Sababu za kushukasurat an Nasr

Sura hii ni katika sura za mwisho kushuka, huwendakuwa ndio ya mwisho kabisa. Masahaba waliamini kuwa sura hii imetabiri kifo cha Mtume S.A.W

Sababu za kushuka surat an-Nasr (idhaa jaa)

SURATUN-NASR
Sura hii imeteremka wakati Mtume (s.a.w) hupo maka wakati wa hija ya mwisho, hija ya kuaga. Sura hii matika mashafu imewekwa katika sura za Madina kwa sababu imeshuka wakati mtume ameshafanya hijira kwenda madina.


 

Sura hii inaitwa ya Madina kwa kuwa ilishuka baada ya Mtume kuhama ingawa iliposhuka ilikuwa ni katika Makka wakati Mtume alipokwenda kufanya Haji ya mwisho. Sura hii imekuja kutabiri kifo cha Mtume (s.a.w).


 

Kutokana na mapokezi ya hadithi sura hii ndiyo sura ya mwisho kushuka katika quran ila sio aya ya mwisho kushuka. Sura hii ilishuka kwenye masiku ya tashriq katika mwezi wa dhul-hija. Baada ya kushuka sura hii Mtume (s.a.w) ndipo akahutubia waumini.

 

Sura hii tukufu inaashiria kugomboka kwa Makka. Na sababu khasa iliyo pelekea kugomboka Makka ni Maqureshi walipo vunja mkataba wa amani wa Hudaibiya kwa kuwashambulia kabila ya Khuzaa', ambao walikuwa wana masikilizano na Mtume s.a.w., na wakawasaidia Bani Bakri katika hayo. Yalipo tokea hayo Mtume akaona waliyo yafanya Maqureshi kuvunja mapatano imembidi ende kuigomboa Makka. Basi akakusanya jeshi la nguvu lenye wapiganaji elfu kumi. Akenda mwezi wa Ramadhani katika mwaka wa nane wa Hijra (Desemba mwaka 630 B.K.) Akawazuia watu wake wasipigane ila wakilazimishwa. Na Mwenyezi Mungu alipenda aingie Nabii na jeshi lake Makka bila ya vita. Na kwa hivi akapata ushindi mkubwa kabisa katika taarikhi ya wito wa Kiislamu, bila ya vita. Na Mwenyezi Mungu akamwezesha kusimamisha dola ya kwanza duniani bila ya vita na bila ya kumwagwa damu.


 

Na huo ugombozi wa Makka ulikuwa na athari za kufikia mbali kwa pande za Dini na siyasa, kwani ilikuwa ni kuung'oa upagani, kuabudu masanamu, katika ngome yake kubwa, kwa kuvunjwa masanamu yaliyo simamishwa katika Al-kaaba, na yakaondolewa mapicha na masanamu yaliyo kuwemo.

 

Na kwa kuingia Makka kwenye boma la Uislamu Nabii s.a.w. aliweza kuzishinda kabila zote zilizo bakia katika Hijazi, ambazo zilizo kuwa zina kani za kijahiliya, kama Hawazan na Thaqif. Mwenyezi Mungu akamwezesha kusimamisha dola si juu ya kabila wala nchi bali juu ya Imani, nayo ni Imani ya Kiislamu, na bendera ya Kiislamu


 

Na Ushindi mkubwa uliotajwa hapa ni ushindi wa Makka ilipoingia katika mamlaka ya Waislamu, mwaka wa 8 wa Hijra, na mwaka uliofuata ikawa makundi-makundi ya makabila ya Waarabu yanakuja ingia Uislamu. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu alivyotimiza bishara Zake za ajabu; na Mtume s.a.w. anaambiwa aombe ghofira kwa ajili ya makundi hayo yatakayoingia Uislamu maana kazi ya kusimamisha sheria ilikuwa kubwa. Seyidna Abu Bakar iliposhuka sura hii alilia. Watu wakamwuliza mbona unalia? Akajibu, Kazi ya Mtume s.a.w. sasa imekwisha na Atatutoka.

