image

Sababu za kushuka surat al Zilzalah

surat Zalzalah ni sura ya 99 katika mpangilio wa Quran, na ina aya 8. Sura hii imeteremshwa Madina ila pia kuna kauli zinathibitisha kuwa ni ya Makkah. Katika hadithi iliyopewa daraja la hassan na Imam Tirmidh Mtume S.A.W amesema kuwa kusoa surat Zilzalah

Asbab Nuzul Surat Zilzalah

Ama kuhusu sababu za kushuka sura hii, hakuna nukuu za kutosha kuonyesha hasa tukio ambalo lilitokea hata sura hii ikashushwa. Hata hivyo kutokana na maelezo ya Sa'id bin Jubair ni kuwa baada ya kushuka aya ya 8 ya surat Al insan watu walidhani kuwa wak=liotoa sadaka kidogo sana hawatalipwa na wengine wakadhani kuwa dhambi ndogo wanazozifanya hawataadhibiwa, hivyo Allah akashuka aya 7 na 8 katika surat al zilzalah.

 

Kutokana na maelezo Maelezo ya Sura hii kuwa ukifanya dhambi iwe ndogo kiasi gani utalipwa malipo yake, na ukifanya wema mdogo kiasi gani pia utalipwa. Ama kuhusu wema kuna maelezo mengine zaidi ni kuwa Quran inasibitisha kuwa wema hulipwa kwa marakumi zaidi ama zaidi ya hapo. Yaani mfano umetenda wema mmoja, basi Allah atazidisha kwa kumi malipo yake. Na huwenda akazidisha zaidi ya hapo hata mara mia saba kama Surat Al Baqarah inavyoeleza ama zaidi na zaidi.

 

Imesimuliwa Kutoka kwa Abdallah Inb Umar kuwa wakati sura hii iliposhuka Abubakar alikuwa amekaa, basi akaanza kulia. Mtume S.A.W akamuuliza "nikipi kinachokuliza ewe Abubakar? " Abubakar akajibu " ni hii sura " basi Mtume wa Allah akasema "lau kama nyinyi mngelikuwa si wenye hamkosei na hamfanyi madhambi basi Allah angeumbwa umma mwingine baada yenu ambao watu wake wanakosea na wanafanya madhambi na kisha wanataka msamaha na Allah atawasamehe"  

 

KIPENGELE CHA TAWHID:

Sura hii ukiisoma kwa mazingatio Ina mambo mengi ya kiimani tunapasa kuyaweka katika fahami zetu:

1. Ardhi itatetemeshwa na itoe kila kilichomo ndani yake marehemu na hazina zilizomo

2. Mwanadamu atapata hofu sana na kujiuliza ina nini hii ardhi

3. Siku ya kiyama Ardhi itatoa siri zote, itatoa ushahidi wa kila wema na uovu uliofanywa na mtu katika ardhi.

4. Allah ameipa idhini Ardhi ianze kutoa habari. katika surat Yasin Allah anatujulisha kuwa siku ya kiyama midomo yetu haitafanya kazi, yaani haitazungumza, ila Allah atazungumzishwa viungo na viseme yaliyo ya kweli, viungo hivyo ni kama mikono, ngozi na vinginevyo. Hivyo hivyo ardhi nayo itapewa idhini ya kuzungumza kweli tupu kila kilichofanywa na mwanadamu iwe kidogo aka kikubwa.

5. basi mwenye kufanya wema ama uovu ulio mdogo kama dhara basi atalipwa kama ni wema kwa wema na kama ni uovu kwa adhabu. Neno dhara hili leo linatafsiriwa kwa maana ya atom. Atom ni chembe ndoogo sana ambayo huwezi kuiona kwa macho ya kawaida kwa udogo wake. Hii inamaanisha kuwa hata kama wema ni mdogo kiasi gani utalipwa na hata kama uovu ni mdogo kiasi gani pia utalipwa.           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021/12/01/Wednesday - 08:54:30 am Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2051


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

HUKUMU YA NUN SAKINA NA TNWIN
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...

Sababu za kshuka surat al Asr
Sura hii ni katika sura za kitawhidi sana. Maulamaa wanasema inatosha sura hii kuwa ni mawaidha. Imamu sharifu anasema kuwa sura hii inatosha kuwa muongozo… Soma Zaidi...

WAQFU WAL-IBTIDAAI
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...

Fadhila za kusoma Quran na umuhimu wa kusoma Quran
Unazijua faida za kusoma Quran, na je ni faida gani utapata ukisoma Quran? Soma Zaidi...

Mpangilio wa quran ni wa kipekee na uliotumia ujuzi mkubwa
Soma Zaidi...

Kulaaniwa Bani Israil
Pamoja na kuteuliwa na Allah(s. Soma Zaidi...

Quran Tafsiri kwa Kiswahili
Tafsiri ya quran kw akiswahili, imeandikw ana Shekh Ali Muhsin al-Barwani Soma Zaidi...

Sababu za kushuka Surat al fatiha (Alhamdu)
Kwa kuwa hakuna sababu mwalumu ikiyonukuliwa kuwa ndio chanzo cha kushushwa suravhii. Basi post hii itakujuza mambo ambayo huwenda hukuyajuwa kuhusu fadhika za surabhii na mengineyo. Soma Zaidi...

Kitabu Cha Darsa za Quran
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

Wanaadamu kushindwa Kuandika Kitabu Mithili ya Qur-an:
Soma Zaidi...

Aina saba za Viraa vya usomaji wa Quran
Post hii inakwenda kukuorodheshea aina saba za viraka vya usomaji wa Quran. Soma Zaidi...

Sababu za kushuka sural Masad (tabat haraka)
Sura hii inazungumzia kuhusu hali ya Abulahab namke wake wakiwa kama Watu waovu. Ni moja katika sura ambazo zilishuka mwanzoni toka Mtume alipoamrishwa kulingana dini kwa uwazi. Soma Zaidi...