Somo hili linakwenda kukuletea sababu za maumivu ya tumbo kitovu i
SABABU ZA MAUMIVU YA TUMBO KITOMVUNI
1.Kuwepo na uvimbe kwenye njia ya chakula (digestive track) kitaalamu hufahamika kama gastroenteritis. Hali hii inaweza kusababishwa na virusi, bakteria ama parasite. Mgonjwa anaweza kusikia maumivu na yanaweza kuwa ni makali sana. Mara nyingi maumivu haya yanapoa yenyyewe bila hata kuhitaji matibabau ha huondoka ndani ya siku chache. Ila ni vyema kumuona daktari kwa uchunguzi zaidi.
2. Kuvimba kwa appendix. Maumivu ya tumbo kwenye kitomfu yanaweza kuashiria ugonjwa wa appendix, kitaalamu hufahamika kama appendicitis. Kama utahisi maumivu makali ya tumo kitomvuni kisha ghafla yanahamia upande wa kulia wa tumbo kwa chini, huashiria tatizo hili.
3.Vidonda vya tumbo
Yes maumivu ya tumbo kitomvuni yanaweza kuwa yamesababishwa na vidonda vya tumbo, huwenda vipo kwenye tumbo la chakula ama sehemu ya juu ya utumbo mdogo inayotambulika kama duodenum.
3. Matatizo kwenye kongosho
Huu ni ugonjwa unaosababisha kuvimba kwa kongosho kitaalamu huitwa Pancreatitis. Maradhi haya yanaweza kuja ghafla sana bila ya kuonyesha ishara za awali.
5.Kuwa na ngriri ya henia
Ugonjwa huu huwapata wanaume, na hutokea pale ambapo baadhi ya tishu za tumboni zinapoingia kwenye misuli ya tumboni karibu na kitomvu. Kwa watu wazima upasuaji hufanyika ili kutibu tatizo.
6.Kama kuna kizuizi katika utumbo kinachozuia chakula kutembea. Tatizo hili likichelewa kutibiwalinaweza kuwa hatari zaidi. Tatizo hili huweza kusababishwa na:-
1.Mashambulizi ya bakteria
2.Henia
3.Uvimbe
4.Kama kulitokea shida wakati wa kufanyiwa upasuaji.
7.Matatizo katika mishipa mikuu ya damu kwenye tumbo (aortic aneurysm). hili ni tatizo la kiafya linalosababishwa na kudhoofu na kutanuka kwa kuta za mishipa mikuu ya damu. Hali hii inaweza kuhatarisha maisha ya mtu kama mishipa ya damu itapasuka na kupelekea damu kuingia tumboni, hii inaweza kupelekea maumivu makli. Maumivu haya yanaweza kuathiri na viungo vingine.
8.Kama kutakuwa na shida wakati wa mzunguko wa damu katika tumbo (mesenteric ischemia). hii hutokea endapodamu inayotembea kwenye utumbo mdogo itapata usumbufu, kwa mfano ikiganda. Mgonjwa anaweza kusikia maumivu makali ya tumbo. Maumivu haya huandamana na dalili kama:-
1.Kuongezeka kwa mapigo ya moyo
2.Kuona damu kwenye choo
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya viungo vinavyoathiriwa na ugonjwa wa malaria
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi aina mbalimbali za Magonjwa ya moyo,kwa kawaida tunajua wazi kuwa kuna moyo mmoja lakini moyo huo unaweza kushambuliwa na magonjwa kwa kila aina kwa mfano kuna Maambukizi kwenye mishipa ya moyo,au kubadilika kwa mapigo ya moyo na m
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea dalili za fangasi wa sehemu za Siri kwa wanawake
Soma Zaidi...Uvimbe kwenye mfuko wa uzazi hukua kutoka kwenye tishu laini za misuli ya uterasi. Fibroids nyingi ambazo zimekuwepo wakati wa ujauzito hupungua au kutoweka baada ya ujauzito, kwani uterasi inarudi kwenye ukubwa wa kawaida.
Soma Zaidi...Kuharibika kwa mimba ni upotevu wa hiari wa ujauzito kabla ya wiki ya 20. Takriban asilimia 10 hadi 20 ya mimba zinazojulikana huisha kwa kuharibika kwa mimba. Lakini idadi halisi labda ni kubwa zaidi kwa sababu mimba nyingi hutokea mapema sana katika u
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya tumbo kitovuni na dalili zake
Soma Zaidi...Seli ni chembechembe hai ambazo zimo ndani ya mwili wa binadamu na hufanya kazi mbalimbali kwenye mwili, binadamu hawezi kuishi bila seli.
Soma Zaidi...Anemia ya upungufu wa vitamini ni ukosefu wa seli nyekundu za damu zenye afya unaosababishwa na kiasi kidogo cha vitamini fulani kuliko kawaida.
Soma Zaidi...Je ukifanya mapenz na mtu mweny aina hi ya fangasi na akawa anayo maambukizi ya ukimwi.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi namna ya kuzuia maambukizi kwenye nephroni, ni njia zinazotumika kuzuia maambukizi kwenye nephroni
Soma Zaidi...