Post hii inahusu zaidi sababu za michubuko kwa watoto wanaozaliwa,ni sababu ambazo uweza kuchangia kuwepo kwa michubuko kwa watoto wanaozaliwa.
Sababu za michubuko kwa watoto wanaozaliwa.
1. Sababu ya kwanza vifaa vinavyotumika kuzalisha watoto.
Kuna wakati mwingine vifaa vinavyotumika kuzalisha watoto usababisha kuchubuka kwa mtoto inawezekana kabisa ni kwa kuchubuka kwa ndani au kuchubuka kwa ngozi ya nje, Kuna Kipindi mtoto anakuwa ameshatoa kichwa ila kutoka nje huwa ni shida na hata kama mama akisukuma kwa namna gani mtoto hawezi kutoka hali inayosababisha vifaa mbalimbali kutumika Ili kuweza kumtoa mtoto nje na kuokoa maisha ya mtoto na Mama kwa hiyo katika kimvuta mtoto atoke usababisha kuwepo kwa michubuko kwa watoto wanaozaliwa kwa hiyo ni vizuri kabisa wataalamu wa afya na wahudumu wa mtoto aliyevutwa kwa kutumia vyuma kuangalia mara kwa mara Ili kuweza kugundua kama michubuko ni ya ndani au ya nje na kuweza kutumia matibabu.
2. Pia michubuko utokea mara nyingi kwa watoto wanaozaliwa kwa kutanguliza matako, kwa kawaida mtoto anapaswa kutanguliza kichwa ikitokea mtoto akatanguliza matako, au miguu usababisha kuwepo kwa michubuko kwa watoto wanaozaliwa,kwa sababu matako na miguu uweza kuzaliwa ila Kuna Kipindi mabega na mikono ushindwa kutoka, katika kupambana ili kuweza kutoa mikono na mabega au pengine kichwa usababisha kuwepo kwa michubuko kwa watoto wanaozaliwa, na pia sio michubuko tu kwa wakati mwingine ulemavu wa mikono na mabega uweza kutokea kwa watoto, kwa hiyo kwa akina mama wanaojifungua ikitokea mtoto alikuwa ametanguliza matako au miguu na akazaliwa kwa shida kwa kupambana ni vizuri kabisa kuangalia mabadiliko yoyote na kumwambia wataalamu wa afya Ili kuweza kuepuka madhara mengine zaidi.
3. Mtoto kutanguliza mabega.
Kuna wakati mwingine mtoto anaweza kutanguliza kichwa na kichwa kikazaliwa ila mabega yakakwama kwenye mfupa wa mama ambao kwa kitaamu huiitwa pubic bone, kwa hiyo katika kupambana kuzalisha mabega Ili mtoto atoke usababisha kuwepo kwa michubuko kwa watoto wanaozaliwa, kwa hiyo ni vizuri kabisa kujua dalili za mtoto aliyetanguliza mabega Ili kuweza kutafuta mbinu za kuzalisha mama huyo au kutafuta wataalamu zaidi, na dalili ambazo ujitokeza ni kama zifuatazo.
Mama huwa na wasiwasi mkubwa kuliko kawaida na pia uhisi kitu ambacho sio cha Kawaida kwa hiyo kwa wahudumu wa afya ni vizuri kabisa kuwa karibu na mama Ili kuweza kumweka mama kwenye hali nzuri na ya kwamba kila kitu kitakuwa sawa.
4.Kichwa cha mtoto kutolingana na kiuno cha mama kwa pale mtoto anapopaswa kupitia.
Kwa kawaida kichwa cha mtoto ni lazima kabisa kulingana na kiuno cha mama kwa pale mtoto anapopaswa kupitia, hali ambayo usababisha mtoto kutumia nguvu nyingi Ili kutoka nje ,hali hii kwa kitaamu huiitwa disproportionate pelvic, kwa hiyo kabla ya mama kujifungua ni lazima kujua hali halisi ya mtoto anapotaka kujifungua kama anaweza kupita au hawezi kupita kwa kufanya hivyo tunaweza kuepuka matatizo mbalimbali kwa watoto kama vile kuchubuka na ulemavu mwingine kama huo.
5. Na tatizo jingine mama kukaa kwenye Kipindi cha kujifungua kwa mda mrefu , yaani kwa kitaamu huiitwa prolonged labor.
Ni hali ambayo mama huwa na uchungu wa mda mrefu na pia anakaa kwenye uchungu kwa mda huo inawezekana ukawa mchache ule ambao haiwezekani mtoto kuzaliwa, kwa hiyo mtoto uchoka na kwa pengine usababisha kuwepo kwa michubuko kwa watoto wanaozaliwa,
6. Vile vile Kuna hali ya uchungu kuwa mkali na kichwa cha mtoto hakishuki chini, kwa kitaamu huiitwa obstruction labour.
