Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu orodha ya madini chanzo chake na faida zake
ORODHA YA MADINI NA CHANZO CHAKE NA FAIDA ZAKE.
Kwa ufupi ninakuletea orodha ya madini mablimbali na vyakula ambavyo hupatikana. Pia utajifunza kazi za kila aina ya dini ndani ya miili yetu.
1. Madini ya sodium (table salt) Madini haya unaweza kuyapata kwenye spinach, maharage,punje za maboga n.k.
2.Madini ya chuma. Haya hupatikana kwenye maini, nyama, maharage, na mboga za majani. Madini haya ni muhimu kwa utengenezwaji wa hemoglobin yaani chembechembe nyekundu za damu.
3.Madini ya kashiam(calcium). Haya hupatikana kwenye maziwa,maini, mboga za majani na cheese. Madini haya husaidia katika uimarishwaji wa mifupa, meno, misuli na utengenezwaji wa neva. Husaidia piaa kuwezesha kuganda kwa damu kwenye majeraha. Husaidia katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula kwa kuzifanya enzymes kuwa active.
4. Madini ya phosphorus, haya hupatikana kwenye nyama, maziwa, samaki, na mayai. Husaidia katika uimarishwaji wa mifupa, meno,misuli na shughuli za mfumo wa fahamu na utengenezwajiwa genetic materials.
5. Madini ya Potashiam (potassium) Hupatikana kwenye ndizi, machungwa,nyama na kaa. husaidia katika kurekebisha kiwango cha majimaji mwilini.
6.Madini yakopa ( copper) Haya hupatikana kwenye nyama, samaki, na maini.husaidia katika mifupa na utengenezwaji wa hemoglobin (chembechembe nyekundu za damu).
7.Madini yamanganese Madini haya hupatikana kwenye figo,maini, chai na kahawa. Husaidia katika utengenezwaji wa mifupa, na katika mmeng'enyo wa chakula kwa kufanya enzymes ziwe active.
8.Madini ya iodine Madini haya hupatikana kwenye chumvi na vyakula vya baharini kama samaki. Husaidia katika uzalishaji wa homoni ya thyroid.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vya kuoambana na mafua
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea faida za MATUNDA mbalimbali na mboga, upatikanaji wake na faida zake kiafya. Pia utakwenda kuona MATUNDA na mboga ambayo Ni kinga dhidi ya maradhi hatari Kama kisukari, saratani, maradhi ya moyo na mfumo wa fahamu pamoja na
Soma Zaidi...Hizi ni aina za vyakula ambavyo husaidia katika kuongeza damu kwa wajawazito na watoto.
Soma Zaidi...Utajuaje kama una upungufu wa vitamini C. Zijuwe dalili za upungufu wa vitamini C hapa
Soma Zaidi...Vyakula hivi vinaweza kuwa na hatai kwenye afya ya meno ama kuharibu kabisa meno.
Soma Zaidi...Katika post hii utakwenda kujifunza aina 20 za vitamini. Utajifunza kazu zake mwilini, vyanzo vyake na madhara yanayoweza kutokea kutokana na upungufu wake.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa kutumia maembe kiafya, tunajua wazi kuwa maembe ni tunda ambalo lina umuhimu kwenye afya na uwa na vitamini C kwa hiyo tunapaswa kujua faida zake kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...