Na waliposema wanafiki na wale wenye maradhi nyoyoni mwao, "Mwenyezi Mungu na Mtume wake hawakutuahidi ila udanganyifu tu.
Na waliposema wanafiki na wale wenye maradhi nyoyoni mwao, "Mwenyezi Mungu na Mtume wake hawakutuahidi ila udanganyifu tu." Na taifa moja miongoni mwao liliposema "Enyi, wenyeji wa Yathribu (Madina)! Hamna mahali pa kukaa nyinyi, basi rudini Na kundi jingine miongoni mwao likaomba ruhusa kwa Mtume kwa kusema: "Hakika nyumba zetu ni tupu, (hapana watu, tunakwenda zetu)," lakini hazikuwa tupu, hawakutaka ila kukimbia tu. Na lau kama yaliingia (Majeshi ya makafiri) juu yao katika pande zote , kisha wakaombwa kufanya vita (juu ya Waislamu) wangevifanya, na wasingelikaa humo (Madina tena) ila muda kidogo tu (33:12-1 4)
Na kwa yakini walikwishafanya ahadi na Mwenyezi Mungu zamani ya kwamba hawatageuza migongo ; na ahadi ya Mwenyezi Mungu ni yenye kuulizwa. (33:15)
Sema: "Kukimbia hakutakufaeni kama mkikimbia mauti au kuuawa, na kwa hivyo, hamtastareheshwa ila kidogo tu, (kisha mara mtakufa)." Sema: "Ni nani ambaye aweza kukulindeni na Mwenyezi Mungu kama (Mungu) akikutakieni uovu, au akikutakieni rehema?" Wala hawatapata mlinzi wala msaidizi kinyume cha Mwenyezi Mungu.Bila shaka Mwenyezi Mungu anawajua wale wanaojizuia miongoni mwenu (wasende vitani pamoja na Mtume) na wawaambiao ndugu zao; "Njooni kwetu (wala msende kwa Muhammad);" wala hawendi katika mapigano ila kidogo tu (ili kuwadanganya Waislamu). (33:16-1 8)
Wakakufanyieni choyo (kukusaidieni) lakini inapokuja hofu, utawaona wanakutazama, macho yao yanazungukazunguka kama yule aliyezimia kwa mauti; lakini hofu inapoondoka, wanakuudhini kwa ndimi zao kali, wanaifanyia choyo kheri, (hawataki kusaidia). Hao hawakuamini, kwa hivyo Mwenyezi Mungu ameviondoshea thawabu vitendo vyao; na hayo ni sahali kwa Mwenyezi Mungu. (Mpaka sasa kwa woga wao) Wanafikiri yale makundi (ya maadui) hayajaondoka. Na kama makundi hayo yangekuja (tena), wangependa laiti wangekua wako jangwani pamoja na Mabedui, wakiuliza tu habari zenu. Na kama wangalikuwa pamoja nanyi wasingalipigana ila kidogo tu. (Mara wangelikimbia kwa woga wao). (33:19-20)
Sifa za wanafiki zilizoainishwa katika aya hizi ni hizi zifuatazo:
(i) Humdhania Mwenyezi Mungu na Mtume wake dhana mbaya. Walisema wakati ule wa Mtume (s.a.w): "Mwenyezi Mungu na Mtume wake hawakutuahidi ila udanganyifu tu."
(ii) Huwahofisha na kuwakatisha tamaa waumini ili warudi nyuma wasipambane na maadui wa Uislamu.
(iii) Hutoa nyudhuru za uwongo ili kuepa majukumu ya kuuhami Uislamu na kuuendeleza.
(iv) Huvunja ahadi kila wanapoahidi.
(v) Hawako tayari kupata misukosuko kwa ajili ya Uislamu na huogopa kufa. Hivyo hujitenga mbali na mapigano dhidi ya maadui wa Uislamu.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Mambo ya faradhi kuhusu maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Zifuatazo ni njia nyingi za kumjua Mwenyezi Mungu (EDK form 2:dhana ya elimu katika uislamu)
Soma Zaidi..."Na (wazazi wako) wakikushurutisha kunishirikisha na (yale) ambayo huna ilimu nayo, usiwatii; lakini kaa nao kwa wema hapa duniani (Maadamu ni wazee wako, ila usiwafuate tu mwenendo wao mbaya); Shika mwenendo wa wale wanaoelekea kwangu, kisha marejeo yenu
Soma Zaidi...Mtazamo wa uislamu juu ya ibada (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Na tukiutafiti Uislamu kwa makini kama mfumo kamili wa maisha tunaona unadhihiri ukweli wa aya hii ya Qur-an.
Soma Zaidi...Maana ya dini kwa mujibu wa makafiri ina utofauti mkubwa na vile ambavyo uislamu unaamini kuhusu dini.
Soma Zaidi...