picha

Mtume Muhammad hakujuwa kusoma wala kuandika ni hoja na kuna hekima zake

(i)Mtume Muhammad (s.

Mtume Muhammad hakujuwa kusoma wala kuandika ni hoja na kuna hekima zake

(i)Mtume Muhammad (s.a.w) Kutojua Kusoma na Kuandika:
Iwazi mno katika historia yake kuwa Mtume (s.a.w) hakujua kusoma wala kuandika. Ukweli huu wa historia unathibitishwa na aya za Qur-an zifuatazo:


"Sema (Wewe Nabii Muhammad): Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume wa Allah kwenu nyinyi nyote, (Allah) ambaye ana ufalme wa mbingu na ardhi, hapana aabudiwaye (kwa haki) ila Yeye, Ndiye ahuishaye na ndiye afishaye.Basi mwaminini Allah na Mtume wake, aliye Nabii Ummy, (asiyejua kusoma wala kuandika), ambaye humwamini Allah na maneno yake na mfuateni yeye ili mpate kuongoka." (7:158)


"Na hukuwa mwenye kusoma kitabu chochote kabla ya hiki, wala hukukiandika kwa mkono wako wa kuume, ingekuwa hivyo wangefanya shaka wale wanaotaka kubadilisha (haki)." (29:48)



Sababu ya Mtume (s.a.w) kutojua kusoma wala kuandika imebainishwa wazi katika aya hii ya (29:48) kuwa angelijua kusoma na kuandika watu wakaidi wasio tayari kumwamini Mtume na kuamini Qu-ran kwa sababu si maneno ya Allah(s.w) bali ni maneno aliyoyatunga Mtume (s.a.w) au ni maneno aliyoyanakili kutoka kwenye vitabu vya kale au ni maneno aliyofundishwa na watunga mashairi mashuhuri na kuyanukuu kwenye kitabu. Mtume (s.a.w) angalijua kusoma na kuandika ingalikuwa vigumu sana kuonesha udhaifu wa madai haya.


Lakini kutojua kusoma wala kuandika kwa Mtume (s.a.w) kumewafanya wapinzani wengi wakose hoja ya uwazi ya kukataa kuwa Qur-an si Kitabu cha Allah (s.w).Hata hivyo, pamoja na ukweli wa historia kuwa Mtume (s.a.w) hakuwa ni mwenye kujua kusoma wala kuandika, walitokea watu waliojitia upofu na kudai kuwa Qur-an ni maneno ya Muhammad (s.a.w). Ili kuwahuzunisha na kuwaonesha kuwa ni waongo katika madai yao hayo, Allah (s.w) aliwawekea watu hao na walimwengu kwa ujumla changa moto ambayo tutaiona katika kipengele cha (ix).



Kwa hiyo Mtume Muhammad (s.a.w) kutojua kwake kusoma wala kuandika na bado akawasilisha kwa watu ujumbe mzito wenye hekima kubwa na wenye kumuongoza mwanaadamu kwa usahihi katika kila kipengele cha maisha yake, ujumbe ambao hapana yeyote anayeweza kuleta mfano wake ni ushahidi mkubwa kuwa Qur-an yote kama ilivyo ni maneno ya Allah (s.w).




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2018-08-01 Topic: Quran Main: Dini File: Download PDF Views 2721

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉2 Kitabu cha Afya    👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉4 Kitau cha Fiqh    👉5 Bongolite - Game zone - Play free game    👉6 Madrasa kiganjani   

Post zinazofanana:

Sababu za kushuka Surat al Kafirun

Sura hii imekuja kukata rai ya Makafiri wa Makka kuhusu ibada ya ushirika. Hivi leo tungesema kuhusu dini mseto.

Soma Zaidi...
HUKUMU ZA QALQALA

Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa

Soma Zaidi...
Hukumu za waqfu na Ibtida

waqfu ni misimamo ambapo msomaji wa Quran anaruhusiwa kusimama, kuhema au kumeza mate. Na ibtidai ni kuanza baada ya kutoka kwenye waqf

Soma Zaidi...
Sababu za kushuka surat Ikhlas

Surat Ikhlas ni katika sura za kitawhid ambazo zilishuka miaka siku za mwanzoni mwa utume. Sura hii imekuja kujibu maswali mengi kuhusu Allah ikiwemo, Allah ni nani?

Soma Zaidi...
Hukumu ya Ikhfau katika tajwid

Ikh-fau ni moja ya hukumu za nun sakina na tanwin kwenye hukumu za Quran tajwid

Soma Zaidi...
HUKUMU ZA TAFKHIIM NA TARQIQ

Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa

Soma Zaidi...
Saratul-humaza

Quran (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Tofauti kati ya sura za makkah na madinah

Quran (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
HUKUMU YA NUN SAKINA NA TNWIN

Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa

Soma Zaidi...