Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu nyanja sita za afya
NYANJA SITA ZA AFYA
Kama tulivyosema hapo juu kuwa afya ni kuwa mzima kimwili na kiakili. Hata hivyo nadharia ya afya haiishii hapa ila inaendelea hata kujengwa katika mambo makuu sita. Mambo haya wataalamu wa afya wanayaita components of health. Mambo haya nitayataja hapa chini kwa ufupi tuu kama ifuatavyo
1.afya ya kimwili (physical health); hapa ni kuwa mzima kimwili, na afya hii huweza kujenga kwa kula vizuri, kufanya mazoezi ya mara kwa mara, kuepuka unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara na matumizi ya madawa ya kulevya. Ukifanya hivi unaweza kuboresha mwili wako na kuboresha afya ya kimwili.
2.afya ya kiakili (mental health); hapa tunaangalia kuwa salama kiakili. Mtu akiwa na afya salama ya kiakili anakuwa na uwezo wa kujiamini, anapenda kujifunza vitu vivya na anavifurahia. Mtu mwenye hali hizi tunasema ana afya ya kiakili. Uwoga wa kuogopa watu ni katika maradhi ya kiakili.
3.afya ya mawazo na hisia (emotional health); hapa mtu anauwezo wa kuelezea hisia zake na mawazo yake. Kama kuna jambo limemuudhi analisema. Matu mwenye afya hii anauwezo wa kutaka msaada kwa mtu mwingine bia ya wasi.
4.Afya ya kiroho (spiritual health); hii ni afya inayojengwa na kuwa na imani juu ya mambo fulani. Na mara nyingi hapa tunazungumzia kuwa na imani juu ya dini. Watalamu wa afya wanaonesha mahusiano makubwa kati ya dini na mtu. Wataalamu wanatuambia zaidi matu mwenye imani ya kuna uwezekano mdogo wa kupata maradhi ya moyo kuliko mtu asiye na imani ya dini. -->
5.afya ya kijamii (social health); hii ni afya inayojengwa na kuwa na mahusiano mazuri na jamii. Kusaidia watu, kuitikia watu wanapokuita na kucheka nao na kuzungumza nao ni katika mambo yanayojenga afya hii. Wataalamu wa saikolojia wanatueleza mengi kuhusu afya hii.
6.afya ya mazingira (environmental health); hii afya hujengwa na mazingira yanayotuzunguka. Mtu awe na uwezo wa kupata hea safi na maji safi. Hivi hujenga afya hii. Mazingira kuwa safi na salama huweza kutengeneza afyahii
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi aina kuu za vidonda,kuna aina kuu tatu za vidonda ambapo kila aina utumiwa kwa njia yake kama tutakavyoona hapo chini.
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kuzuia kiungulia
Soma Zaidi...Hii posti inahusu zaidi sifa za mkojo usio wa kawaida,ukiona mkojo wa namna hii unapaswa kwenda hospitalini kwa matibabu au vipimo vya zaidi.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu anayetokwa na damu ya pua
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa aliyeungua na Moto.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi rangi za mkojo na maana zake, hizi ni rangi ambazo uweza kutokea kwenye mkojo wa mtu mmoja na mwingine kwa sababu ya kuwepo kwa magonjwa, chakula,na mtindo wa maisha inawezekana unywaji wa maji au kutokunywa maji.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi kutoa huduma ya kwanza kwa mtu aliyekula chakula chenye sumu, kula sumu ni kitendo Cha kula kitu chochote kama dawa,pombe, kemikali na chakula kichafu.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi huduma ya kwanza kwa mtu aliyengatwa na wadudu. Wadudu ni viumbe vidogo ambavyo hukaa sehemu mbalimbali kama vile kwenye miti na sehemu kama hizo
Soma Zaidi...Vipi utamsaidia mti ambaye amepaliwa na maji? Post hii itakwenda kukifundisha jambo hili.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea utaratibu wa maisha kwa aliye athirika
Soma Zaidi...