image

Sababu za kushuka surat al alaqa

Asbsb nuzul surat al alaqa, sababu za kushuka surat alaqa. Sura hii imeshuka Makka na ina aya 19. Ni sura ya 96 katika mpangilio wa Quran.

{بسم الله الرحمان الرحيم}

اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ ﴿١﴾ خَلَقَ الْإِنسَانَ مِنْ عَلَقٍ ﴿٢﴾ اقْرَأْ وَرَبُّكَ الْأَكْرَمُ ﴿٣﴾ الَّذِي عَلَّمَ بِالْقَلَمِ ﴿٤﴾ عَلَّمَ الْإِنسَانَ مَا لَمْ يَعْلَمْ ﴿٥

Sura hii imeteremka Maka kwa makubaliano ya Mufasiruna wote. Pia Jamhuri ya mufasirun wanakubaliana kuwa sura hii ndio ya kwanza kushuka. 

 

Hata hivyo zipo baadhi ya kauli kuwa sura ya kwanza kushuka ni Yaa ayuha al mudathir, hii kauli amesema Jabir Ibn Abdllah. Na imesemwa pia sura ya kwanza ni alhamdu amesema kauli hii Abu Maisarah na pia imesemwa sura ya kwanza ni aya ya 151 ya surat al anam . lakini kauli zote hizi sio sahihi. Iliyo sahihi ni kuwa sura ya jwanza ni surat al 'alaq

 

أَرَءَيْتَ ٱلَّذِى يَنْهَىٰ
[Surah Al-`Alaq: 9]

Aya hii na zinazofuata zinamzungumzia Abujahal mmoja katika maadui wa Mtume Muhammad wakati bado yupo Makkah. 

 

Abujahal alikuwa akimuudhi Mtume hakuishia hapo pia alikuwa akimzuia kufanya ibada. Sio hivyo tu pia alikuwa akizuia watu wengine wasiende kwa Mtume wala kukutana nae. 

 

Abujahal alikufa kwenye vita vya Badri na aliburutwa kifudifudi kuelekea kwenye shimo la kuzikia. Na wenzie wengine kama Abulahab alikufa siku chache baadaye. 

 

Allah anasema: 

9. Umemwona yule anaye mkataza 
10 . Mja anapo sali? 
11. Umeona kama yeye yuko juu ya uwongofu? 
12. Au anaamrisha uchamngu? 
13. Umeona kama yeye akikanusha na anarudi nyuma? 
14. Hajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anaona? 
15. Kwani! Kama haachi, tutamkokota kwa shungi la nywele! 





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2397


Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 kitabu cha Simulizi     👉5 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Aina za Madd far-iy
Mada zipo katika makundi mawili ambayo ni madda far-iy na mdada twab-iy. Soma Zaidi...

Mtume Muhammad hakujuwa kusoma wala kuandika ni hoja na kuna hekima zake
(i)Mtume Muhammad (s. Soma Zaidi...

Sababu za kushuka surat Ikhlas
Surat Ikhlas ni katika sura za kitawhid ambazo zilishuka miaka siku za mwanzoni mwa utume. Sura hii imekuja kujibu maswali mengi kuhusu Allah ikiwemo, Allah ni nani? Soma Zaidi...

Sababu za kushuka surat al alaqa
Asbsb nuzul surat al alaqa, sababu za kushuka surat alaqa. Sura hii imeshuka Makka na ina aya 19. Ni sura ya 96 katika mpangilio wa Quran. Soma Zaidi...

Wanaoongozwa na wasioongozwa na quran
Soma Zaidi...

Sababu za kushuka kwa surat al_ikhlas (qul huwallahu) na fadhila zake
3. Soma Zaidi...

Muhammad hakufundishwa quran na padri Bahira
Soma Zaidi...

Sababu za kushuka Surat al Kafirun
Sura hii imekuja kukata rai ya Makafiri wa Makka kuhusu ibada ya ushirika. Hivi leo tungesema kuhusu dini mseto. Soma Zaidi...

Quran haikunukuliwa kutoka kwa mayahisdi na wakristo
(vi)Madai Kuwa Mtume (s. Soma Zaidi...

Sababu nyengine zilopelekea kushushwa kwa suratul ikhlas
Soma Zaidi...

Hukumu za Tajwid katika usomaji wa bismillah (basmalah)
Hapa utajifunza kanuni za tajwid katika kusoma bismillah au basmalah. Soma Zaidi...

Madai ya makafiri dhidi ya quran na hoja zao
Soma Zaidi...