Hii ni Sina ya labor ambapo uchungu unakuwepo wa kutosha lakini kichwa cha mtoto hakishuki, kwa sababu uchungu upo na mtoto anapambana kutoka ila kichwa hakishuki kwa hiyo hali hiyo usababisha kuchoka kwa mtoto na pia mtoto uweza kupata michubuko,hali hii pia usababisha mama kupasuka kizazi na kusababisha kupoteza mtoto na pia kuleta matatizo kwa mama na pengine kizazi kikisha pasuka usababisha kutolewa hali hii inaweza kumfanya mama kushindwa kupata naomba ya watoto aliokusudia kupata.
7. Pengine hali inayosababisha kupata michubuko kwa watoto ni pamoja na uchungu kuwa mkubwa zaidi na WA mda mfupi, kwa kitaamu huiitwa precipitate labor.
Ni aina ya uchungu ambao utokea kwa akina mama kwa kawaida utokea kwa mda mfupi na pia mama uweza kujifungua kwa mda mfupi huo, kwa kawaida uchungu huo utumia masaa matatu tu, na pia mtoto uweza kuzaliwa, kwa hiyo mtoto ni kama vile anatoka kwa spidi kubwa na kujibamiza kwenye mifupa mbalimbali ya kiuno cha mama na kusababisha hali ya michubuko.
6. Kwa hiyo akina mama wanapaswa kuwa makini katika Kipindi cha ujauzito kwa sababu Kuna vitu vingine ambavyo usababisha madhara kwa watoto na vile vile akina mama wanapaswa kuhudhuria Kipindi cha mahudhulio yote wakati wa ujauzito Ili kuweza kugundua dalili za hatari na mambo ambayo usababisha michubuko na matatizo mengi mbalimbali .
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1253
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi
👉2 Kitau cha Fiqh
👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉4 Madrasa kiganjani
👉5 Kitabu cha Afya
Fahamu kuhusu vitamini C na kazi zake
Makala hii itakujulisha kazi kuu za vitamini C mwilini. Hapa pia utatambuwa ni kwa nini tunahitaji vitamini C na wapi tutavipata Soma Zaidi...
Mawakala wa maradhi
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu mawakala wa maradhi Soma Zaidi...
Upungufu wa vitamin
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu madhara ya upungufu wa vitamin Soma Zaidi...
Namna ya kutoa huduma ya kwanza
Huduma ya kwanza ni huduma anayopewa mgonjwa au mtu yeyote aliyepata ajali kabla ya kumpeleka hospitalini Soma Zaidi...
Fahamu kuhusu michubuko kwa watoto wakati wa kuzaliwa
Post hii inahusu zaidi michubuko ambayo mara nyingi utokea kwa watoto wakati wa kuzaliwa,na mara nyingi uweza kupona baada ya masaa ishilini na manne au ndani ya masaa ishilini na manne. Soma Zaidi...
Zijue kazi za Figo mwilini
Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa Figo mwilini, Figo ni ogani ambayo kazi yake ni kuchuja sumu mwilini. Soma Zaidi...
Aina za kuungua
Post hii inahusu Aina za kuungua, kuungua ni Hali ya kubabuka kwa ngozi ya mwili na kusababisha madhara mbalimbali Soma Zaidi...
Madhara ya chakula kutosagwa vizuri tumboni.
Posti hii inahusu zaidi madhara ya chakula kushindwa kumengenywa vizuri tumboni, haya ni madhara ambayo utokea kwa sababu ya chakula kushindwa kumengenywa vizuri tumboni. Soma Zaidi...
Haya hayawezi kuambukiza UKIMWI
Somo hili linakwenda kukuletea Mambo ambayo hayawezi kuambukiza UKIMWI Soma Zaidi...
Huduma ya kwanza kwa mgonjwa aliyepata ajali ya kichwa
Ajali ya kichwa na ajali inayotolewa kwenye sehemu mbalimbali za kichwa, ambavyo husababishwa madhara kwa aliyepata ajali hiyo Soma Zaidi...
Aina za vidonda.
Posti hii inahusu zaidi aina kuu za vidonda,kuna aina kuu tatu za vidonda ambapo kila aina utumiwa kwa njia yake kama tutakavyoona hapo chini. Soma Zaidi...
Nini husababisha kibofu cha mkojo kuuma na baadae kutoka damu
Katika post hii utajifunza sababu zinazowezabkuorlekea kibofu kuuma upande mmoja Soma Zaidi...