image

Sababu za kutoshika mimba kwa mwanamke

Post hii inahusu zaidi sababu za kutoshika mimba kwa mwanamke, kuna kipindi ambacho mwanamke hushindwa kushika mimba kuna sababu mbalimbali mojawapo ni kama zifuatazo

Sababu za kutoshika mimba kwa mwanamke

1. Kutokuwa na uwiano mzuri wa homoni ambapo kwa kitaalamu huitwa hormonal imbalance, kwa hiyo ili mimba iweze kutungwa ni lazima kuwepo na usawa wa homoni yaani zote zilingane.

 

2. Ovari kushindwa kutoa mayai.

Kuna wakati mwingine ovary hazitoi mayai  hii ni kwa sababu ya kuwepo kwa Maambukizi au tatizo lolote kwenye mfumo wa uzalishaji.

 

3. Kuziba kwa mirija ya uzazi ambayo kwa kitaalamu huitwa follapiani tube kwa hiyo mishipa hii ikiziba usababisha mayai kushindwa kukutana na mbegu za mwanaume wakati wa urutubishaji.

 

4. Kuna wakati mwingine mirija ya uzazi kujaa maji, hali hii utokea kwa sababu ya kuwepo kwa Maambukizi kwenye mirija ya uzazi na ikishajaa maji usababisha mayai au yai kushindwa kukutana na mbegu za mwanaume.

 

5. Kuwepo kwa uvimbe kwenye kizazi.

Kuna wakati mwingine uvimbe kwenye uzazi usababisha mama kutozaa kwa sababu mtoto hawezi kupata sehemu ya kukaa na kukua.

 

6. Magonjwa mbalimbali na yenyewe usababisha mwanamke kushindwa kupata mimba, magonjwa kama kisonono, kaswende, kisukari na pia maambukizi kwenye via vya kiza, haya Magonjwa yakiwa sugu usababisha ugumba.

 

7. Kuwepo kwa msongo wa mawazo.

Kwa kawaida ili mimba iweze kushika mwanaume na mwanamke wanapaswa kuwa katika hali nzuri bila mawazo wakifanya hivyo ni rahisi kushika kwa mimba.

 

8. Utoaji wa mimba.

Kuna wakati mwingine kutoa mimba mara kwa mara nakwo usababisha kutoshika kwa mimba kwa sababu kuna wakati mwingine via vya uzazi vinakuwa vimechokonolewa vya kutosha na baadae mimba haiwezi kushika.

 

9. Matumizi ya pombe, bangi, sigara na ulevi wa kupindukia usababisha kutoshika kwa mimba kwa sababu baadhi ya vileo usababisha kupungua kwa homoni za uzazi.

 

10. Kuwa na uzito kupita kiasi.

Kwa kawaida uzito mkubwa nao ni sababu ya kutoshika mimba kwa sababu ili mimba ishike mwili wa mama unapaswa kuwa kwenye hali ya usawa .

 

11. Kwa hiyo baada ya kufahamu haya ni vizuri kurekebisha mtindo wa maisha kwa wale ambao wana changamoto za kutopata mimba ili waweze kupata watoto na ni vema kabisa kupata ushauri wa kitaalamu kama kuna tatizo la kukosa mimba.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 5989


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Hiv n kweli majivu hutoa mimb ya siku moja hadi wiki moja
Inashangaza sana, wakati wengine wanahangaika kutafutavijauzito kwa gharama yoyote ile, kuna wengine wanataka kutoa ujauzito kwa gharama yeyote ile. Unadhani njia za kienyeji sa kutoa mimba ni salama? Soma Zaidi...

Je, wajua sababu zinazopelekea maumivu ya Matiti kwa wanawake?
Maumivu ya matiti ni malalamiko ya kawaida miongoni mwa wanawake yanaweza kujumuisha uchungu wa matiti, maumivu makali ya kuungua au kubana kwenye tishu zako za matiti. Maumivu yanaweza kuwa ya mara kwa mara au yanaweza kutokea mara kwa mara tu. Maumiv Soma Zaidi...

Hatua Saba za kutibu au kuepuka uvimbe kwenye kizazi
Posti hii inahusu zaidi hatua ambazo unaweza kuzitumia ili kuweza kutibu uvimbe au kwa kitaalamu huitwa fibroids. Hizi hatua zikitumika uweza kusaidia kupunguza kiwango cha kupata au kuwepo kwa uvimbe kwenye kizazi. Soma Zaidi...

Mambo yanayopelekea Mjamzito kutokwa na damu
Posti hii inahusu zaidi mambo mbalimbali ambayo yanapelekea Mjamzito kutokwa na damu, hizi ni baadhi ya sababu ambazo usababisha Mjamzito kutokwa na damu. Soma Zaidi...

Ni ili sababu ya kutokea kwa tezi dume
Tezidume ni moja ya magonjwa hayari yanayotokea katika mwili wa mwanaume.Hapa nimekuandalia sababu za kutokea kwa tezi dume. Soma Zaidi...

Madhara ya kutumia madawa ya kupunguza maumivu
Posti hii inahusu zaidi madhara ya kutumia madawa ya kupunguza maumivu,ni madhara ambayo utokea kwa mtu anayetumia madawa ya kupunguza maumivu. Soma Zaidi...

Dalili za kasoro ya moyo za kuzaliwa kwa watoto
Ikiwa mtoto wako ana kasoro ya moyo wa kuzaliwa, ina maana kwamba mtoto wako alizaliwa na tatizo katika muundo wa moyo wake. Baadhi ya kasoro za moyo za kuzaliwa kwa watoto ni rahisi na hazihitaji matibabu, kama vile tundu dogo kati ya chemba za moyo amb Soma Zaidi...

Sababu za mama kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua.
Posti hii inahusu zaidi sababu za mama kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua, hili ni tatizo ambalo uwapata akina Mama wengi wanapomaliza kujifungua kwa hiyo tutaweza kuziona sababu zinazosababishwa na tatizo hili. Soma Zaidi...

Ukweli kuhusu njia za uzazi wa mpango.
Posti hii inahusu zaidi ukweli kuhusu njia za uzazi wa mpango, sio kwa imani potofu ambazo Watu utumia kuelezea uzazi wa mpango. Soma Zaidi...

Nini sababu ya kuwashwa kwa njia ya mkojo kwa wanaume
Habari ya muda huu Dokata. Soma Zaidi...

Damu, majimaji na uteute unaotoka kwenye uke wa Mjamzito, sababu zake na dalili zake
Unataka kujuwa sababu za mjamzito kutokwa na damu, utelezi ama majimaji kwenye uke wake. Na dalili gani zinaashiriwa na majimaji haya Soma Zaidi...

Mimi ni mama ninaye nyonyesha toka nimejefunguwa sijawai kuziona siku zangu lakini nilipo choma sindano za yutiai nikaaza kutokwa na tamu kama siku tano na mwanangu ana mwaka moja je ninahatali ya kubeba mimba
Kunyonyesha ni moja katika njia za asili za kuzuia upatikanaji wa miba nyingine. Hata hivyo hii haimaanishi kuwa huwezi kupata mimba ukiwa unavyonyesha. Soma Zaidi...