Kama unapata maumivu wakati wa tendo la ndoa, suluhisho lako lipo kwenye makala hii

Hii ni hali inayowapata wanawake kwa kiasi kikubwa wakati wanaposhiriki tendo la ndoa. Maumivu haya pia yanaweza kumpata mwanaume ila kwa uchache sana. Hali hii kitaalamu inafahamika kama dyspareunia.
Maumivu haya yanaweza kutokea wakati wa uume unapoingia kwa mara ya kwanza, ama wakati wote wa kuingia na kutoka ama baada ya kumaliza tendo la ndoa. Maumivu ya wakati wa tendo la ndoa yanaweza kutokea kwenye uke, ama uume ama kwenye tumbo kwa kwa wanawake. Makala hii itakwenda kukuorodheshea sababu za maumivu wakati wa tendo la ndoa.
Sababu za maumivu wakati wa tendo la ndoa
1.Uke kuwa mkavu kutokana na maandalizi mabovu kabla ya kuingiza uume. Pia inaweza kuwa ni kutokana na kukosa hamu ya kushiriki tendo.
2.Kuwepo kwa majeraha kwenye uume ama uke. Majeraha haya yanaweza kuwa ni kukeketwa ana ya namna nyingine.
3.Kuwepo kwa uvimbe ama ukawa na matatizo ya ngozi katika sehemu za siri. Haya yote yanaweza kusababisha maumivu wakati wa kuingia kwa uume.
4.Maumbile ya uke. Wakati mwingine jinsi uke ulivyo inaweza kuwa ni tatizo. Kuwa uke mwingine unatabia ya kubana misui yake. Hali hii inaweza kupelekea maumivu wakai wa kupenya kwa uume.
5.Matatizo ya kimaumbile, kwa mfano kuwa na ukilema kwenye uke, ama kuwa na nyama ama ngozi ambayo inaweza kuzuia kupenya kwa uume.
6.Kuwepo kwa maradhi katka mfumo wa uzazi wa kike. Matatizo haya ya kiafya yanaweza kuwa kwenye ovari, ama kukawa na uvimbe ndani ya kizazi ama kukawa na shida katika mirija ya uretas.
7.Kufanyiwa baadhi ya matibabu katika maeneo ya siri. Kwa mfano baadhi ya matibabu ya saratani katika sehemu za siri, matibabu haya yanaweza kusababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa
8.Matatizo ya kisaikolojia na misongo ya mawaso. Wakati mwingine uoga, kuwa na msongo wa mawazo ama kukumbuka maumivu uliyoyappata siku zanyuma, hali hizi zinaweza kupelekea maumivu wakati mwingine.
9.Staili iliyotumika wakati wa kufanya sex. Wakati mwingine mikao ya kufanya tendo la ndoa inaweza kuwa ni sababu ya maumivu. Ni vyema kutumia mikao iliyo rahisi.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za mimba kuanzia siku ya 7 Hadi ya 14
Soma Zaidi...Kichefuchefu ni moja katika dalili za mimba za mapema, Lucinda je upo uwezekano kwa mwanamke kuwa na ujauzito bila hata ya kuwa na kichefuchefu?
Soma Zaidi...Kutokwa Majimaji sehemu za siri kwa mwanamke sio jambo la kushangaza na kuhisivunaumwa. Majimajivhaya ndio huboresha afya ya uzazi kwa kusafisha na kulinda via vya uzazi. Lakini majimajivhaya yakiwa mengi, ama yanawasha ama yanaharufu haa ndipo kwenye tat
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia za kuzuia ugumba, ni njia ambazo utumiwa na wapenzi ambao wameshindwa kupata watoto hasa kwa wale ambao wamezaliwa wakiwa na uwezo wa kupata watoto lakini kwa sababu tofauti tofauti wanashindwa kupata watoto kwa hiyo njia zifu
Soma Zaidi...Kama uume wako unauma ama unahisi kuwa unaunguza ama kuchoma choma, post hii imekuandalia somo hili.
Soma Zaidi...Korodani ni kiungo muhimu kwa mwanaume, katika afya ya uzazi. Unaweza kusema ni kiwanda cha kutengeneza mbegu za kiume. Kiungo hiki ni sawa na ovari kwa mwanamke.
Soma Zaidi...