SABABU ZA KUSHUKA SURAT AT TAKAATHUR


image


Kuwa na tamaa huhitaji vitu vya watu si jambo jema. Ila kama tamaa hii itakuhamasisha na wewe kutafuta kitu hicho, kwa uwezo ambao Allah amekupa bila ha kuvuka mipaka yake, hili sio tatizo. Sura hii itakufundisha mengi


Surat At-takaathur

 

SURAT AT-TAKAATHUR
Wanazuoni wengi zaidi wanakubaliana ya kuwa sura hii ilishuka Makka. Imam Bukhari anaeleza ya kuwa ilishuka Madina. Lakini sahaba mmoja, Ibni Abbas, anasema ya kuwa ilishuka Makka. Neno Takaathur anasema Ibn Abbas maana yake ni tamaa nyingi ya mali na watoto (Bukhari). Abu Huraira anasimulia ya kuwa Mtume s.a.w. aliposoma sura hii alisema, "Mwanadamu anasema, hii ni mali yangu, hii ni mali yangu. Kumbe aliyokula na kuvaa ameichakaza, aliyotoa katika njia ya Mwenyezi Mungu, ndiyo kaiweka akiba na iliyobaki si yake ni mali ya watu."


 

Sababu za kushuka sura hii:-
Muqatil na Al-Kalb wamesema “sura hii ilishuka kutokana na makabila mawili ya Kikurayshi, ambayo ni Banu Abd Manafi na Banu Sahm. Kila kabila lilikuwa likijisifu na kujigamba juu ya lingine. Hivyo ikafikia hadi wakaanza kuheabu ni kabila lipi lina machifu wengi na viongozi wengi kuliko lingine. Banu Abd Manafi walikuwa wakisema “sisi tuna machifu wengi, viongozi wengi na hata kabila letu lina watu wengi”. pia banu Sahm walikuwa wakisema hivyohivyo. Basi baada ya kuhesabu ikaonekana kweli Banu Abd Manafi wana watu wengi kwenye kabila lao. Baada ha yapo wakasema “twendeni tukahesabu makaburi ya watu wetu waliokufa. Hivyo wakayaendea makaburi hapo wakaata jibu kuwa Banu Saham ni wengi waliokufa kuliko Banu Abd Manafi.


 

Qatada amesema kuwa sura hii ilishuka kuwahusu Mayahudi waliosema “sisi ni wengi ssana kuliko wakina fulani na fulani ….., hivyo walikuwa wakiendelea na madai yao haya na kujisahau, kumuasi mungu hadi mauti anawafikia.



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    2 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    3 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    4 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    5 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    6 Jifunze fiqh    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Asbab nuzul surat at Tin, Sababu za kushuka surat at Tin (watin wazaitun)
Post hii itakwenda kukufundisha sababu za kushuka kwa surat at Tin (watin wazaitun). Soma Zaidi...

image Faida za kujuwa Quran tajwid
Hapa nitakufindisha faida za kusoma quran kwa Tajwid. Soma Zaidi...

image Ni zipi hukumu za nuni yenye sakina au tanwin?
Hapa utajifunza usomaji wa Quran pindi utakapokuta nuni yenyebsakina au tanwin Soma Zaidi...

image Maana ya qalqala na aina zake katika usomaji wa Quran tajwid
Qalqala imegawanyika katika makundi mawili ambayo ni Qalqalatul qubra yaani qalqala kubwa na qalqalat as shughura yaani qalqala ndogo. Soma Zaidi...

image Aina za Madda twabiy kwenye usomaji wa Quran
Madda zimegawanyika katika maeneo makuu mawili ambayo ni madda twabiy na madda fariy Soma Zaidi...

image Sababu za kushuka surat al adiyat
Sura hii iliposhuka ilikuwa kama imekuja kuwasuta Wanafiki waliokuwa wakizungumzahabari za uongo kuhusu jeshi alilolituma Mtume wa Allah. Soma Zaidi...

image Hukumu za Tajwid katika usomaji wa bismillah (basmalah)
Hapa utajifunza kanuni za tajwid katika kusoma bismillah au basmalah. Soma Zaidi...

image Sababu za kushuka surat an-Nas na surat al Falaq
Sura mbili hizi pia hujulikana kwa jina la al muawidhatain ambazo ni surat an Nas na surat al falaq. Soma Zaidi...

image Sababu za kushuka surat at Takaathur
Kuwa na tamaa huhitaji vitu vya watu si jambo jema. Ila kama tamaa hii itakuhamasisha na wewe kutafuta kitu hicho, kwa uwezo ambao Allah amekupa bila ha kuvuka mipaka yake, hili sio tatizo. Sura hii itakufundisha mengi Soma Zaidi...

image Ni nini maana ya id-gham katika hukumu za tajwid
Hapa utajifunza kuhusu maana ya id-ghamu na aina zake. Soma Zaidi...