Sababu za kutoka kwa mimba na dalili zake
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za kutoka kwa mimba na dalili zake
KUTOKA KWA UJAUZITO, DALILI ZAKE NA SABABU ZAKE.Kutoka kwa ujauzito mara nyimgi hutokea katika hiki kipindi cha kwanza yaani ndani ya wiki 12 za mwanzo. Inakadiriwa kuwa robo ya mimba zinazotoka basi hutoka katika kipindi hiki. Mwanamke anaweza akatokwa na mimba kwa kujuwa ana bila ya kujuwa. Inaweza kutokea pia mwanamke akabeba ujauzito na ukatoka bila kuwa na habari yeyote kama alikuwa na miba na imetoka. Ni kuwa mimba inaweza kutoka bila ya kuwa na dalili za wazi kama kutoka na damu.
Dalili za kutoka kwa mimba:A.Maumivu ya mgongoB.KuharishaC.KichefuchefuD.Maumivu ya maeneo ya nyonga na kiuno kama unahisi unataka kuingia kwenye siku zakoE.Maumivu makali ya tumboF.Kutokwa na majimaji kwenye uke.G.Kutokwa na vitu kama vijioande vya nyama vijidogo kwenye ukeH.Uchovu mkali sana usio na sababuI.Kupotea kwa dalili nyingine za ujauzitoJ.Kutokwa na damu mabonge manonge ama damu nyingi
Kumbuka hizi ni dalili tu, unaweza kuwa nazo na ujauzito ukawa salama kabisa. Ukiona unahisi dalili hizo muone daktari atathibitisha vyema kwa vipimo ikiwemo utrasound ama kuangalia kiwango cha homoni ya ujjauzito kwneye damu yako.
Ni zipi sababu za kutoka kwa mimba?Mara nyingi kutoka kwa ujauzito kunaweza kusababishwa na chromosomal abnormalities. Hili ni tatizo la kigenetics. Hapa seli za mtoto zinashindwa kugawanyika vyema na kukuza mtoto. Sababu nyingine za kutoka ujauzito ni:-A.Matatizo katika homoni kuwa nyingi sana ama kidogo sanaB.Kama mama mjamzito ana kisukari na hafuati masharti vyemaC.Mazingira yanaweza kuchangia kama kuna mionzi hatari kama ya madini ya uraniumD.Maambukizi na mashambulizi ya vijidudu kama bakteria kwenye via vya uzazi.E.Shida katika mlango wa uzazi (cevix)F.Kutumia madawa kiholela ama kutumia madawa kusudi kwa lengo la kutoa ujauzitoG.Ugonjwa wa endometriosis (kuvimba kwa kuta za mji wa mimba “uterus”)H.Magonjwa ya ngono kama gonoria
Sababu nyingine za kutoka kwa mimbaA.Utapia mloB.Kuwa na kitambiC.Matumizi ya vilevi na sigaraD.Maradhi ya tezi ya thyroidE.Shinikizo la damu la juu sana
NITAZUIAJE MIMBA KUTOKA?Mimba nyingi zinazotoka husababishwa na genetics ama mambo ya kiafya ambayo si rahisi kuzuilika. Hivyo kwa mimba hizi ni ngumu sana kuzuia kutoka kwake. Hata hivypo kitu ambacho unaweza kukifanya ni kuhakikisha kuwa unabakia katika afya salama kabla na baada ya kubeba ujauzito. Fafya mabo yafuatayo yatasaidia katika kuboresha afya yako na kuzuia kiutoka kwa ujauzito:-
A.Kula mlo kamili wenye virutubisho (balanced diet)B.Fanya mazoezi mara kwa mara. Si lazima eti mazoezi ya kukutoa mijasho, unaweza kufanya mazoezi ya viungo pia hata ukiwa kitandani.C.Wacha ama punguza kutumia pombe, sigara ama dawa za kulevya.D.Punguza unywaji wa chai kama unakunywa kwa wingi kupitiliza. Hapa ninazungumzia chai ya majani ya chai ambayo ina caffein.E.Fanya uchunguzi wa afya yako mara kwa mara.F.Wacha kutumia dawa kiholelaG.Jiepushe na mambo ambayo yataweza kuwa ni hatari kwa ujauzito kama kupigana ama miereka.H.Fuata maelekezo vyema kutoka kwa wahudumu wa afya.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 kitabu cha Simulizi π2 Kitau cha Fiqh π3 web hosting π4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) π5 Kitabu cha Afya π6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina
Post zinazofanana:
Sababu za kutangulia kwa kitovu wakati Mtoto anazaliwa
Posti hii inahusu zaidi sababu za kutangulia kwa kitovu wakati wa mtoto anapozaliwa.
Soma Zaidi...Kutokwa na damu baada ya tendo la ndoa
Kutokwa na damu baada ya tendo la ndoabkunaweza kuashiria kuwa kuna majeraha yametokea huwenda ni michubuko ilitokea ndio ikavujisha damu. Lakini kwa nini hali kama hii itokee. Posti hii itakwwnda mujibu swali hili.
Soma Zaidi...Faida na hasara za kutumia kondomu kama njia ya uzazi wa mpango
Kondomu ni mpira ambao uwekwa kwenye uke au uume kwa ajili ya kuzuia mimba wakati wa kujamiiana
Soma Zaidi...Mimi nilipima na kipimo mwenyewe nkakuta mistari miwili iliokoza lkn nikifanya tendo nakua naumia sana tatizo ni Nini docta
Je anapatwa maumivu Γ°ΕΈΛΒ makali wakati wa tendo la ndoa ama ukiwa katika hedhi? Soma makala hii hadi mwisho
Soma Zaidi...