image

Sababu za kushuka surat al bayyinah

Asbab nuzul surat al bayyinh. Sura hii imeteremka Madina na ina aya nane.

Surat al bayyinah imeshuka Madina kwa maelezo ya Jamhuri ya wanazuoni akiwemo Ibn Abas.   Hata hivyo wapo ambao wamesema imeshuka Makka kwa kauli ya Yahya Ibn Sallaam (Tafsir qurtub). 

 

Sura hii iliposhuka Mtume s. a.w aliamrishwa amsomee Ubayya. 

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ لِأُبَيِّ بْنِ كَعْبٍ: "إِنَّ اللَّهَ أَمَرَنِي أَنْ أَقْرَأَ عَلَيْكَ: " لَمْ يَكُنِ الَّذِينَ كَفَرُوا " قَالَ: وَسَمَّانِي لَكَ؟ قَالَ: "نَعَمْ". فَبَكَى.
وَرَوَاهُ الْبُخَارِيُّ، وَمُسْلِمٌ، وَالتِّرْمِذِيُّ، وَالنَّسَائِيُّ، مِنْ حَدِيثِ شُعْبَةَ، بِهِ  .

 

Imepokewa hadithi kutoka kwa Anas Ibn Malik kuwa amesema Mtume s.a. w kumwambia Ubayya Ibn Ka‘ab "Hakika Allah ameniamuru nikusomee (sura hii)  lam yakun ladhiina kafaruu" akasema Ubayya "na nimetajwa kwa jina? " akasema Mtume "naam" hapo akalia kwa furaha (Bukhari na Muslim). 

 

Sababu za kushuka sura hii

Hakuna tukio maalumu lilopelekea kushuka sura hii. Hata hivyo sura ipo wazi inaonyesha dhahiri kike ambacho kilikuwa kikiaminiwa na ahalul kitab na washirikina. 

 

Sura inaeleza kuwa hapo awali Ahalul kitab na washirikina walikuwa wakiamini kuwa atakuja mtume wa Mwisho. Mahubiri haya yalikuwa yakitolewa na Mayahudi na Wakristo kuwaambia waumini wao na waarabu. 

 

Lakini Mtume wa mwisho alipokuja wakamkataa na kumpinga. Alikuwa wakipinga ukweli kwa sababu ya chuki zao. 

Allah anasema katika sura hii: - 

(وَمَا تَفَرَّقَ ٱلَّذِینَ أُوتُوا۟ ٱلۡكِتَـٰبَ إِلَّا مِنۢ بَعۡدِ مَا جَاۤءَتۡهُمُ ٱلۡبَیِّنَةُ)
[Surah Al-Bayyinah 4]

Wala hawakufarikiana walio pewa Kitabu ila baada ya kuwajia hiyo bayana.

 

Mwisho kwa uovu huu wa kufarikiana na haki baada ya kuwajia bayana (uwazi na ukweli wa mambo) Allah amewaahidi kukaa maisha ya Motoni milele. 

 

Fadhila za sura hii

kuhusu fadhila za sura hii,  kuna hadithi nyingi lakini zinatikiwa shaka usahihi wake. Miongoni mwazo kuna inayosema kuwa sura hii haisomwi na mtu mnafiki wala mtu ambaye ana shaka juu ya Mwenyezi Mungu na kuwa Malaika wanaosoma sura hii na mwenye kuisoma Allah atampa Malaina wamuhifadhi…. Hadithi hii sio sahihi. Angalia Matini ya hadithi hapo chini. 

