(ii)Qur-an Yenyewe Inajieleza kuwa ni Ufunuo Kutoka kwa Allah (s.
(ii)Qur-an Yenyewe Inajieleza kuwa ni Ufunuo Kutoka kwa Allah (s.w) :
Ukiisoma Qur-an kwa makini utakuta kuna aya nyingi zinazojieleza kuwa Qur-an imeshushwa kutoka kwa Allah, kama inavyodhihirika katika aya chache zifuatazo:
Lakini Allah anayashuhudia kuwa aliyokuteremshia (kuwa ni haki) ameyateremsha kwa ilimu yake, na Malaika (pia) wana shuhudia. Na Allah anatosha kuwa shahidi. (4:166).
"Uteremsho wa Kitabu hiki hauna shaka kuwa umetoka kwa Muumba wa ulimwengu. Je, wanasema: "Amekitunga mwenyewe ". (Sivyo hivyo). Bali hicho ni haki itokayo kwa Mola wako ili uwaonye watu wasiojiwa na muonyaji kabla yako. Huenda wakaongoka." (32:2-3)
Na Kitabu tulichokuletea kwa wahyi ndicho cha haki, kinasadikisha (vitabu) vilivyokuwa kabla yake. Bila shaka Allah kwa waja wake ni Mwenye kuwajua vyema na kuwaona vizuri." (35:31)
Ni mwenye kuleta baraka (kweli kweli) yule aliyeteremsha Qur-an kwa mja wake, ili awe muonyaji kwa walimwengu wote. (25:1)
Uteremsho wa Kitabu hiki umetoka kwa Allah, mwenye nguvu, na mwenye hikima. (45:2)
Aya zote hizi na nyingi nyinginezo kama hizi zilizomo ndani ya Qur-an hujieleza wazi wazi kuwa Qur-an ni Kitabu cha Allah (s.w) alichowashushia wanaadamu kupitia kwa Mtume Muhammad (s.a.w). Pangelikuwa na haja gani Mtume kuandika kitabu kisha adai kuwa kinatoka kwa Allah (s.w) tukikumbuka kuwa yeye amekuwa mwaminifu na mkweli katika historia yote ya maisha yake.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
Sura mbili hizi pia hujulikana kwa jina la al muawidhatain ambazo ni surat an Nas na surat al falaq.
Soma Zaidi...Surat Al-Asri imeteremshwa Makka, na hapa utazujuwa sababu za kushuka kwa sura hii
Soma Zaidi...Hapa utajifunza maana ya iqlab katika usomaji wa Quran kwa tajwid
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kufundisha fadhila na faida za kusoma Alhamdu.
Soma Zaidi...Quran (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Kuwa na tamaa huhitaji vitu vya watu si jambo jema. Ila kama tamaa hii itakuhamasisha na wewe kutafuta kitu hicho, kwa uwezo ambao Allah amekupa bila ha kuvuka mipaka yake, hili sio tatizo. Sura hii itakufundisha mengi
Soma Zaidi...Maulamaa katika elimu ya Quran wametofautiana juu ya aya ya mwisho kushuka. Hata hivyo hapa nitakutajia ambayo imependekezwa zaidi
Soma Zaidi...SURAT AL-QURAYSH Sura hii ina majina mawili.
Soma Zaidi...Hukumu za kim sakina na tanwin ni idgham shafawiy, idh-har shafawiy, na Ikhfau shafawiy
Soma Zaidi...