Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat al-Baqarah

Na katika watu, wako (wanafiki) wasemao: "Tumemwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho"; na hali ya kuwa wao si wenye kuamini.

Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat al-Baqarah

Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat al-Baqarah


Na katika watu, wako (wanafiki) wasemao: "Tumemwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho"; na hali ya kuwa wao si wenye kuamini. Wanatafuta kumdanganya Mwenyezi Mungu na wale walioamini, lakini hawadanganyi ila nafsi zao; nao hawatambui. Nyoyoni mwao mna maradhi, na Mwenyezi Mungu amewazidishia maradhi. Basi watakuwa na adhabu iumizayo kwa sababu ya kule kusema kwao uwongo. (2:8-10)


Na wanapoambiwa: "Msifanye uharibifu ulimwenguni." Husema "Sisi ni watengenezaji. "Hakika wao ndio waharibuji, laini hawatambui.Na wanapoambiwa: "Aminini kama walivyoamini watu" Husema"Oh! Tuamini kama walivyoamini wale wapumbavu?" Hakika wao ndio wapumbavu lakini hawajui. (2:11-1 3)



Na wanapokutana na walioamini husema: "Tumeamini"; na wanapokuwa peke yao kwa mashetani wao husema: "Hakika sisi tu pamoja nanyi, tunawacheza shere tu." Mwenyezi Mungu atawalipa shere yao na kuwawacha katika upotofu wao wakitangatanga ovyo. Hao ndio waliokhiari upotofu kuliko uongofu; lakini biashara yao haikupata faida wala hawakuwa wenye kuongoka. (2:14-1 6)


Mfano wao (hawa wanafiki) ni kama mfano wa wale (wasafiri waliokumbwa na kiza) wakakoka moto, (na) ulipowaonyesha yaliyo pembezoni mwao, Mwenyezi Mungu aliiondoa nuru yao hiyo na kuwawacha katika viza; hawaoni. (2:17)


Viziwi, mabubu, vipofu; kwa hivyo hawatarejea. (2:18)


Au (mfano wao pia) ni kama mvua kubwa itokayo mawinguni; ndani yake mkawa mna viza na radi na umeme; wakawa


wakitia vidole vyao masikioni mwao kwa ajili ya mingurumo, kwa kuogopa kufa; (na kufanya hivyo hawakusaidii kitu). Na Mwenyezi Mungu anawajua vyema hao makafiri. (2:19)


Unakaribia umeme huo kunyakua macho yao; kila unapowaangazia huenda ndani yake na unapowafanyia giza husimama. Na Mwenyezi Mungu angependa angaliondoa kusikia kwao na kuona kwao. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kuweza juu ya kila kitu. (2:20)



Kutokana na aya hizi tunajifunza sifa za wanafiki zifuatazo:
(i)Kuonesha imani ya uongo. Katika vinywa vyao wanadai kuwa ni waumini lakini katika nafsi zao na matendo yao wanaikanusha imani yao.
(ii)Wanauchukia Uislamu nyoyoni mwao, na wanazidi kuuchukia kila Uislamu unavyosonga mbele.
(iii)Hufanya uharibifu katika nchi huku wakidai kuwa wanatengeneza.
(iv)Huwabeza waumini wa kweli wanaofuata Uislamu vilivyo.
(v)Hawana msimamo. Wanataka wapate maslahi ya Uislamu na wakati huo huo wawe pamoja na makafiri.
(vi)Wanawacheza shere Waislamu.
(vii)Kwa mujibu wa mfano uliopigwa katika aya ya 17 (2:17) wamekhiyari kupotea baada ya kujiwa na mwongozo (nuru).
(viii)Kwa sababu wamedhamiria upotevu badala ya uongofu kwa ajili ya maslahi ya dunia, hata ukiwaita kwenye uongofu hawawezi kuja. Wamefananishwa na watu wenye vilema vitatu kwa pamoja vya uziwi, ububu na upofu. Hivyo hawawezi kusikia neno la mwenye kuadhini wala la mwenye kukimu.


Kwa mujibu wa mfano uliopigwa katika aya ya 19 na 20 (2:19-20), wanafiki wanatamani matunda yatokanayo na kusimama kwa Uislamu katika jamii lakini hawako tayari kukabiliana na changamoto zinazotokana na mchakato mzima wa kusimamisha Uislamu katika jamii. Wanafurahia matunda yanayotokana na mvua nzuri za masika lakini hawako tayari kukabiliana na radi, ngurumo na umeme vinavyoandamana na mvua hizo.




                   


Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 126

Post zifazofanana:-

JE NITUMIE SIMU YANGU WAKATI INACHAJI?
Watu wengi wamekuwa wakijiuliza swali hili. Soma Zaidi...

dua ya kuomba jambo ufanikiwe
hii ni damna ya kuomba dua ukubaliwe, dua ya kuomba jambo ufanikiwe Soma Zaidi...

Qur-an Yenyewe Inajieleza kuwa ni Ufunuo Kutoka kwa Allah (s.w)
(ii)Qur-an Yenyewe Inajieleza kuwa ni Ufunuo Kutoka kwa Allah (s. Soma Zaidi...

hadithi ya 8
' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ': "' ' ' ' ' ?... Soma Zaidi...

Sababu za maumivu ya tumbo
hapa utajifunza maradhi mbalimbali yanatopelekea kuwepo kwa maumivu ya tumbo Soma Zaidi...

uwanja wa burudani
Jifunze mengi kuhusu Afya, kuwa nasi kwenye makala hii hadi mwisho. Soma Zaidi...

Taratibu za ndoa ya kiislamu, hatua kwa hatua
Soma Zaidi...

Haki na wajibu kwa jirani
Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Chungwa
Soma Zaidi...

Dalili za vidonda vya tumbo, matibabu na dawa zake, sababu za kutokea kwake
Utajifunza chanzo cha vidonda vya tumbo, dalili zake, dawa na matibabu yake pamoja na njia za kujilinda na vidonda vya tumbo Soma Zaidi...

Siku za kupata mimba
Nitakujulisha siku ya kupata mimba na sifa zake, na namna ya kuweza kuitafuta Soma Zaidi...

TOFAUTI KATI YA MAKATOZO NA MAAMRISHO KATIKA SUNNAH
' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ': ' ' ' ' ' ' ' ' ': "'... Soma Zaidi...