(iv)Qur-an Kushuka Kidogo Kidogo kwa Kipindi cha Miaka 23:
Historia inatuthibitishia kuwa Mtume Muhammad (s.a.w) hakuanza kuufundisha Uislamu na kuutangaza ulimwengu mzima kwa kurejea Qur-an kama Kitabu tulicho nacho hivi sasa bali aya za Qur-an zilikuwa zikimshukia kidogo kidogo kulingana na haja na wakati kwa kipindi chote cha Utume wake cha miaka 23. Kwa maana nyingine Qur-an imeshuka kidogo kidogo katika kipindi chote cha utume kuanzia mwanzo wa Utume 610 A.D. mpaka siku chache kabla ya kutawafu Mtume(saw), 632 A.D. Kuhusu Qur-an kushuka kidogo kidogo tunafahamishwa katika aya zifuatazo:
Na Qur-an tumeigawanya sehemu mbali mbali ili uwasomee watu kwa kituo, na tumeiteremsha kidogo kidogo. (17:106)
Na wakasema wale waliokufuru; Mbona hakuteremshiwa Qur-an yote kwa mara moja? Kama hivi (mnavyoona, tumeiteremsha kidogo kidogo) ili tuuthibitishe, (tuutie nguvu), moyo wako (kwa hizo aya mpya mpya zinazoteremshwa wakati baada ya wakati) na tumeipanga kwa uzuri. (25:32)
Hakika sisi tumekuteremshia Qur-an sehemu sehemu (kidogo kidogo). (76:23).
Kama inavyoonekana katika aya hizi. Qur-an imeshushwa kidogo kidogo ili iwe wepesi kwa Mtume Muhammad (s.a.w) kuufikisha ujumbe uliotangulia kwa ukamilifu kinadharia na kimatendo kabla ya ujumbe mwingine uliofuata.
Kwa upande mwingine Qur-an imeshuka kidogo kidogo ili kuwawezesha waumini wa mwanzo kuihifadhi Qur-an kwa wepesi, kuyaelewa fika mafundisho yake kinadharia na kuwawezesha kuitekeleza Qur-an katika kila kipengele cha maisha yao ili wawe jamii bora ya kuigwa na jamii zitakazofuatia.
Kushuka Qur-an kidogo kidogo kwa muda wa miaka 23 ni hoja nyingine kuwa Qur-an ni Kitabu cha Allah (s.w). Kwa yeyote yule anayeisoma Qur-an kwa makini na akajua mpangilio wake wa aya na sura kama vile sura moja kuwa na mchanganyiko wa aya za mwanzo na zilizoshushwa mwishoni lakini bado kunapatikana mtiririko mzuri wa maudhui na mpangilio wa sura usiofuata mtiririko wa kushuka, utaona kuwa haiyumkiniki kuwa Qur-an ni Kitabu kilichoandikwa na Mtume Muhammad (s.a.w) kama wanavyodai makafiri.
Pia Qur-an ingelikuwa imeandikwa na Mtume Muhammad (s.a.w) isingelichukua muda wote huo, bali ingelibidi aiandike yote kwa muda mfupi ili aweze kuitumia katika kazi yake ya kuwaongoza watu. Ni kawaida kuwa ili kufanikiwa katika utekelezaji wa jambo lolote ni lazima kwanza pawe na nadharia nzuri inayoelekeza namna ya utekelezaji. Halikadhalika, Mtume Muhammad (s.a.w) aliyekuwa kiongozi wa Dola ambaye mfano wake haujapatikana, asingeliweza kufanya kazi nzito na kubwa kiasi hicho bila ya kuwa na nadharia ya kumwongoza. Hivyo, kwa kutokuwa na Qur-an yote mkononi mwake ili kuitumia katika kila hatua ya kazi yake, inadhihirisha kuwa alikuwa akiletewa mwongozo kutoka kwa Allah(sw) katika kila hatua ya kazi yake mpaka alipoikamilisha.
Umeionaje Makala hii.. ?
TAHADHARI KWA WASOMAJI WA QURAN Wasomaji wa qurani wawe na tahadhari katika usomaji wao.
Soma Zaidi...Maulamaa katika elimu ya Quran wametofautiana juu ya aya ya mwisho kushuka. Hata hivyo hapa nitakutajia ambayo imependekezwa zaidi
Soma Zaidi...Surat Ikhlas ni katika sura za kitawhid ambazo zilishuka miaka siku za mwanzoni mwa utume. Sura hii imekuja kujibu maswali mengi kuhusu Allah ikiwemo, Allah ni nani?
Soma Zaidi...Sura hii ni miongoni mwa Sura fupi sanya huwenda ndiosura yenye aya chache kuliko sura zote katika Quran.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza maana ya Tajwid kilugha na kisheria. Pia nitakujuza jukumu ya kusoma tajwid.
Soma Zaidi...