image

Sababu za kushuka surat al adiyat

Sura hii iliposhuka ilikuwa kama imekuja kuwasuta Wanafiki waliokuwa wakizungumzahabari za uongo kuhusu jeshi alilolituma Mtume wa Allah.

Ibni Mas'ud, Jabir, Al-Hasan, Ikrama na Ataa wanasema ya kuwa sura hii ilishuka Makka.

 

Dhabhan ni namna  moja ya mbio za wanyama (Mufradat);  tena ni sauti maalumu inayotoka katika vifua  vya farasi wanapokimbia (Akrab). Wakimbiaji wanaotweta, mradi wa maneno haya ni farasi.

 

 Abdullah bin Abbas na wanazuoni wengine kama Mujahid, Ikrama, Ataa, Qatada na Dhahhaak wote  wanakubali ya kuwa mradi ni farasi.  Na lugha ya Kiarabu pia inasaidia maana hii.

 

Iliposhuka sura hii watu walikuwa na ngamia, na hakukuwa sana desturi ya kuwatumia farasi.  Lakini Mwenyezi Mungu kwa kuiteremsha Aya "Wakimbiaji wanaotweta" akabashiri ya kuwa hawa watu wa Makka  wapandao ngamia siku moja watakuwa wapandao farasi.  

 

Na kweli, baadaye desturi ya kuwapanda farasi ilienea sana, na farasi wakazidi kabisa, na Waislamu wakawa wakimbiaji juu ya farasi katika matukio ya vita na amani.  

 

Kwa neno zima, Aya hii inajulisha ya kuwa Waislamu walikuwa na shauku na huba sana ya kuitumikia dini, hata wakawabana maadui waliokuwa na nguvu nyingi na silaha kubwa.  Wao walikuwa wanakwenda mbio na wakiwakimbiza farasi kwa kutoa sadaka maisha yao. 

 

Sababu za kushuka sura hii: 

Muqatil amesema kuwa Mtume s.a. w Alituma jeshi liende kabila la bani Kinana na akamteua Mundhir bin Amr al Ansariy awe kama kiongozi wa jeshi hilo. 

 

Sasa muda mrefu umepita yapata mwezi habari za jeshi hili hazikufika Madina. Wanafiki wakaanza kutangaza kuwa wotevwaneuliwa. 

 

Hapo ndipo Allah akatoa taarifa za jeshi hili na kisha ikashuka sura hii. 





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1906


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Sababu za kushuka kwa Surat al-Kawthar na fadhila zake
SURATUL-KAUTHAR Imeteremshwa maka, na sura hii imeshuka kwa sababu al-aAs ibn Waail. Soma Zaidi...

Historia ya kushuka kwa quran
Soma Zaidi...

sura ya 11
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...

idadi sahihi kati ya sura zilizoshuka Makka na zile za madina
A. Soma Zaidi...

Sababu za kushuka kwa surat al_ikhlas (qul huwallahu) na fadhila zake
3. Soma Zaidi...

MAANA YA Quran
Maana na majina ya Quran Maana ya Wahyi. Soma Zaidi...

ASBAB-NUZUL SABABU ZA KUSHUKA AYA NA SURA KWENYE QURAN
ASBAB NUZUL SABABU ZA KUSHUKA AYA NA SURA KWENYE QURAN Quran imeteremka kwa muda wa miaka 23 kidogokido. Soma Zaidi...

HUKUMU ZA QALQALA
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...

Sababu za kushuka surat al Quraysh
Qurayh ni jina la kabila la Mtume Muhammad S.A.W. Sura hii itakwenda kukujulisha neema ambazo Maquraysh wamepewa na hawataoewa wao wowote baada ya wao. Soma Zaidi...

AINA ZA MADA YAANI KUVUTA KWENYE USOMAJI WA QURAN: MADD (Al-Maddul-Far-’iy), Maddul-Jaaiz Al-Munfaswil, Maddul-Liyn,
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...

Wanaoongozwa na wasioongozwa na quran
Soma Zaidi...

quran na sayansi
YALIYOMONENO LA AWALI1. Soma Zaidi...