Sababu za kutangulia kwa kitovu wakati Mtoto anazaliwa
Posti hii inahusu zaidi sababu za kutangulia kwa kitovu wakati wa mtoto anapozaliwa.
Sababu za kutangulia kwa kitovu wakati Mtoto anazaliwa.
1. Kwa kawaida tunajua kuwa mtoto utanguliza kichwa ila kwa wakati mwingine Kuna uwezekano mkubwa wa mtoto kutanguliza kitovu, na kwa wakati mwingine kitovu hicho kinaweza kuja kimejivilingisha kwenye shingo na mtoto akipata shida wakati wa kutoka kitovu kinaweza kumniga akafariki au kama Kuna ujuzi zaidi kwa wataalamu wa afya mtoto anaweza kuokolewa kwa hiyo zifuatazo ni sababu za kitovu kutangulia wakati mtoto anapozaliwa.
2. Jinsi mtoto alivyolala.
Kwa kawaida mtoto tunamtegemea aanze kutoa kichwa wakati wa kuzaliwa ila Kuna watoto wanatanguliza matako, kichwa, uso, mgongo na vitu kama hivyo ambavyo ni kawaida na kichwa kwa hiyo katika kujigeuza geuza Ili aweze kupata sehemu ya kutanguliza saa nyingine kitovu kinatanguli mbele kabla ya mtoto.
3. Mtoto kuwa zaidi ya mmoja.
Kwa wakati mwingine hasa kwa akina Mama ambao ujifungua mapacha kwa sababu ya kuwepo mtoto Zaid ya mmoja kila mtoto utafuta jinsi ya kutoka Ili aweze kuzaliwa kwa hiyo katika kiangaika Ili kupata nafasi usababisha kutangulia kwa kitovu badala ya kichwa.
4. Kupasuka kwa membrane kabla ya mtoto kuingiza kichwa kwenye mlango wa kizazi.
Kuna wakati mwingine chupa upasuka mapema sana kabla ya mtoto kuingiza kichwa kwenye mlango wa kizazi hali hii nayo usababisha mtoto kutanguliza kitovu.
5. Muundo wa mlango wa kizazi.
Pengine Kuna akina Mama wameumbwa tofauti kabisa na kuwa na uwezo wa kupitisha mtoto na akifika wakati wa kusukuma mtoto hawezi kupita ingawa anahisi uchungu na sifa zote za kujifungua anakuwa Nazo katika kuangaika anajikuta mtoto ashatanguliza kitovu.
6. Kwa hiyo hali hii ni ya hatari endapo wahudumu wa afya hawana utaalamu wa kugundua mapema tatizo hili, ni vizuri kuligundua Ili kuweza kuokoa maisha ya Mama na mtoto wakati Mama akiwa anajifungua.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitau cha Fiqh 👉2 Madrasa kiganjani 👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉4 Dua za Mitume na Manabii 👉5 Simulizi za Hadithi Audio 👉6 web hosting
Post zinazofanana:
Utaratibu wa chakula kwa Mama mjamzito.
Post huu inahusu zaidi utaratibu wa chakula kwa Mama mjamzito, ni chakula anachopaswa kutumia na ambavyo hapaswi kutumia kwa Mama mjamzito mzito, kwa sababu Mama mjamzito anapaswa kuwa makini katika matumizi ya chakula ili kuweza kuongeza vitu muhimu mwil
Soma Zaidi...Sababu za Mtoto Kukosa Hamu ya Kula
Mtoto kukosa hamu ya kula ni changamoto inayowapa wazazi wengi hofu na msongo wa mawazo. Hata hivyo, ni muhimu kuelewa kuwa hamu ya kula ya mtoto hubadilika kulingana na umri, hatua za ukuaji, na hata hali yake ya afya. Makala hii inaangazia sababu zinazoweza kumfanya mtoto apunguze hamu ya kula na nini unaweza kufanya ili kumsaidia.
Soma Zaidi...Dalili za kuziba kwa mirija ya uzazi
Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo zinaweza kutokea kwa sababu ya kuziba kwa mishipa ya uzazi, ni baadhi ya dalili ambazo ujitokeza kwa sababu ya kuwepo kwa tatizo la kuziba kwa mishipa ya uzazi.
Soma Zaidi...Dalili za mwanzo za ujauzito katika wiki ya kwanza
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za mwanzo za ujauzito katika wiki ya kwanza
Soma Zaidi...Fahamu dalili za hatari kwa wajawazito.
Posti hii inahusu zaidi dalili za hatari kwa mama mjamzito, kwa sababu kuna baadhi ya Dalili zikitokea kwa mama mjamzito ni vizuri kabisa kuwahi hospitali mara moja.
Soma Zaidi...Dalili za mimba kutoka.
Post hii inahusu zaidi dalili za mimba kutoka, hizi ni dalili ambazo ujitokeza kwa mimba zote ambazo utaka kutoka kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...