image

Papai (papaya)

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula papai

Papai (papaya)

Papai ni katika matunda yanayoingiza afya sana kwenye mwili wa binadamu. Papai lina vitamin C na vitamini A kwa wingi pia kuna potassium na folate. Pia tafiti zinaonesha kuwa antioxidant aina ya lycopene iliyomo kwenye papai husaidia katika kuzuia kupata saratani.

 

Pia papai lina vitamin B, vitamin E na vitamin K. Pia lina madini ya calsium (kashiam) potassium, mgnessium na copper. Pia punje za papai ni dawa kwa baadhi ya matatizo ya ini na figo. Pia kwenye papai kuna protelytic enzymes hawa husaidia katika kuuwa bakteria na minyoo pamoja na wadudu wengine hatari ndani ya tumbo (mfumo wa kum eng’enya chakula).

 

Papai linatambulika kwa kuwa na uwezo wa kuulinda mwili na maradhi ya uzee kama macho, misuli na kuzeheka kwa haraka. Ndani ya papai kuna Zeaxanthin hii ni anti oxidant ambayo inakazi ya kuchija miale hatari ya jua. Pa inaaminika kuwa antioxidant hizi husaidia katika afya ya macho na husaidia katika kudhibiti kudhoofu kwa misuli.

 

Papai huaminika kusaidia kupunguza hatari ya kuwa na ugonjwa wa pumu. Hupunguza hatari ya kuuguwa pumu. Ndani ya papai kuna virutubisho vingi, lakini uwepo wa beta-carotene ndani ya papai husaidia kwa wagonjwa wenye pumu.

 

Ulaji wa antioxidanti zilizopo kwenye papai kama beta-carotene husaidia katika kupunguza athari za kupata maradhi ya saratan kwa vijana. Ulaji wa tunda hili husaidia katika kudhibiti upatikanaji wa saratani ya kwenye via vya uzazi hasa saratani ya korodani.

 

Papai ni katika matunda yenye vitamini K ambavyo ni muhimu katika afya ya mifupa. Hivyo ulaji wa tunda hili husaidia katika kuimarisha afya ya mifupa na kudhibiti kupasuka kwa mifupa. Vitamin k pia husaidia katika ufyonzwaji wa madini ya calcium na huzuia upotevu wa madini haya kupitia mkojo. Kupuka madini haya pia ni muhimu katika kuimarisha na kudhibiti afya ya mifupa.

 

Tafiti za kisayansi zinaonesha kuwa papai n I tunda zuri kwa wenye kisukari. Papai ni katika vyakula vya kambakamba ambacho kina maji kwa wingi. Tafiti zinaonesha kuwa watu wenye kisukari type 1 diabetes wameweza kupunguza kiwango cha sukari mwilini mwao. Wakati huohuo watu wenye kisukari type 2 diabetes wameweza kuimarisha kiwango cha sukari mwilini pamoja na kiwango cha homoni ya insulin.

 

Ndani ya papai kuna enzyme zinazoitwa papain hizi husaidia katika mmeng’enyo wa chakula. Pia kama tulivyo sema papai lina maji nmengi na kambakamba vyote kwa pamoja husaidia katika upatikanaji wa choo na kusaidia katika kudhibiti mmeng’enyo wa chakula.

 

Madini ya potassium (aina ya chumvi) na vitamini vilivyomo kwenye papai husaidia katika kulinda afya ya moyo dhidi ya maradhi hatari yanayoshambulia mfumo wa usukumwaji wa damu. Ulaji wa madini haya wakati huohuo ukiwa unapunguza ulaji wa madini ya sodium (chumvi hii tunayotumia) husaidia katika kuulinda moyo dhidi ya maradhi hatari kama shambulio la moyo, presha na kiharusi (stroke).

 

Ndani ya papai kuna madini ya Choline, haya ni muhimu katika kusaidia miili yetu hasa kulala, kujongea kwa misuli (kukunja na kukunjuka, kutanuka na kusinjaa). pia husaidia katika kulinda mpangiliuo wa utando wa seli, husaidia katika kutunza kumbukumbu pamoja na kujifunza yaani kusoma. Pia husaidia katika ufyonzwaji wa fati (mafuta).

 

Kwa ufupi papai lina matumizi mengi sana kama ukuaji wa nywele na kuzifanya zing’ae, kupona kwa vidonda, ukuaji wa tishu na ukuaji wa mwili kwa ujumla. Na haya yote ni kutokana na kuwepo kwa vitamin c na vitamin A





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1588


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Vyakula vyenye maji kwa wingi
Somo Hili linakwenda kukuletea vyakula vyeny maji kwa wingi na umuhimu wake mwilini Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula viazi vitamu
Soma Zaidi...

Faida za kula asali
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula asali Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula kungumanga
Soma Zaidi...

Vyakula hatari kwa vidonda vya tumbo, na vyakula salama kwa vidonda vya tumbo
Makala hii inakwenda kufundisha vyakuna na vinjwaji salama anavyopaswa kutumia mgonjwa wa vidonda vya tumbo. Pia utajifunza vyakula na vinywaji hatari kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo. Soma Zaidi...

Fahamu vyakula vya nyuzinyuzi
Posti hii moja kwa moja inaenda kuelezea vyakula vya nyuzinyuzi zinazopatikana kwenye matunda na mboga mboga. Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula bamia/okra
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula bamia Soma Zaidi...

Madhara ya upungufu wa protini mwilini
Madhara ya upungufu wa protini ni mengi kiafya. Miongoni mwa madhara hayo ni.. Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Komamanga
Soma Zaidi...

Faida za kula ukwaju
Uchachu wa ukwaju, ndio ubora wake, kuna virutubisho vingi kwa kula ukwaju, soma makala hii Soma Zaidi...

Vitamini C Ni nini?
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maana na historia ya vitamin C Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula mihogo
Some Hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula mihogo Soma Zaidi...