 

عَنْ أَبِي الدَّرْدَاءِ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى الله: (لو يعلم الناس ما في [لَمْ يَكُنِ [الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ،، لَعَطَّلُوا الْأَهْلَ وَالْمَالَ، فَتَعَلَّمُوهَا) فَقَالَ رَجُلٌ مِنْ خُزَاعَةَ: وَمَا فِيهَا مِنَ الْأَجْرِ يَا رَسُولَ اللَّهِ؟ قَالَ: (لَا يَقْرَؤُهَا مُنَافِقٌ أَبَدًا، وَلَا عَبْدٌ فِي قَلْبِهِ شَكٌّ فِي اللَّهِ. وَاللَّهِ إِنَّ الْمَلَائِكَةَ المقربين يقرءونها  Ù…نذ خلق الله السموات وَالْأَرْضَ مَا يَفْتُرُونَ مِنْ قِرَاءَتِهَا. وَمَا مِنْ عَبْدٍ يَقْرَؤُهَا إِلَّا بَعَثَ اللَّهُ إِلَيْهِ مَلَائِكَةً يَحْفَظُونَهُ فِي دِينِهِ وَدُنْيَاهُ، وَيَدْعُونَ لَهُ بِالْمَغْفِرَةِ وَالرَّحْمَةِ (. قَالَ الْحَضْرَمِيُّ: فَجِئْتُ إِلَى أَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ نُمَيْرٍ، فَأَلْقَيْتُ هَذَا الْحَدِيثَ عَلَيْهِ، فقال: هذا قَدْ كَفَانَا مَئُونَتَهُ، فَلَا تَعُدْ إِلَيْهِ. قَالَ ابْنُ الْعَرَبِيِّ:" رَوَى إِسْحَاقُ بْنُ بِشْرٍ الْكَاهِلِيُّ عن مالك ابن أَنَسٍ، عَنْ يَحْيَى بْنِ سَعِيدٍ، عَنِ ابْنِ الْمُسَيَّبِ: عَنْ أَبِي الدَّرْدَاءِ، عَنِ النَّبِيِّ ï·º: (لَوْ يَعْلَمُ النَّاسُ مَا فِي [لَمْ يَكُنْ [الَّذِينَ كَفَرُوا لَعَطَّلُوا الْأَهْلَ وَالْمَالَ وَلَتَعَلَّمُوهَا) . حَدِيثٌ بَاطِلٌ

Angalia Tafsir Qurtub

 

Khabari njema kwa waumini

Mwisho sura inatia habari za furaha kuwa waliamini na kufanya vitendo vizuri yaani amali njema malipo yao ni pepo na wakae humo milele. 

 





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2060


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Quran si njozi za mvurugano alizoota Mtume Muhammad
(ii)Dai kuwa Qur-an ni zao la njozi za Mtume (s. Soma Zaidi...

Qur-an Yenyewe Inajieleza kuwa ni Ufunuo Kutoka kwa Allah (s.w)
(ii)Qur-an Yenyewe Inajieleza kuwa ni Ufunuo Kutoka kwa Allah (s. Soma Zaidi...

Mpangilio wa quran ni wa kipekee na uliotumia ujuzi mkubwa
Soma Zaidi...

quran na sayansi
YALIYOMONENO LA AWALI1. Soma Zaidi...

quran na sayansi
QURANI KATIKA ZAMA ZA SAYANSI NA TEKNOLOJIAAsalaalaamu alykum warahmatullah wabarakaatuh. Soma Zaidi...

Nini maana ya Iqlab katika hukumu za tajwid
Hapa utajifunza maana ya iqlab katika usomaji wa Quran kwa tajwid Soma Zaidi...

ADABU ZA KUSOMA QURAN
Adabu wakati wa kusoma quran 1. Soma Zaidi...

Historia ya kushuka kwa quran
Soma Zaidi...

Jinsi Mtume Muhammad (s.a.w) alivyoipokea Qur-an:
(iii)Jinsi Mtume Muhammad (s. Soma Zaidi...

HUKUMU ZA IDGHAM
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...

Fadhila za kusoma surat al Imran
Post hii itakufundisha fadhila na faida za kusoma surat al Imran Soma Zaidi...

Sababu nyengine zilopelekea kushushwa kwa suratul ikhlas
Soma Zaidi...