Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat Al-Imran

Na kuwapambanua wale waliokuwa wanafiki.

Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat Al-Imran

Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat Al-Imran


Na kuwapambanua wale waliokuwa wanafiki. Nao waliambiwa: "Njooni mpigane katika njia ya Mwenyezi Mungu au mzuie (maadui pamoja na sisi)" Wakasema: "Tungejua kuwa kuna kupigana bila ya shaka tungelikufuateni." Wao siku ile walikuwa karibu na ukafiri kuliko na Uislamu (japokuwa siku zote wakidhihirisha Uislamu wa uwongo). Wanasema kwa midomo yao yasiyokuwa nyoyoni mwao. Na Mwenyezi Mungu anajua vyema (yote) wanayoyaficha. (3:167)


Wale waliosema juu ya ndugu zao - na (wao wenyewe) wamekataa kwenda (hawakwenda) vitani: "Wangalitutii wasingeuawa." Sema: "Jiondoleeni mauti (nyinyi) wenyewe msife maisha ikiwa mnasema kweli." (3:168)



"Wala usiwadhani wale waliouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni wafu (maiti). Bali wahai, wanaruzukiwa kwa Mola wao." (3:169).
Kutokana na aya hizi tunapata sifa za wanafiki zifuatazo:



(i)Hawako tayari kujitoa muhanga kupigania dini ya Allah (s.w) isimame katika jamii au kuihami isiangushwe baada ya kusimama kwake.



(ii)Wanasema kwa midomo yao yasiyokuwa nyoyoni mwao. Baada ya mapambano dhidi ya maadui wa Dini ya Allah (s.w) kwisha, wanafiki hujikosha kwa kusema uwongo kuwa hawakuwa na taarifa juu ya mapambano ya Waislamu dhidi ya maadui zao, vinginevyo wangelikuwa Pamoja katika vita hivyo hali ya kuwa walijificha wasiende vitani kwa kuogopa kufa.



(iii)Huwabeza na kuwalaumu wale wanaouliwa au kupata misuko suko katika kuupigania Uislamu.
Katika aya ya 168 na 169 (3:168-1 69), Allah (s.w) anawasuta wanafiki na kuwakatisha tamaa kuwa mtu hafi kwa kuwa amepigania dini ya Allah (s.w), bali kila mtu atakufa kwa ajali yake aliyopangiwa:



“… Sema: (uwaambia wanafiki): "Jiondosheeni mauti (nyinyi wenyewe msife milele) ikiwa mnasema kweli."



Pia Allah (s.w) anawakatisha tamaa wanafiki na kuwatumainisha waumini kuwa hapana jambo lililozuri na bora kwa mtu kuliko kufa katika njia ya Allah (s.w) (kufa shahidi).




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Jifunze Main: Dini File: Download PDF Views 672

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi    👉2 Kitabu cha Afya    👉3 Simulizi za Hadithi Audio    👉4 Bongolite - Game zone - Play free game    👉5 Kitau cha Fiqh    👉6 Madrasa kiganjani   

Post zinazofanana:

(xvi)Huepuka ugomvi na mabishano

Waumini wa kweli huepuka kabisa tabia ya ugomvi na mabishano.

Soma Zaidi...
Maswali juu ya hadithi

Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya)

Soma Zaidi...
Kitabu Cha Darsa za dua

Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet.

Soma Zaidi...
(ix)Wenye kuhifadhi swala

Waumini wa kweli waliofuzu huhifadhi swala kwa kutekeleza kwa ukamilifu shuruti zote za swala nguzo zote za swala na huswali kama alivyoswali Mtume (s.

Soma Zaidi...
(xiii)Huwa muaminifu

Waumini wa kweli waliofuzu huchunga amana.

Soma Zaidi...
HADITHI YA MZEE WA KWANZA NA MBUZI

Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA MZEE WA KWANZA NA MBUZI WAKE.

Soma Zaidi...