Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat at-Tawbah

Mwenyezi Mungu amekuwia radhi (amekusamehe).

Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat at-Tawbah

Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat at-Tawbah



Mwenyezi Mungu amekuwia radhi (amekusamehe). Kwa nini umewapa ruhusa ?(Ungengoja)mpaka wanaosema kweli wakupambanukie, na uwajue waongo(9:43).


Hawatakuomba ruhusa wale wanaomuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho. (Hawatakutaka ruhusa) kutoipigania dini ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na nafsi zao. Na Mwenyezi Mungu anawajua wanaomcha.(9:44)


Wanakuomba ruhusa wale wasiomuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, na nyoyo zao zina shaka; kwa hivyo wanasitasita kwa ajili ya shaka yao. (9:45)


Na kama wangalitaka kutoka (kwenda vitani) bila shaka wangaliandalia maandalio yake (lakini hawakufanya lolote, ni alama kuwa hawakuwa na nia ya kwenda huko vitani). Mwenyezi Mungu hakupenda kutoka kwao (kwenda huko vitani). Na kwa hivyo akawazuia na ikasemwa (na Shetani) "Kaeni pamoja na wanaokaa. "Kama wangalitoka pamoja nanyi wasingalikuzidishieni ila mchafuko, na wangekwenda huku na huku baina yenu kukutakieni fitina (kukugombanisheni).Na miongoni mwenu wako wanaowasikiliza (watu wabaya hao). Na Mwenyezi Mungu anawajua madhalimu. Tangu zamani walitaka kukutilieni chokochoko (na fitina) na wakakupindulia mambo chini juu, mpaka ikafika haki na kudhihirika amri ya Mwenyezi Mungu; juu ya kuchukia kwao. (9: 46-48)


Na miongoni mwao yuko anayesema (kumwambia Mtume): "Niruhusu (nisije vitani) wala usinitumbukize katika fitina (kwa kuona wanawake wa huko nikafitinika nao)." Hakika wao wamekwishatumbukia katika fitina. Na kwa yakini Jahannamu itawazunguka makafiri (wasiwe na pa kutokea). Ukikufikia wema (wewe Mtume na Masahaba) unawachukiza; na ukikufikia msiba husema: "Tuliangalia vizuri tangu zamani mambo yetu (kwa hivyo hatukufikwa na balaa hii)," na hugeuka wanakwenda zao nao wamefurahi. Sema: "Halitatusibu ila alilotuandikia Mwenyezi Mungu. Yeye ni Mola wetu." Basi Waislamu nawamtegemee Mwenyezi Mungu tu. (9:49-51)



Sema: "Nyinyi hamtutazamii sisi ila (kupata) moja katika mema mawili (ima kushinda tukapata ngawira au kuuawa tukapata Pepo). Na sisi tunakutazamieni kuwa Mwenyezi Mungu akufikishieni adhabu itokayo kwake au (inayopatikana) kwa mikono yetu. Basi ngojeni, nasi tunangoja pamoja nanyi." Sema: (kuwaambia hawa wanafiki): Toeni (mali yenu) kwa kupenda au kwa kutopenda, hakutakubaliwa kwenu (kutoa huko). Hakika nyinyi ni watu maasi. " Na haikuwazuilia ikubaliwe kwao michango yao, ila kwa sababu walimkataa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala hawafiki mahala pa kusali ila katika hali ya uvivu. (9:52-54)


Wala hawatoi (hivyo wanavyovitoa) ila kwa kuchukia. Yasikufurahishe mali yao wala watoto wao. Anataka Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa hayo katika maisha ya dunia, na zitoke roho zao, na hali ya kuwa ni makafiri. Na


wanaapa kwa (jina) la Mwenyezi Mungu kwamba wao ni pamoja nanyi. Wala wao si pamoja nanyi.Bali wao ni watu wanaoogopa (ndio maana wanasema uwongo huku kwa Waislamu na huko kwa makafiri). Kama wangalipata pa kukimbilia au mapango au mahali (pengine) pa kuingia, (bila shaka) wangekimbilia mbio huko, wanakwenda shoti (kama farasi waliochafuka). (9:55-5 7)


Na miongoni mwao (hao wanafiki) wako wanaokusema katika (kugawa kwako) sadaka. Wanapopewa katika hizo (Sadaka na Zaka) huridhika; na wakitopewa katika hayo wanakasirika. Na kama wangeyaridhia yale aliyowapa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na wakasema: "Anatutoshea Mwenyezi Mungu, karibuni Mwenyezi Mungu atatupa katika fadhila zake, na Mtume wake (pia); hakika sisi tunaelekea kwa Mwenyezi Mungu." (9:58-59)



Sadaka hupewa (watu hawa): - Mafakiri na masikini na wanaozitumikia na wanaotiwa nguvu nyoyo zao (juu ya Uislamu) na katika kuwapa Uungwana watumwa na katika Kuwasaidia wenye madeni na katika mambo aliyoamrisha Mwenyezi Mungu na katika (kupewa) Wasafiri (walioharibikiwa). Ni faradhi inayotoka kwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi (na) Mwenye hikima. Na miongoni mwa (hao wanafiki) wako wanaomuudhi Mtume na kusema: "Yeye ni sikio tu" (yaani anasikia maneno bila ya kuyapima. Waongo wakubwa). Sema "Sikio la kheri kwenu "; anamuamini Mwenyezi Mungu na anawasadiki wanaoamini. Na ni rehema kwa wale wanaoamini miongoni mwenu. Na wanaomuudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu watakuwa na adhabu inayoumiza (9:60-61)


