikisha afya yake na kuepuka hali Ile ya kumwambikiza mtoto.

 

Pia na wakunga wanapaswa kuwa macho wakati wa kumzalisha Mama Ili kuepuka kuendelea kuleta madhara kwa Mtoto na jamii kwa ujumla.

 

4. Maambukizi ya Homa ya inni yanaweza  kupitia kwenye sehemu za uwazi kama vile kwenye vidonda,michubuko na Kuna wengine wanaweza kupata kupitia kwa jasho la mwilini kama likigusana na sehemu ya uwazi.

 

5. Kufanya ngono zembe.

Pengine ugonjwa huu unaweza kupitia kwenye ngono zembe kutoka mtu mmoja kwenda mwingine kwa kupitia kujamiiana kwa hiyo watu wanapaswa kutumia kondomu wakati wa kujamiiana Ili kuepuka hali ya kusambaa kwa ugonjwa huu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine, na pia elimu inabidi kutolewa kwa jamii Ili kuepuka madhara makubwa zaidi ya kuenea kwa ugonjwa wa Homa ya inni.

 

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF Views: 2288

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉2 web hosting     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 Bongolite - Game zone - Play free game    

Post zinazofanana:

Fahamu Ugonjwa wa hepatitis A

Hepatitis A ni ugonjwa wa kuambukiza wa ini unaosababishwa na virusi vya Hepatitis A. Virusi ni mojawapo ya aina kadhaa za virusi vya Hepatitis vinavyosababisha kuvimba na kuathiri uwezo wa ini wako kufanya kazi.

Soma Zaidi...
Ugonjwa wa degedege na dalili zake

Ugonjwa wa degedege ni ugonjwa unaowapata sana watoto chini ya miaka mitano ingawa na watu wazima wanapatwa na ugonjwa huo

Soma Zaidi...
Dalili za ukomo wa hedhi (Menopause) na jinsi ya kuishi nazo.

Ukomo wa hedhi (Menopause) ni hatua ya kibaolojia ambapo mzunguko wa hedhi wa mwanamke husimama kabisa, ikiashiria mwisho wa uwezo wa uzazi. Hali hii huthibitishwa baada ya mwanamke kupita miezi 12 mfululizo bila kupata hedhi. Ni mchakato wa asili unaosababishwa na kupungua kwa homoni za uzazi (estrogen na progesterone). Ingawa inaweza kuleta changamoto za kimwili na kihisia, mbinu sahihi za kimaisha na matibabu ya ushauri yanaweza kuboresha hali ya maisha kwa kiasi kikubwa.

Soma Zaidi...
Dalili zake mtoto mwenye Ugonjwa wa Maambukizi kwenye koo

Pisti hii inahusu zaidi dalili za mtoto mwenye Maambukizi ya ugonjwa wa Dondakoo, tunajua wazi kuwa ugonjwa huu uwashambulia hasa watoto wadogo ambao wako chini ya miaka mitano, kwa hiyo zifuatazo ni baadhi ya Dalili zinazoweza kujitokeza kwa watoto hawa.

Soma Zaidi...
Dalili za fangasi kwenye mapafu

Posti hii inaonyesha dalili za fangasi kwenye mapafu.

Soma Zaidi...
Dalili za Kisukari kwa Watu Wazima

Makala hii inaelezea dalili za ugonjwa wa kisukari kwa watu wazima, sababu zake na namna ya kujikinga.

Soma Zaidi...