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021/11/29/Monday - 08:29:45 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1250

Post zifazofanana:-

Dalili za mimba katika mwezi wa kwanza
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za mimba katika mwezi was kwanza Soma Zaidi...

Dalili za saratani ya kibofu Cha nyongo
Saratani ya kibofu cha nyongo ni Saratani inayoanzia kwenye kibofu cha nyongo. Nyongo yako ni kiungo kidogo, chenye umbo la peari upande wa kulia wa tumbo lako, chini ya ini lako. Kibofu cha nyongo huhifadhi nyongo, Kioevu cha usaga Soma Zaidi...

Vipimo vya minyoo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vipimo vya minyoo Soma Zaidi...

mambo ambayo utaulizwa mama mjamzito ukifika kituo cha afya unatakiwa utoe majibu sahihi.
Posti hii inahusu zaidi mambo ambayo Mama mjamzito anaweza kuulizwa pindi anapokuja kwenye kliniki ya uzazi ,ni mambo muhimu na ya lazima yanayopaswa kuongea na Mama mjamzito ili kuweza kuona maendeleo yake kama ifuatavyo. Soma Zaidi...

Fahamu kuhusu kazi za ini.
Posti hii inahusu zaidi kazi za ini, kwa kawaida tunafahamu kwamba ini ni sehemu muhimu kwenye mwili wa binadamu kwa sababu ni.likikosa kufanya kazi yake maisha ya binadamu yanakuwa hatarini kwa sababu mbalimbali. Soma Zaidi...

Mtume kumuoa bi khadija
Sara na historia ya Mtume Muhammad s.a.w, sehemu ya 15. Hapa utajifunza kuhusu chimbuko la ndoa ya Mtume s.a.w na bi Khadija. Soma Zaidi...

Sababu zinazoweza kusababisha kukosa choo (kinyesi)
Kukosa choo aina ya kinyesi'ni kutoweza kudhibiti kinyesi, hivyo kusababisha kinyesi kuvuja bila kutarajiwa kutoka kwenye puru. Pia huitwa kutoweza kudhibiti utumbo,'Upungufu wa kinyesi'hutoka kwa kuvuja mara kwa mara kwa kinyesi huku ukipitisha gesi had Soma Zaidi...

Dalili za saratani ya kwenye Njia ya haja kubwa.
Saratani ya kwenye Njia ya haja kubwa ni aina isiyo ya kawaida ambayo kitaalamu hujulikana Kama saratani ya mkundu.Mfereji wa mkundu ni mirija fupi iliyo mwisho wa puru yako ambayo kinyesi hutoka mwilini mwako. Saratani ya kwenye Njia ya  ha Soma Zaidi...

Vita vya Al Fijar na sababu zake
Historia na shida ya Mtume Muhammad S.A.W, sehemu ya 12. Hapa utajifunza kuhusu kutokea kwa vita vya al fijar. Soma Zaidi...

Maji pia yanawezakuwa dawa kwa akili
Umeshawahi kuumwa na dawa yako ikawa maji? Huwenda bado basi hapa nitakujuza kidogo tu, juu ya jambo hili. Soma Zaidi...

Dalili za kupasuka kwa mfuko wa uzazi.
Posti hii inahusu zaidi dalili za kupasuka kwa mfuko wa uzazi,ni Dalili ambazo ujitokeza kwa Mama ambaye anakuwa amepasuka mfuko wa kizazi. Soma Zaidi...

Huduma ya kwanza kwa mgonjwa aliyepata ajali ya kichwa
Ajali ya kichwa na ajali inayotolewa kwenye sehemu mbalimbali za kichwa, ambavyo husababishwa madhara kwa aliyepata ajali hiyo Soma Zaidi...