Wanakuapieni Mwenyezi Mungu ili kukuridhisheni (japo wanamuudhi Mwenyezi Mungu na Mtume), hali ya kuwa Mwenyezi Mungu - na Mtume wake (pia) - ana haki zaidi ya kuwa wao wamridhishe, ikiwa wao ni wanaoamini. Je, hawajui ya kwamba anayeshindana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi yeye atapata moto wa Jahannamu kukaa humo daima? Hivyo ndiyo hizaya kubwa (udhalilifu inayowangojea). (9:62 -63)



Wanafiki wanaogopa kuteremshiwa sura itakayowatajia (unafiki wao) uliomo katika nyoyo zao. Sema: "Fanyeni tu mzaha, hakika Mwenyezi Mungu atayatoa nje hayo mnayoyaogopa." Na kama ukiwauliza (kwa nini waifanyia mzaha dini) wanasema: "Sisi tulikuwa tukizungumzazungumza na kucheza tu." Sema: "Mlikuwa mkimfanyia mzaha Mwenyezi Mungu na Aya zake na Mtume wake?" Msitoe udhuru (wa uwongo); umekwisha kudhihiri ukafiri wenu baada ya kule kuamini kwenu (kwa uwongo). (9:64-66)


Wanaume wanafiki na wanawake wanafiki, wote ni hali moja; huamrisha yaliyo mabaya na huyakataza yaliyo mazuri, na kuizuilia mikono yao (hawasaidii mambo ya kheri); wamemsahau Mwenyezi Mungu (wamepuza amri Zake); na


Yeye pia amewasahau (amewapuza). Hakika wanafiki ndio wavunjao amri.Mwenyezi Mungu amewaahidi wanafiki wanaume na wanafiki wanawake na makafiri, moto wa Jahannamu kukaa humo daima.Huo unawatosha (kuwaadhibu); na Mwenyezi Mungu amewalaani; nao wana adhabu itakayodumu. (9:67-68)



Sifa za Wanafiki zilizoainishwa katika aya hizi ni hizi zifuatazo:
(i)Huepa jukumu la kupambana na maadui wa Uislamu kwa kutoa nyudhuru za uongo.
(ii)Nyoyo zao zina shaka, kwa hivyo wanasita sita kwa ajili ya shaka yao.
(iii)Huchochea fitna baina ya Waislamu.
(iv)Wanachukia mafanikio ya Waislamu.
(v)Waislamu wanapopatwa na msiba hufurahia.
(vi)Huendea swala kwa uvivu.
(vii)Wanapotakiwa watoe mali kwa ajili ya Allah (s.w), hutoa kwa kuchukia.
(viii)Huapa kwa jina la Allah kuwa wapo pamoja na Waislamu. Kihalisia hawapo pamoja na Waislamu bali wao ni maadui wa Waislamu.
(ix)Ni waoga. Wanaogopa kufa.
(x)Mgao wa zakat na sadaqat ukiangukia kwao hufurahia lakini ukienda kwa wengine wanaostahiki zaidi kuliko wao hukasirika na kunung'unika.
(xi)Wanamuudhi Mtume (viongozi) kwa kumtukana na kumkejeli.
(xii)Wanaogopa kudhihirishwa uovu wao waliouficha vifuani mwao.
(xiii)Humfanyia mzaha Mwenyezi Mungu na Mtume wake. (xiv)Huamrisha mabaya na kukataza mema.




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Tawhid Main: Dini File: Download PDF Views 818

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya    👉2 Madrasa kiganjani    👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉4 Simulizi za Hadithi Audio    👉5 kitabu cha Simulizi    👉6 Kitau cha Fiqh   

Post zinazofanana:

Kujiepusha na maringo na majivuno

Maringo, majivuno, majigambo, dharau ni vipengele vya kibri.

Soma Zaidi...
Nafsi ya mwanadamu inavyothinitisha uwepo wa Allah

Mwanadamu ukifikiria vyema. Kuhusu nafsi yako, hakika utapatabfikra yabuwepp wa Mwenyezi Mungu

Soma Zaidi...
Nafasi ya Elimu katika uislamu

Elimu imepewa kipaumbele kikubwa kwenye uislamu. Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu nafasi ya Elimu katika uislamu.

Soma Zaidi...
Haki za kielimu za mwanamke katika uislamu

Haki ya ElimuKatika Uislamu kujielimisha ni faradhi inayowahusu Waislamu wote, wanaume na wanawake: "Soma kwa jina ?

Soma Zaidi...
Maswali juu ya dini anayostahiki kufuata mwanadamu

Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Mtazamo wa Uislamu juu ya maana ya dini

Uislamu unaitazama dini katika nyanja zote za maisha ya mwanadamu. Hii ni tofauti na mtazamo wa kikafiri juu ya dini.

Soma Zaidi...