Sababu za kuwepo fangasi ukeni
Posti hii inahusu zaidi sababu za kuwepo kwa Ugonjwa wa fangasi,ni sababu mbalimbali ambazo zinaweza kusababisha fangasi.
Sababu za kuwepo kwa fangasi ukeni.
1. Mabadiliko ya homoni yaani vichocheo.
Kuna wakati mwingine vichocheo vya mwili usababisha kuwepo kwa fangasi ukeni hasa wakati wa uchevushaji wa mayai,uja uzito, uzazi wa mpango na kukoma kwa hedhi, kutokana na hali hizo usababisha kuwepo kwa fangasi.
2. Kuwepo kwa upungufu wa kinga mwilini.
Kwa kawaida kinga ya mwili ikipungua kila ugonjwa unakuwepo kwa hiyo watu wale wenye magonjwa ya kupunguza kinga ya mwili wako kwenye hatari Kupata fangasi za ukeni ,kama vile wenye kansa, Ukimwi na magonjwa makubwa makubwa wako kwenye hatari ya kupata tatizo la fangasi ukeni.
3. Wenye ugonjwa wa kisukari.
Kwa kawaida walio na Ugonjwa wa kisukari wana sukari nyingi mwilini kwa hiyo na fangasi wanapenda sana sukari na pia wenye kisukari hasa cha mda mrefu wanakuwa katika hatari ya kupungua kwa kinga ya mwili.
4. Kuwepo kwenye mazingira ya joto.
Kwa kawaida watu wanaopenda kuvaa nguo zinazoingiza joto hasa za siri wako kwenye hatari ya kupata tatizo la fangasi ukeni, kwa hiyo ni vizuri kuvaa nguo ambazo haziruhusu joto kuingia kwenye shehemu za siri.
5. Matumizi ya kondomu na mbegu za kiume.
Kwa wale wote wanaotumia sana kondomu wakati wa kujamiiana wako katika hatari ya kupata fangasi ukeni.
6. Walio na vidonda kwenye sehemu za siri.
Kwa sababu ya kuwepo kwa wa aina ya uwazi kwenye sehemu za siri kama vile vidonda ni rahisi sana kuingiwa na fangasi kwenye sehemu za siri.
7. Kutumia sabuni wakati wa kujitawadha
Kwa kawaida kama mtu anajitawadha na sababu anaua bakteria wazuri na kusababisha kuwepo kwa fangasi ukeni
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Dua za Mitume na Manabii 👉2 Kitabu cha Afya 👉3 Bongolite - Game zone - Play free game 👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉5 Madrasa kiganjani 👉6 kitabu cha Simulizi
Post zinazofanana:
Ijue kazi ya homoni ya HCG wakati wa kupima mimba.
Posti hii inahusu zaidi kazi ya homoni ya HCG katika kupima mimba, HCG maana yake ni human chorionic gonadotropin ni homoni ambayo uonekanekana kwenye mkojo na damu kama mtu ana mimba.
Soma Zaidi...Mambo yanayopelekea Mjamzito kutokwa na damu
Posti hii inahusu zaidi mambo mbalimbali ambayo yanapelekea Mjamzito kutokwa na damu, hizi ni baadhi ya sababu ambazo usababisha Mjamzito kutokwa na damu.
Soma Zaidi...Dalili za kupata uvimbe kwenye kizazi (fibroid)
Post hii inaenda kufundisha kuhusiana na uvimbe wa kizazi kwa wanawake. Uvimbe wa kizazi no uvimbe ambao hutokea kwenye tumbo la kizazi ambao unaweza kuwa ndan ya kizazi uvimbe huu ndan ya mwanamke hujulikana kama (uterine myoma au fibroid). Uvi
Soma Zaidi...