Pilipili kali

Pilipili kali

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za pilipili kali

Pilipili kali.

 Watu wengi wamekuwa wakiacha kutumia pilipili etu kwa sababu ya ukali wake. Ila itambulike kuwa ijapokuwa ni kali lakini ila faida nyingi sana kwa afya ya mtu. Pilipili pia ina vitamini c ndani yake kwa kiasi. Vitamini hivi ni muhimu sana katika mfumo mzima wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa na wadudu shambulizi.

 

Pilipili zote zina vitamin A, C na K lakini pilipili nyekundu zimezidi wenzie. Wataalamu wa afya wanazungumza kuwa antioxidant, vitamin A na C vilivyomo kwenye pilipili husaidia katika kuzuia maradhi ya saratani na baadhi ya maradhi yanayohusiana na kuzeheka, na pia husaidia katka kuboresha mfumo wa kinga. Pia vitamin K husaidia katika kuganda kwa damu, kuimarisha mifupa pia husaidia katika kulinda seli.

 

Pilipili nyekundu ni chanzo kizuri cha carotenoid ambayo hutambulika kama lycopene, hii ni mujarabu sana katika kuzuia mwili kupata maradhi ya saratani ya kibofu, njia ya uzazi kwa kinamama na saratani ya kongosho.pia kuna carotenoid inayotambulika kama cryptoxanthin hii nayo hujulikana kwa uwezo wake wa kupambana na kuzuia mwili kupata saratani ya mapafu inayohusiana na uvutaji wa sigara.

 

Wataalamu wa afya wanatueleza kuwa pilipili husaidia katika kurekebisha mapigo ya moyo na kuongeza joto la mwili kwa muda wa dakika 20 baada ya kuila. Hii inaonesha kuwa mwili utakuwa na uwezo wa kuunguza mafuta na cholesteral za ziada kwa muda huo. Pia tafiti nyingine zinaonesha kuwa pilipili husaidia katka kupunguza athari za vidonda vya tumbo kwani husaidia katika kuuwa bakteria ndani ya tumbo.

 

Ndani ya pilipili kuna antioxidant iitwayo piperine. Wataalamu wa afya wanadai kuwa ulaji wa antioxidant husaidia katika kuimarisha afya ya mtu. Piperine inatambulika kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kudhibiti na kulinda uharibifu wa seli. Pia ulaji wa pilipili husaidia katika kuimarisha afya ya ubongo.

 

Kwa ufupi pilipili husaidia sana kwa afya ya mlaji. Pia pilipili husaidia katika kuulinda mwili dhidi ya maradhi ya kisukari, saratani na maradhi ya moyo. Afya ya ubongo, kuimarisha mapigo ya moyo pamoja na kupunguza mgando wa mafuta kwenye mirija ya damu. Pilipili husaidia katika kuufanya mwili uweze kunyonya virutubisho muhimu kutoka kwenye chakula.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Vyakula Main: Post File: Download PDF Views: 3266

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 web hosting     👉3 ai web app     👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉5 Dua za Mitume na Manabii     👉6 Kitau cha Fiqh    

Post zinazofanana:

Vyakula salama na vyakula hatari kwa vidonda vya tumbo

Kamala hii inakwenda kufundisha vyakuna na vinjwaji salama anavyopaswa kutumia mgonjwa wa vidonda vya tumbo. Pia utajifunza vyakula na vinywaji hatari kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo.

Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kula korosho

Somo hili linakwenda kukuletea faida za kiafya za kula korosho

Soma Zaidi...
Vyakula vyenye madini kwa wingi

Somo hili linakwenda kukuletea baadhi ya vyakula vyenye madini kwa wingi

Soma Zaidi...
Namna ya kuandaa mdalasini kwa ajili ya tiba.

Posti hii inahusu namna au njia za kuandaa mdalasini kwa ajili ya tiba ya homoni imbalance kwa wanawake.

Soma Zaidi...