image

Sababu ya uislamu kuwa ndiyo dini sahihi pekee

Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

  1. Sababu Ya Uislamu Kuwa Ndiyo Dini Sahihi Pekee. 

Uislamu ndio dini pekee inayostahiki kuchaguliwa na kufuatwa kama muongozo sahihi wa maisha na watu wote kwa sababu zifuatazo;

 

  1. Uislamu unaeleza ukweli juu ya maumbile na nafasi ya mwanaadamu hapa Duniani;

Uislamu unaeleza lengo la kuumbwa mwanaadamu kuwa ni ibada na kumtumikia Mwenyezi Mungu na kuwa msimamizi wa sheria na hukumu zake hapa ulimwenguni ili kupata radhi zake.

Rejea Qur’an (51:56) na (2:29).

 

  1. Sheria na kanuni za Uislamu zinaendana na kanuni za kimaumbile;

Uislamu ndiyo dini pekee inaenda na kuzingatia kanuni na taratibu zote za kimaumbile za kibailojia kifizikia na kikemia ya viumbe vyote vilivyo na visivyo hai ikiwa ni pamoja na maumbile au mazingira yanayotuzunguka.

Rejea Qur’an (3:83) na (30:30).

 

  1. Uislamu ndio dini inayotosheleza matashi yote ya mwanaadamu kimwili na kiroho;

Uislamu ni dini inayotoa muongozo namna ya mtu kumiliki hisia zake na kuendea mambo katika hali tofauti tofauti kama vile wakati wa furaha, shida, huzuni, misiba, n.k.

Rejea Qur’an (2:155-157).

 

  1. Uislamu ni njia kamili ya maisha;

Ni Uislamu pekee ndio mfumo kamili wa maisha ya kila siku ya mwanaadamu katika fani na nyanja zote za kibinafsi na kijamii kama vile kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni.

 

  1. Uislamu una ibada maalum za kumjenga mwanaadamu kimaadili;

Uislamu umeweka muongozo katika kumuadilisha mwanaadamu kupitia ibada maalum kama vile swala, funga, hija, kutoa zakat na sadaqat na zinginezo za sunnah.

 

  1. Uislamu ni dini ya walimwengu wote na wa nyakati zote;

Uislamu umekuwa ni mwongozo wa maisha tangu binaadamu wa kwanza hadi wa mwisho katika Nyanja zote za maisha bila kujali taifa, ukoo, rangi na hadhi ya watu.

Rejea Qur’an (42:13).

 

  1. Uislamu ni dini ya kusimamia haki, uadilifu na usawa;

Ni dini ya Uislamu ndiyo inayotoa na kusimamia kwa usawa na uadilifu haki, hukumu na adhabu zote kwa watu wote bila ya upendeleo na ubaguzi wa rangi, taifa, hadhi na ukoo.

Rejea Qur’an (103:1-3), (9:33), (61:9) na (17:105).





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1184


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Upinzani Dhidi ya Ujumbe wa Mtume(s.a.w)
Mtume(s. Soma Zaidi...

Nabii Ibrahiim(a.s) Kuulingania Uislamu kwa Jamii Yake
Nabii Ibrahim(a. Soma Zaidi...

Vita vya uhudi
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Mtume Muhammad s.a.w analelewa na Babu yako ikiwa na umri wa miaka 6
Sura na historia ya Mtume Muhammad s.a. w sehemu ya 9. Soma Zaidi...

NI IPI FAMILIA YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) NA NI IPI NASABA YAKE, UKOO WAKE NA KABILA LAKE
FAMILIA YA MTUME (S. Soma Zaidi...

Mambo ya Msingi Aliyofanya Mtume(s.a.w) Katika Kuanzisha Dola ya Kiislamu Madinah.
Mambo ya Msingi Aliyofanya Mtume(s. Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII YUSUFU
Soma Zaidi...

Maandalizi ya hijrah ya mtume na waislamu kuhamia madinah
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Daud(a.s)
Kutokana historia ya Nabii Daud (a. Soma Zaidi...

Nabii Isa(a.s) Azungumza Akiwa Mtoto Mchanga
Maryam akamtwaa mwanawe, akaenda naye kwa jamaa zake amembeba. Soma Zaidi...

Mapambano ya Dola ya kiislamu dhidi ya maadui wa kikristo (warumi) wakati wa Mtume
Soma Zaidi...

HISTORIA NA MAISHA YA NABII ISMAIL(A.S)
Ismail(a. Soma Zaidi...