Somo la nane mafunzo ya php, katika somo hili utajifunza kuhusu array na jinsi ya kutengeneza array.
SOMO LA 9
PHP ARRAY
Array ni kama variable, tofauti hii ni kuwa inahifathi thamani ya data nyingi ndani ya variable moja. Yaani variable moja hapa itabeba thamani nyingi tofauti na tulivyosoma hapo nyuma. Cheki mifano hapo chini:-
Array sikuzote inaaznia kuhesabu kuanzia 0 na kuendelea. Unaweza kuchaguwa list katika array ipi unataka kuionyesha na ipi hutaki utafanya hivi kwa kuiondoa namba ya array hiyo ama kuiweka.
Mfano:
$masomo = array("hisabati", "sayansi", "maarifa", "kiswahili", "uraina", "kiingereza");
echo "ninasoma" . $masomo [0] . "," . $masomo[1] . "," . $masomo[3]. "," . $masomo[4]. "," . $masomo[5]. "," . ".";
Hii itakupa matokeo
ninasomahisabati,sayansi,uraina,kiingereza,.
Hapo kwa kutumia variabl ilitakiwa tuweke kila kimoja hapo na variable yake. Mfano hapo tungepata variable 5, yaani
$masomo = “sayansi”;
$masomo = “kiswahili”;
Na kuendelea. Hivyo kwa kutumia array tumeweza kupunguza kazi. Kwa kutumia array unaweza kuwa na list ya vitu hata 1000 kwenye array moja na ukakiweka kila kimoja unapotaka kwa kuangalia index namba ya ke kwa kuanzia 0.
KANUNI YA KUTENGENEZA ARRAY:
Kutengeneza array tunatumia function ya array (); kisha ndani yake ndipo zitafata hizo string ambazo kila moja hutenganishwa kwa kutumia , koma. String ya kwanz akatika array ndio array ya kwanza kuhesabiwa ambayo itakuwa ni namba 0, na inayofata itapewa namba 1.
Kuesabu jumla ya array
Kufanya hivi tutatumia function ya count() mfano.
$masomo = array("hisabati", "sayansi", "maarifa", "kiswahili", "uraina", "kiingereza");
echo count($masomo);
?>
Hii itakupa jibu 6, ina maana ndani yake kuna array sita ambazo zimeanza kuhesabiwa kutoka 0,1,2,3,4,5. hapa unapata jumla ya sita.
Pia unaweza kuonyesha array zote bila hata ya juzitajia nmba zao kama ilivyo kwenye mfano wa kwanza.
$masomo = array("hisabati", "sayansi", "maarifa", "kiswahili", "uraina", "kiingereza");
$arrlength = count($masomo);
for ($a = 0; $a < $arrlength; $a++){
echo $masomo [$a];
}
?>
Hii itakuletea matokeo
Hisabatisayansimaarifakiswahiliurainakiingereza
Tutajifunza zaidi juu ya kufanya hivi katika muendelezo wa masomo haya.
Mafunzo haya yanakujia kwa ihsani ya bongoclass
Web: www.bongoclass.com
Email:mafunzo@bongoclass.com
Phone: 0774069753 unaweza kunicheki wasap kwa link hii https://wa.me/message/7CTQP5BSWBR5I1
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Hapa utajifunza utofauti kati ya php constant na variable. Na hili ni somo la nane katika mfululizo wa masomo haya ya php level 1.
Soma Zaidi...Somo la pili katika mafunzo ya HTML level 2. Katika somo hili utajifunza maana ya HTML pamoja na historia yake fupi.
Soma Zaidi...Huu ni muendelezowa mafunzo ya database kwa kutumia MySQl na hili ni somo la 12. katika somo hili tutajifunza namna ya kufanya mahesabu kwa kutumia SQl katika database
Soma Zaidi...Karibu tena katika somo la nne la mafunzo ya HTML level2 html full course for beginners. Katika somo hili utajifunza kuhusu attributes na namna zinavyofanya kazi
Soma Zaidi...Katika somo hili la php level 1 somo la 6 utajifunza namna ya kutumia tarehe yaani function date() kwenye PHP
Soma Zaidi...Haya ni mafunzo ya muda mfupi katika kujifunza hasa ujuzi wa kutengeneza Android App hata kama haujui kitu kuhusiana na Android Development
Soma Zaidi...Hili ni somo la Tatu katika mfululizo wetu wa mafunzo ya HTML kwa basic level kwa wanaoanza kujifunza. Hapa tutakwenda kujifunza tag za html ambazo huwa zinatumika katika uandishi.
Soma Zaidi...Huu ni muendelezo wa mafunzo ya database kwa kutumia MySQL na hili ni somo la 6. Katika somo hili tutakwenda kuona jinsi ya kutengeneza table kwa kutumia MySQL na kwa kutuma SQL.
Soma Zaidi...Hili ni somo la nne katika mafunzo ya html basic level. Hapa tutakwenda kuona jinsi ya kuzifanyia kazi tag ambazo umejifunza katika somo lililotangulia.
Soma Zaidi...Huu ni muendelezo wa mafunzo ya Database kwa kutumia MySQL na hili ni somo la 10. katika somo hili tutakwenda kuendelea namna ya kupangilia muonekano wa data zako kwenye database.
Soma Zaidi...