image

Sababu za kushuka surat al-Fiyl

Al fiyl ni neno la Kiarabu lenye maana ya tembo. Sura hii inazungumziakisa cha jeshi lenye tembo. Jeshi hili lilikuwa na nia ya kuvunja al qaaba

Sababu za kushuka kwa surat al-Fiil

SURAT AL-FIIL
Sura hii imeteremshwa Makkah na ina Aya Sita pamoja na Basmallah. Sura hii imeshuka ili kueleza kuhusu tukio la kuangamizwa kwa jeshi la tembo. Na hii ni katika sura ambazo zinataja neema ambazo wamepewa Maquraysh, nao ni ule ushindi dhidi ya Makafiri walotaka kuvunja Al-Ka’abah. Tukio hili limeelezwa kwa kirefu kwenye vitabu vya Sirah na hapa nitaleta kwa ufupi zaidi


 

Kiongozi mmoja wa kiyemeni aliyetambulika kwa jina la Abrah aliona waarabu kutoka maeneo mbalimbali wanafunga misafara kuelekea Makkah kwa lengo la kwenda kuhiji. Hivyo akaamuwa kujenga kanisa kubwa sana ambalo alifikiri kuwafanya waarabu wasiende Makkah ila waende kuhiji kwenye kanisa lake. Kulikuwa na kijana mmoja kutoka katika kabila la Kinana alifahamu jambo hili la Abraha. Hivyo akaingia kwenye kanisa wakati wa usiku kisha akachafua ukuta wa kanisa kwa kuupaka vinyesi. Abraha alipolijuwa jambo hili akaandaa jeshi kubwa sana ili akaivunje Al-ka’aba. Jeshi la Abraha lilikuwa na washujaa elfu sitini (60,000). kisha akachaguwa tembo aliye mkubwa ndio akampanda yeye. Katika jeshi hili kulikuwa na tembo kati ya tisa mpaka kumi na tatu. (9-13)


 

Safari ya Abraha iliendelea mpaka akafika sehemu inayoitwa Magmas. Na hapo ndipo akaliweka sawa jeshi lake na akaliweka tayari kwa kuingia Makkah. Akaendelea mpaka akafika sehemu iitwayo Bonde la Muhassar bonde hili lipo kati ya Muzdalifah na Mina. Na hapo ndipo tembo wa abraha akakataa kuendelea na safari. Tembo alipiga magoti na kukaa chini, na kugoma kabisa kuelekea upande wa Makkah. Basi akimuelekeza upande mwingine anakubali lakini pindi akimuelekeza upande wa Makkah anagoma kabisa.


 

Na hapo ndipo Allah alipoleta jeshi la ndege waliobeba vijiwe vya moto na kuwapiga nvyo jeshi la Abraha. Ndege hawa kila mmoja alibeba vijiwe vitatu, kijiwe kimoja kwenye mdomo na viwili kwenye miguu yao. Kila kijiwe kiliuwa mtu katika jeshi la Abraha. Kuna wengine walikufa palepale na wengine walikimbia na kufia mbele ya safari. Abraha alibahatika kukimbia kwani alijeruhiwa vibaya, alipofika sehemu iitwayo San’a hali yake ikawa mbaya zaidi na akafariki.


 

Kwa upande mwingine wakazi wa Makkah walikimbia mji na kujificha kwenye majabali. Na huu ni ushauri walopewa na kiongozo wao Abdul Al-Muttalib. Baada ya maombi waloyaomba kwa Allaha na hatimaye wakamuachia Allah ailinde Nymba yake na wao wanusuru maisha yao. Basi jeshi la Abraha baada ya kuangamizwa wakazi wa Makkah wakarudi majumbani kwao wakiwa salama.


 

Tukio hili lilitokea mwezi wa Muharram siku hamsini aua hamsini na tano kabla ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w) ambapo ni sawa nan Mwezi wa Pili au mwanzoni mwa Mwezi wa Tatu mwaka 571 B.K. na hii ilikuwa ni zawadi kutoka kwa Allah kwenda kwa mtume wake na watu wa familia yake. Na hapo ndipo Nyumba ya Allah yaani Al-ka’aba ilipata maarufu kwa utukufu wake. Na mwaka huu waarabu wakauita mwaka wa Tembo





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1693


Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 Madrasa kiganjani     ๐Ÿ‘‰2 kitabu cha Simulizi     ๐Ÿ‘‰3 Kitau cha Fiqh     ๐Ÿ‘‰4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

quran na sayansi
YALIYOMONENO LA AWALI1. Soma Zaidi...

Saratul-asr 103
Quran (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

HIKUMU YA BASMALLAH YAANI KUSOMA BISMILLAH
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...

Sababu za kushuka surat al Zilzalah
surat Zalzalah ni sura ya 99 katika mpangilio wa Quran, na ina aya 8. Sura hii imeteremshwa Madina ila pia kuna kauli zinathibitisha kuwa ni ya Makkah. Katika hadithi iliyopewa daraja la hassan na Imam Tirmidh Mtume S.A.W amesema kuwa kusoa surat Zilzalah Soma Zaidi...

Sababu za kushuka kwa surat An-Nasr (idhaa jaa)
SURATUN-NASR Sura hii imeteremka wakati Mtume (s. Soma Zaidi...

Sababu za kushuka surat al bayyinah
Asbab nuzul surat al bayyinh. Sura hii imeteremka Madina na ina aya nane. Soma Zaidi...

surat al mauun
SURATUL-MAMโ€™UUN Imeteremshwa Maka, anasimulia Ibn Jurayj kuwa Abuu Sufyan ibn Harb alikuwa na kawaida ya kuchinja ngamia wawili kila wiki, hivyo siku moja yatima mmoja alikuja kwake na kumlilia shida, na hakumsaidia kwa chochote na hatimaye akampiga yat.. Soma Zaidi...

quran na sayansi
QURANI KATIKA ZAMA ZA SAYANSI NA TEKNOLOJIAAsalaalaamu alykum warahmatullah wabarakaatuh. Soma Zaidi...

Naman ya kuiendea quran na kuifanyia kazi baada ya kuisoma
Soma Zaidi...

Fadhila za kusoma surat al Kahaf siku ya Ijumaa
Je unajuwa ni kwa nini unatakiwa usikose kusoma surat al Kahaf siku ya ijumaa. Makala hii itakujibu swali hili Soma Zaidi...

Sababu za kushuka surat al qadir
Asbab nuzul surat al qadi. Hii ni sura ya 97 katika mpangilio wa mashaf. Surat al qadir imeteremshwa Madina na ina aya 5. Soma Zaidi...

HUKUMU ZA MIIM YENYE SAKINA
SURA YA NNE HUKUMU ZA MIYM YENYE SAKNA HUKUMU ZA MIYM SAKINA: Mym sakina ni miym ambayo haina iโ€™rab ( ู…ู’). Soma Zaidi...