PHP level 1 somo la nane (8)
Hapa utajifunza utofauti kati ya php constant na variable. Na hili ni somo la nane katika mfululizo wa masomo haya ya php level 1.
SOMO LA 8
PHP COSTANTS
Constant ni jina linalowakilisha thamani fulani. Thamani hi haiwezi kubadilika wakti wa code kufanya kazi. Constant inaweza kuanzwa kwa herufi lakini si kwa alama ya dola $ kama ilivyo kwenye variable.
Jinsi ya kuweka constant kwenye php.
Utaanza kuweka neno define likifuatiwa na mabano mfano define() ndani ya mabano utaweka jina la constant na thamani vyote vinatakiwa viwekwe kwenye funga semi.
Mfano:-
<?php
define("tunda", "Tunda ni zao la mti linalopatikana baada ya uwa");
echo tunda;
?>
Hii itakupa matokeo:
Tunda ni zao la mti linalopatikana baada ya uwa
Constant hutumika katika kuweka data ambazo hazitakiwi kubadilika wakati wa kuchakata code. Kwa mfano password na database connection.
KUTUMIA CONSTANT KWENYE PHP FUNCTION
Unaweza kutumia constant kwenye code zako zote yaani constant moja unaweza kuitumia katika code zako bila kujali ipo wapi. Kwa urahisi ni sawa na kusema unaweza kutumia constant hata kwenye function ama kwingineko.
Mfano:-
<?php
define("salamu", "halo hujambo");
function mfano() {
echo salamu;
}
mfano();
?>
Hii itakupa matokeo
Halo hujambo
Mafunzo haya yanakujia kwa ihsani ya bongoclass
Web: www.bongoclass.com
Email:mafunzo@bongoclass.com
Phone: 0774069753 unaweza kunicheki wasap kwa link hii https://wa.me/message/7CTQP5BSWBR5I1
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game 👉2 web hosting 👉3 kitabu cha Simulizi 👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉5 Madrasa kiganjani 👉6 Dua za Mitume na Manabii
Post zinazofanana:
Mafunzo ya HTML kwa wenye kuanza (basic level)
Huu ni utangalizi wa mafunzo ya HTML kwa wenye kuanza level ya kwanza kwa lugha ya kiswahili. Haapa utapata msingi wa kuweza kutengeneza tovuti na blog.
Soma Zaidi...Mafunzo ya HTML Level 2 somo la 8 (HTML FULL COURSE FOR BEGINNERS LESSON 8)
Hili ni somo la mwisho mafunzo ya HTML level 2 (html full course for beginners)
Soma Zaidi...Utangulizi wa Android App Development
Haya ni mafunzo ya muda mfupi katika kujifunza hasa ujuzi wa kutengeneza Android App hata kama haujui kitu kuhusiana na Android Development
Soma Zaidi...Mafunzo ya DATABASE - MySQL database somo la 5
Huu ni muendelezo wa mafunzo ya DATABASE kwa kutumia software ya MySQL na hili ni somo la tano. katika somo hili utajifunza type of data yaani aina ya taarifa ambazo unaweza kuzihifadhi kwenye database yako.
Soma Zaidi...PHP level 1 somo la tano (5)
Haya ni mafunzo ya php na hili ni somo la tano. Katika somovhili utajifunza namna ya kutengeneza functions.
Soma Zaidi...Mafunzo ya HTML level 1 somo la 3 (HTML basic level FOR BEGINNERS)
Hili ni somo la Tatu katika mfululizo wetu wa mafunzo ya HTML kwa basic level kwa wanaoanza kujifunza. Hapa tutakwenda kujifunza tag za html ambazo huwa zinatumika katika uandishi.
Soma Zaidi...