Kukosolewa Mtume (s.a.w) katika Qur-an ni Ushahidi Mwingine kuwa Qur-an ni Kitabu cha Allah (s.w):

(v)Kukosolewa Mtume (s.

Kukosolewa Mtume (s.a.w) katika Qur-an ni Ushahidi Mwingine kuwa Qur-an ni Kitabu cha Allah (s.w):

(v)Kukosolewa Mtume (s.a.w) katika Qur-an ni Ushahidi Mwingine kuwa Qur-an ni Kitabu cha Allah (s.w):



Hoja nyingine inayotufanya tuamini pasi na tone la shaka kuwa Qur-an ni Kitabu cha Allah (s.w) ni kule kukosolewa Mtume (s.a.w) ndani ya Qur-an. Si jambo la kawaida kwa mwanaadamu yeyote mwenye akili timamu kutangaza aibu zake na kujikosoa kwa namna Mtume (s.a.w) alivyokosolewa katika Qur-an, katika Kitabu chake mwenyewe. Atakalolifanya mwandishi mkweli na muadilifu ni kuacha tabia mbaya au udhaifu aliokuwa nao na kuwapa wengine ujumbe kuwa waache udhaifu huo.


Lakini katika Qur-an tunaona kuwa pale Mtume Muhammad (s.a.w) alipoonesha kidogo udhaifu wa kibinaadamu na akaenda kidogo nje ya utendaji anaouridhia Allah (s.w) pale pale Allah (s.w) alimkosoa na kumrejesha katika njia iliyo sawa. Kwa mfano Mtume Muhammad (s.a.w) alipohisi ugumu katika kutekeleza amri ya Allah(sw) ya kumuoa Zainabu bint Jahsh baada ya kuachwa na Zaidi bin Harith, aliyekuwa mtoto wake wa kulea kwa kuchelea Uislamu kutukanwa na kupakwa matope na makafiri na wanafiki, Allah (s.w) ali mzi ndua katika aya zifuatazo:



Na(wakumbushe)ulipomwambia yule ambaye Mwenyezi Mungu amemneemesha (kwa kumuafikia Uislamu) na wewe ukamneemesha kwa kumpa uungwana. naye ni Bwana Zaid bin Haritha ulipomwambia): 'Shikamana na mkeo na umche Mwenyezi Mungu(usimuache)' na ukaficha katika nafsi yako aliyotaka Mwenyezi Mungu kuyatoa(Nayo ni kuwa Mwenyezi Mungu amekuamrisha umuoe wewe huyo mkewe atakapomuacha ili iondoke ile itikadi iliyokuwa ikiitakidiwa ya kuwa mtoto wa kulea ni kama mtoto wa kumzaa), na ukawachelea watu, hali Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye haki zaidi ya kumchelea. Basi alipokwisha Zaidi haja yake na mwanamke huyo, Tulikuoza wewe ili isiwe taabu kwa Waislamu kuwaoa wale wa watoto wao wa kupanga wanapokuwa hawana haja nao. na amri ya Mwenyezi Mungu ni yenye kutekelezwa (33:37)
Mfano mwingine ni pale Mtume (s.a.w) aliposusa kula asali ili kuwaridhisha wake zake ambapo Allah (s.w) alimwonya kama aya ifuatayo inavyotufahamisha:


Ewe Mtume! Mbona (kwa nini) unaharamisha alichokuhalalishia Allah? Unatafuta radhi za wake zako ndiyo maana ukafanya hivi! Na Allah ni mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. (66:1)



Mfano mwingine ni ule wa kukosolewa Mtume (s.a.w) katika Qur-an ni pale alipomkasirikia sahaba kipofu aliyetaka kupata mawaidha mapya na badala yake akawaelekea wakubwa wa makafiri kwa matumaini kuwa watasilimu na kuleta nafuu kubwa katika kazi ya kuusimamisha Uislamu. Kitendo hiki hakukiridhia Allah (s.w) na akamkosoa Mtume wake katika aya zifuatazo:


Alikunja (Mtume) paji akageuza uso, kwa sababu alimjia kipofu, na nini kilichokujulisha (kuwa huyo sahaba pofu hahitaji mawaidha mapya) labda atatakasika (akisikia mawaidha mapya), au atakumbuka (aliyoyasahau) ukumbusho huo upate kumfaa, ama ajionaye hana haja (ya dini), wewe ndiye unayemshughulikia! Na si juu yako kama hakutakasika, lakini anayekukimbilia - naye anaogopa, wewe unampuuza (usifanye hivyo). Sivyo! Hakika hii (Qur-an) ni nasaha (mawaidha), basi kila apendaye atawaidhika (asiyetaka basi muachilie mbali). (80:1-12).



Ni dhahiri kuwa kama Mtume (s.a.w) asingelikuwa Mtume wa Allah(s.w) na kama ndiye yeye aliyeiandika Qur-an, kamwe asingelithubutu kudhihirisha aya hizo katika kitabu chake. Kwa aya hizi na nyingine kama hizi kubakia katika Qur-an na Mtume (s.a.w) kuzitangaza kwa watu kama zilivyo kwa muda wote wa maisha yake ya Utume, ni hoja nyingine kuwa Qur-an si maneno ya Mtume Muhammad (s.a.w) bali ni maneno matukufu ya Allah (s.w).




                   




Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 233


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Kukosolewa Mtume (s.a.w) katika Qur-an ni Ushahidi Mwingine kuwa Qur-an ni Kitabu cha Allah (s.w):
(v)Kukosolewa Mtume (s. Soma Zaidi...

Dalili Kubwa za kukaribia Siku ya kiama
Soma Zaidi...

fadhila za sura kwenye quran
FADHILA ZA BAADHI YA SURA Umuhimu na ubora wa baadhi ya sura na aya. Soma Zaidi...

Hutuba ya ndoa wakati wa kuoa
Soma Zaidi...

Kumkafini maiti namna ya kushona sanda ya maiti na utaratibu wa kumvisha sanda maiti
2. Soma Zaidi...

Maana ya Mirathi na kurithi katika uislamu
Maana ya MirathiMirathi katika Uislamu ni kanuni na taratibu alizoziweka Allah (Sw) katika kuwagawawia na kuwarithisha familia na jamaa, mali aliyoiacha marehemu. Soma Zaidi...

Maana ya Swaumu na Lengo la kufunga
Soma Zaidi...

Mapambano Dhidi ya Maadui wa Dola ya Kiislamu
1. Soma Zaidi...

Sifa za Wanafiki zilizotajwa katika surat Hashir
Huwaoni wale wanafiki wanawaambia ndugu zao walio makafiri miongoni mwa watu waliopewa Kitabu (kabla yenu) Mayahudi (Wanawaambia): "Kama mkitolewa, (mkifukuzwa hapa) tutaondoka pamoja nanyi, wala hat utamtii yoyote kabisa juu yenu. Soma Zaidi...

Kupigwa vita Uislamu Tanganyika na Afrika Mashariki
Soma Zaidi...

Uchaguzi wa Omar (Umar) kuwa khalifa wa Pili baada ya Mtume
Uchaguzi wa 'Umar bin Khattab kuwa Khalifa wa Pili. Soma Zaidi...

Utaratibu wa kuzika maiti ya kiislamu, hatua kwa hatua
Kuzika Kuzika ni kitendo cha nne cha faradh tunacho lazimika kumfanyia ndugu yetu aliyetutangulia kufa. Soma Zaidi...