Huwaoni wale wanafiki wanawaambia ndugu zao walio makafiri miongoni mwa watu waliopewa Kitabu (kabla yenu) Mayahudi (Wanawaambia): "Kama mkitolewa, (mkifukuzwa hapa) tutaondoka pamoja nanyi, wala hat utamtii yoyote kabisa juu yenu.
Huwaoni wale wanafiki wanawaambia ndugu zao walio makafiri miongoni mwa watu waliopewa Kitabu (kabla yenu) Mayahudi (Wanawaambia): "Kama mkitolewa, (mkifukuzwa hapa) tutaondoka pamoja nanyi, wala hat utamtii yoyote kabisa juu yenu. Na kama mkipigwa vita lazima tutakusaidieni." Na Mwenyezi Mungu anashuhudia ya kuwa wao ni waongo. Kama wakifukuzwa hawatatoka pamoja nao, na kama wakipigwa hawatawasaidia; na kama wakiwasaidia kwa yakini watageuza migongo (wende mbio); kisha hawatanusuriwa. (59:11-1 2)
Hakika nyinyi (Waislamu) mnaogopwa zaidi katika nyoyo zao kuliko wanavyomuogopa Mwenyezi Mungu; maana wao ni watu wasiofahamu (lolote). (59:13)
Hawatapigana nanyi kwa mkusanyiko isipokuwa katika vijiji vyao vilivyohifadhiwa, au nyuma ya kuta. Vita vyao baina yao vikubwa. Utawadhani kuwa wako pamoja; kumbe nyoyo zao ni mbali mbali. Hayo ni kwa sababu wao ni watu wasio na akili. Hali yao (hawa Mayahudi wa Kibanu Nadir) ni kama ya wale (Mayahudi wa Bani Qaynuqai) waliowatangulia (kufikwa na baa) hivi karibuni; walionja ubaya wa mambo yao; na watapata adhabu (nyingine) iumizayo (vile vile). Ni kama Shetani anapomwambia mtu: "Kufuru;" na anapokufuru akamwambia: "Mimi si pamoja nawe, hakika namuogopa Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu. "(59:14-16)
Basi mwisho wa wote wawili hao ukawa waingie Motoni kukaa humo daima; na hiyo ndiyo jaza ya madhalimu. (59:17)
Sifa za wanafiki zilizoainishwa katika aya hizi ni hizi zifuatazo:
(i)Hushirikiana na kusaidiana na makafiri katika kuuhujumu Uislamu na Waislamu.
(ii)Wanawaogopa watu kuliko wanavyo muogopa Allah (s.w)
(iii)Wanaonekana kuwa wamoja lakini kiutendaji kila mmoja yuko na lake. Umoja wao ni kama ule wa inzi, likitupwa jiwe kila mmoja hutawanyika kikwake tofauti na mshikamano ule wa kundi la nyuki ambao wakichozwa hushambulia kwa pamoja mpaka kumkibiza adai
Umeionaje Makala hii.. ?
Ni upi mgawanyo sahihi wa elimu kwa mtazamo wa uislamu (EDK form 1: mgawanyo sahihi wa elimu kwa mtazamo wa uislamu
Soma Zaidi...Maringo, majivuno, majigambo, dharau ni vipengele vya kibri.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunz akuhusu nuzo 6 za imani ya uislamu na pia utajifunz akuhusu mafunzo yanayoweza kupatikana kwenye Nguzo hizi.
Soma Zaidi...Kwenye kipengele hichi tutajifunza lengo la kuumbwa mwaanadamuengo la kuumbwa ulimwengu na viumbe vilivyomo.
Soma Zaidi...Elimu ndiyo zana aliyotunukiwa mwanadamu ili aitumie kutekeleza majukumu yake kama Khalifa wa Allah (s.
Soma Zaidi...Mafundisho ya mitume ni eneo lingine linalo thibitisha kuwepo Allah (s.
Soma Zaidi...Wanapokujia wanafiki, husema: "Tunashuhudia ya kuwa kwa yakini wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu.
Soma Zaidi...