picha

Sifa za wanafiki zilizotaja katika surat An-Nisaa (4:60-63, 88, 138-145)

Huwaoni wale wanaodai kwamba wameamini yale yaliyoteremshwa kwako na yaliyoteremshwa kabla yako?

Sifa za wanafiki zilizotaja katika surat An-Nisaa (4:60-63, 88, 138-145)

(3) Sifa za wanafiki zilizotaja katika surat An-Nisaa (4:60-63, 88, 138-145)


Huwaoni wale wanaodai kwamba wameamini yale yaliyoteremshwa kwako na yaliyoteremshwa kabla yako? Nao wanataka wakahukumiwe kwa njia ya twaghuuti; na hali wameamrishwa kukataa njia hiyo. Na Shetani anataka kuwapoteza upotofu (upotevu) ulio mbali (na haki).(4:60)


Na wanapoambiwa "Njooni katika yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, na (njooni) kwa Mtume," utawaona wanafiki wanajiweka mbali nawe kabisa. Basi itakuwaje utakapowafikia msiba kwa sababu ya yale iliyotanguliza mikono yao?Kisha wakakujia wakiapa "Wallahi! Hatukutaka ila wema na mapatano." Hao ndio wale ambao Mwenyezi Mungu anayajua yaliyomo nyoyoni mwao. Basi waachilie mbali, (lakini) uwape mawaidha na uwaambie maneno yenye taathira yatakayoingia katika nafsi (nyoyo) zao. (4:61-63)


Imekuwaje nyinyi kuwa makundi mawili katika khabari ya wanafiki, na hali Mwenyezi Mungu amewageuza kwa sababu ya yale (mabaya) waliyoyachuma? Je! Mnataka kumwona mwongofu ambaye Mwenyezi Mungu amemhukumu kuwa kapotea? Na aliyemhukumu Mwenyezi Mungu kuwa amekwisha potea hutampatia njia (ya kuambiwa mwongofu). (4:88)


Waambie wanafiki kwamba watapata adhabu inayoumiza. (Wanafiki) ambao huwafanya makafiri kuwa marafiki badala ya Waislamu. Je! Wanataka wapate utukufu kwao? Basi utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu. (Hauko katika mkono wa mtu). Naye amekwisha kuteremshieni katika Kitabu (hiki) ya kwamba mnaposikia Aya za Mwenyezi Mungu zinakataliwa na kufanyiwa stihzai, basi msikae pamoja nao, hata waingie katika mazungumzo mengine. (Mtakapokaa) mtakuwa kama wao. Hakika Mwenyezi Mungu atawakusanya wanafiki na makafiri wote pamoja katika Jahannam. (4:138-140)



(Wanafiki) ambao wanakungojeni (mpate msiba): basi mkipata kushinda kunakotoka kwa Mwenyezi Mungu, husema (kukwambieni): "Je! Hatukuwa pamoja nanyi?" (Na kama makafiri wamepata sehemu (ya kushinda) husema: (kuwaambia makafiri), "Je, hatukukurubia kukushindeni (tulipokuwa katika jeshi la Waislamu), tukakuzuilieni na (kudhuriwa na hao). Waislamu?" Basi Mwenyezi Mungu atahukumu baina yenu siku ya Kiyama. Na Mwenyezi Mungu hatawajaalia makafiri njia ya kuwashinda Waislamu (kabisa kabisa mpaka waiondoshe dini yao. Hawatajaaliwa kupata hayo). Wanafiki hutaka kumdanganya (hata) Mwenyezi Mungu. Naye atawaadhibu kwa sababu ya kudanganya kwao (huko). Na wanaposimama kusali husimama kwa uvivu, wanaonyesha watu (kuwa wanasali) wala hawamtaji Mwenyezi Mungu ila kidogo. (4:141-42)



Wanayumbayumba baina ya huku (kwa Waislamu na huko kwa makafiri). Huku hawako wala huko hawako. Na ambaye Mwenyezi Mungu amemhukumu kupotea, huwezi kumpatia njia (ya kuhisabika kuwa mwongofu). Enyi mlioamini! Msiwafanye makafiri kuwa marafiki badala ya Waislamu. Mnataka awe nayo (Mtume wa) Mwenyezi Mungu hoja dhahiri juu yenu (ya kuwa nyinyi wabaya)? Bila shaka wanafiki watakuwa katika tabaka la chini kabisa katika moto. Hutamkuta kwa ajili yao msaidizi (yo yote). (4:143-145)



Katika aya hizi sifa za wanafiki zinaainishwa kama ifuatavyo:
(i)Wanapendelea kuhukumiwa kwa sheria za Kitwaghuut kuliko kuhukumiwa kwa sheria za Allah (s.w)
(ii)Hawako tayari kuishi kwa kufuata Qur-an na Sunnah.
(iii)Hutumia sana viapo katika kuficha uovu wao dhidi ya Uislamu na Waislamu.
(iv)Huwafanya makafiri kuwa marafiki badala ya Waislamu.
(v)Hujikomba kwa makafiri kwa kutaraji kupata vyeo au kuonekana wa maana kwao.
(vi)Wanashirikiana na makafiri katika kuzifanyia stihizai aya za Allah (s.w) na Uislamu kwa ujumla.
(vii)Waislamu wakishinda, hujikomba kuwa pamoja nao na hujinakshi (hujigamba) kuwa wao ndiwo waliosababisha kupatikana kwa ushindi.
(viii)Makafiri wakishinda hujikomba kwao na kujinakshi kuwa ndio waliowawezesha kushinda.
(ix)Hawana msimamo. Kwa Waislamu hawapo na kwa makafiri hawapo. Hivyo hawaaminiki kote kote.
(x)Wanaposimama kuswali, husimama kwa uvivu.
(xi)Hufanya amali kwa riya (kwa kuonyesha watu). (xii Hawamtaji Mwenyezi Mungu ila kidogo tu.




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2018-08-01 Topic: Tawhid Main: Dini File: Download PDF Views 930

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 ai web app    👉2 Bongolite - Game zone - Play free game    👉3 web hosting    👉4 Simulizi za Hadithi Audio    👉5 Kitau cha Fiqh    👉6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana:

MAANA NA HUKUMU YA TAJWIDI

Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa

Soma Zaidi...
Kujiepusha na kuua nafsi bila ya Haki

Kuua nafsi bila ya Haki, ni kuiua nafsi isiyo na kosa linalostahiki hukumu ya kifo.

Soma Zaidi...
Maswali juu ya nguzo za Imani

Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Mtazamo wa kikafiri juu ya maana ya dini.

Maana ya dini kwa mujibu wa makafiri ina utofauti mkubwa na vile ambavyo uislamu unaamini kuhusu dini.

Soma Zaidi...
Humtegemea Mwenyezi Mungu peke yake

Hawamuogopi au kumtegemea yeyote kinyume na Mwenyezi Mungu.

Soma Zaidi...
jamii muongozo

Haja ya Mwongozo kutoka kwa Allah (s.

Soma Zaidi...
Nguzo za Imani kwa mujibu wa mafunzo ya kiislami.

Makala hii inakwenda kukufundisha kuhusu nguzo sita za imani katika Uislamu.

Soma Zaidi...
Tofauti kati ya Quran na vitabu vingine vya mwenyezi Mungu

Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...