Muhammad hakufundishwa quran na padri Bahira
(a)Dai la Kufundishwa na Padri Bahira:
Baadhi ya makafiri wanadai kuwa Mtume Muhammad (s.a.w) alijifunza Uyahudi na Ukristo katika safari zake mbili za biashara alizofanya Sham (Syria), hasa katika safari yake ya kwanza alipokutana na Padri Bahirah, alipokuwa na umri wa miaka 12. Tunavyojifunza katika historia ni kuwa Bahirah alikutana na Mtume (s.a.w) njiani na kuashiria kwa Ami yake Abutwalib, kuwa anamkisia kijana wake (Muhammad) ana sifa za yule mtume aliyetabiriwa katika Injili (Rejea Qur-an 61:6).
Je, inamkinika kuwa mazungumzo haya ya njiani ya muda mfupi yawe ndiyo yaliyompelekea Mtume (s.a.w) kuandika Qur-an miaka 28 baada ya makutano hayo? Ikumbukwe kuwa Mtume (s.a.w) alianza kushushiwa wahy wa Quran alipokuwa na umri wa miaka arobaini ambapo alikutana na Bahirah akiwa na umri wa miaka kumi na mbili.
Safari ya pili ya Mtume (s.a.w) kwenda Syria kwa biashara ni pale alipokodiwa na Bibi Khadijah alipokuwa na umri miaka ishirini na tano. Katika kumbukumbu za historia, Mtume (s.a.w) hakufanya mkutano wowote na Wakristo wala Mayahudi kabla ya Utume.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game 👉2 web hosting 👉3 Kitabu cha Afya 👉4 Kitau cha Fiqh 👉5 Dua za Mitume na Manabii 👉6 Madrasa kiganjani
Post zinazofanana:
Mtume Muhammad hakujuwa kusoma wala kuandika ni hoja na kuna hekima zake
(i)Mtume Muhammad (s.
Soma Zaidi...Tofauti kati ya sura za makkah na madinah
Quran (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...yaliyomo: HUKUMU YA MIM SAKINA, NUN SAKINA, MADA, WAQFU, QALAQALA, TAFKHIM NA TARQIQ, USOMAJI WA QURAN
DARSA ZA TAJWID YALIYOMOSURA YA 01 .
Soma Zaidi...