Maadili kati surat Al-Hujurat (49:1-13)

Enyi mlioamini!

Maadili kati surat Al-Hujurat (49:1-13)

(5) Maadili kati surat Al-Hujurat (49:1-13)


Enyi mlioamini! Msitangulize (neno lenu) mbele ya (neno la) Mwenyezi Mungu na Mtume wake; na Mcheni Mwenyezi Mungu; hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua. Enyi mlioamini! msipaze sauti zenu kuliko sauti ya Mtume wala msiseme naye kwa sauti ya nguvu kama mnavyosemezana nyinyi kwa nyinyi, visije vitendo vyenu vikakosa thawabu, na hali hamtambui. (49:1-2)



Kwa hakika wale wanaoangusha sauti zao mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, hao ndio Mwenyezi Mungu amezisafisha nyoyo zao kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu. Basi yatakuwa kwao maghufira na thawabu kubwa (kabisa). Wale wanaokwita nyuma ya nyumba; (uko ndani kwako, wanakuja kukugongea dirisha na kukwita); wengi wao hawafahamu (adabu).Na kama wangalingoja mpaka uwatokee, ingekuwa bora kwao.Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghufira (na) Mwenye rehema. (49:3-5)


Enyi mlioamini! Kama fasiki, (asiyekuwa wa kutegemewa) akikujieni na habari (yoyote ile msimkubalie tu) bali pelelezeni (kwanza), msije mkawadhuru watu kwa ujahili na mkawa wenye kujuta juu ya yale mliyoyatenda. Na jueni ya kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu yuko pamoja na nyiye. (Basi msikilizeni yeye anavyokuambieni). Lau yeye angekutiini katika mambo mengi (mnayoyasema) bila shaka mngetaabika. Lakini Mwenyezi Mungu ameupendezesha kwenu Uislamu na ameupamba nyoyoni mwenu, na amekufanyeni mchukie ukafiri na ufasiki na uasi. Hao ndio walioongoka. (49:6-7)


Kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na neema (zake mmepata haya). Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hikima. Na ikiwa makundi mawili katika waislamu yanapigana, basi fanyeni suluhu baina yao; na likiwa moja la hayo linamdhulumu mwenziwe, basi lipigeni lile linaloonea mpaka lirudie katika amri ya Mwenyezi Mungu. Na kama likirudi, basi yap atanisheni baina yao kwa uadilifu. Na hukumuni kwa haki.Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanaohukumu kwa haki. Kwa hakika Waislamu wote ni ndugu; basi patanisheni baina ya ndugu zenu, na Mcheni Mwenyezi Mungu, ili mrehemewe. (49:8-10)


Enyi mlioamini! Wanaume wasiwadharau wanaume wenzao; huenda wakawa bora kuliko wao; wala wanawake wasiwadharau wanawake wenzao; huenda wakawa bora kuliko wao. Wala msitukanane kwa kabila, wala msiitane kwa majina mabaya (ya kejeli): Jina baya kabisa kuambiwa mtu ni asi baada ya kuwa ni Muislamu. (Na kufanya haya ni uasi) Na wasiotubu, basi hao ndio madhalimu (wa nafsi zao). (49:11)


Enyi mlioamini! Jiepusheni sana na (kuwadhania watu) dhana (mbaya) kwani (kuwadhania watu) dhana (mbaya) ni dhambi. Wala msipeleleze (habari za watu). Wala baadhi yenu wasiwasengenye wengine. Je! Mmoja wenu anapenda kula nyama ya nduguye aliyekufa? La, Hampendi; (Basi na haya msiyapende). Na Mcheni Mwenyezi Mungu. Bila shaka Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba (na) Mwingi wa kurehemu. Enyi watu! Kwa hakika tumekuumbeni (nyote) kwa (yule) mwanamume (mmoja, Adamu) na (yule yule) mwanamke (mmoja; Hawwa). Na tumekufanyeni mataifa na makabila (mbali mbali) ili mjuane (tu basi; siyo mbaguane). Hakika ahishimiwaye sana miongoni mwenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule amchaye Mungu zaidi katika nyinyi. Kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye habari (za mambo yote). (49:12-13)


Mafunzo
Kutokana na aya tulizozisoma tunajifunza yafuatayo:
Kwanza
, waumini wa kweli ni wale ambao hawafanyi jambo lolote kinyume na alivyo agiza Mwenyezi Mungu na Mtume wake.



Pili, waumini wa kweli wanatakiwa wawe na adabu katika kuongea. Wakiongea na wakubwa zao ki-umri au kicheo, wanalazimika kushusha sauti zao.



Tatu, waumini wote ni ndugu moja na waislamu wameamrishwa na Allah (s.w) kuudumisha udugu huu kwa kujizatiti katika kusuluhisha waliogombana wakiwa mmoja mmoja au katika kundi.



Nne, ili kudumisha udugu baina yao, waislamu wanaamrishwa na Mola wao kujiepusha na uzushi, dharau, kutukanana, dhana mbaya, kusengenya na kujiona na kujikweza.



Tano, waumini wanaaswa wasitoe hukumu dhidi ya watu kutokana na tetesi tu. Hawanabudi kufanya uchunguzi juu ya shutuma zilizokuja na kisha kutoa hukumu baada ya kupatikana ushahidi wa wazi




                   




Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 142


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Vipengele vya Mikataba ya 'Aqabah na faida zake katika kuimarisha uislamu Maka na Madina
Katika Hija iliyofuatia katika mwaka wa 621 A. Soma Zaidi...

HISTORIA YA MTUME SULAIMAN(A.S)
Sulaiman(a. Soma Zaidi...

(xvi)Huepuka ugomvi na mabishano
Waumini wa kweli huepuka kabisa tabia ya ugomvi na mabishano. Soma Zaidi...

Mchango wa Waislamu Katika Kuleta Uhuru Tanganyika
i. Soma Zaidi...

maana na asili ya dini, kazi zake na nadharia potofu za makafiri kuhusu dini
2. Soma Zaidi...

historia na maisha ya Mtume IS-HAQ(A.S.) NA YA'AQUUB(A.S.)
Is-haq(a. Soma Zaidi...

Hukumu ya Mtu asiyefunga kwa makusudi mwezi wa ramadhani
Soma Zaidi...

Himizo la kuwasamehe waliotukosea
'Na wasiape wale wakarimu na wenye wasaa miongoni mwenu, kujizuia kuwasaidia jamaa zao, maskini na wale waliohama kwa ajili ya Dini ya Allah; na wasamehe na waachilie mbali (wapuuze yaliyopita). Soma Zaidi...

Qur-an Kushuka Kidogo Kidogo kwa Kipindi cha Miaka 23:
Soma Zaidi...

quran na sayansi
QURANI KATIKA ZAMA ZA SAYANSI NA TEKNOLOJIAAsalaalaamu alykum warahmatullah wabarakaatuh. Soma Zaidi...

Imam Ibn Majah na Sunan Ibn Majah
Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Ayyuub(a.s)
Kutokana na kisha hiki cha Nabii Ayyuub(a. Soma Zaidi...