Sababu za mimba kutoka

Post hii inahusu zaidi sababu za mimba kutoka, hili ni tatizo ambalo linawakumba wanawake wengi ambapo mimba utoka kabla ya kumfikisha mda wake, kwa kawaida Ili kawaida mimba nyingi utoka zikiwa na miezi chini ya Saba au wengine wanaweza kusema kwamba mim

Sababu za mimba kutoka.

1. Sababu ya kwanza ni kuwepo kwa maambukizi hasa kwa akina Mama.

Maambukizi kama vile kaswende kisonono na mengine kama hayo usababisha mimba kutoka hasa pale yanaposhambuliwa sehemu ya kondo la nyuma na kusababisha kulegea na hatimaye mimba kutoka.

 

2.  Kuwepo kwa homa inayozidi kipimo au homa kuwa juu sana, kwa kawaida kiwango cha homa kwa mwanamke kinapaswa kuwa kawaida ila kikizidi kiasi usababisha kuwepo kwa kuharibu sehemu mbalimbali hasa kwa mtoto hatimaye kusababisha mimba kutoka, kwa hiyo akina Mama wanapaswa kufahamu kwamba homa yoyote isiyo ya kawaida wakati wa ujauzito ni hatari kwa makuzi ya mtoto tumboni.

 

3. Mishutuko mbalimbali.

Mishutuko mbalimbali inayoweza kuwa ya moja kwa Moja au isiyokuwa ya Moja kwa Moja usababisha mimba kutoka, kwa mfano mama kupigwa sehemu za tumbo usababisha mishutuko kwenye sehemu zilizoshikilia mtoto na kusababisha mimba kutoka au kwa wakati mwingine mishutuko inayosababishwa na msongo wa mawazo pamoja na mambo ya kusikitisha yanaweza kusababisha mimba kutoka. Kwa hiyo jamii inapaswa kumtunza Mama na kuhakikisha anapata mazingira mazuri Ili kuweza kuruhusu mimba kukua vizuri.

 

4. Magonjwa mbalimbali nayo usababisha mimba kutoka.

Kuna baadhi ya magonjwa ambayo usababisha mimba kutoka hasa kama ni ya mda mrefu kwa mama mjamzito hayo ni kama kisukari cha kupanda na kushuka, shinikizo la damu na ukosefu wa baadhi ya homoni au vichocheo vinavyosababisha makuzi ya mtoto mfano kichocheo cha progesterone kikipungua ni hatari kwa makuzi ya mtoto tumboni, sio kwamba walio na magonjwa haya wote mimba utoka hapana ila wakiamua kuchukua matibabu na kufuata mashariti Wana uwezo wa kujifungua salama. Kwa hiyo kama mjamzito yeyote anajua ana tatizo hilo ni vizuri kabisa kupata ushauri kwa wataalamu wa afya na kupata matibabu Ili kuokoa maisha ya Mama na mtoto.

 

5. Baadhi ya madawa na mazingira magumu usababisha mimba kutoka.

Kuna watu ambao katika maisha yao wamezoea kutumia madawa ambayo ni hatari wakiendelea kutumia hasa wakiwa na wajawazito madawa hayo ni kama madawa ya kulevya,watumiaji wa quinine wakiwa na malaria, matumizi ya vinywaji vikali kama vile konyagi matumizi ya sigara, haya yote usababisha kutoka kwa mimba kabla ya wakati, kwa hiyo ni vizuri kabisa kama mama akubeba mimba anapaswa kuachana nayo kabisa Ili aweze kupata mtoto mwenye afya.

 

6. Kukosa mlo  kamili wa kutosha na wenye virutubisho mbalimbali.

Kwa kawaida mama akibeba mimba damu upungua kwa hiyo anapaswa kula vyakula vya kuongeza damu Ili kuweza kupata mtoto mwenye afya na afya ya mama mwenyewe, ila Kuna akina Mama ambao wakibeba mimba hawali kabisa au wanakula chakula kidogo hali inayosababishwa kutoka kwa mimba au wakati mwingine wanakula aina Moja ya chakula na kusababisha kukosa kwa madini kwa mtoto hatimaye mimba kutoka, kwa hiyo akina Mama wanashauliwa kula mboga za majani, matunda na vyakula vya madini ya chuma.

 

7. Kuwepo kwa maambukizi kwenye mfuko wa kizazi.

Kuna wakati mwingine kwenye mfuko wa kizazi kunakuwepo na maambukizi, hali ambayo usababisha mimba kutoka kwa sababu ya kuwepo kwa maambukizi. Kwa hiyo akina Mama wanapaswa kutumia dawa mbalimbali Ili kuweza kuepuka mimba kutoka kwa sababu ya kuwepo kwa maambukizi.

 

8. Kutoa mimba mara kwa mara.

Hii ni tabia inayohusu zaidi akina dada wakiwa bado hawajahitaji watoto ila wanakuwa na wapenzi wao hali inayosababisha kubeba mimba na kutoka kwa hiyo kwenye mfumo wa uzazi ujitengenezea mazingira ya kutoa mimba kabla ya kukomaa hali inayosababisha mimba kutoka kwa sababu ya mazoea ya mara kwa mara. Kwa hiyo akina dada wanapaswa kuacha tabia ya kutoa mimba ila watumie uzazi wa mpango au wasubiri wakati.

 

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/11/01/Tuesday - 04:10:22 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1180

Post zifazofanana:-

Kujaa kwa memory au hard disc
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vitu vya kufanya endapo memory au hard disk itajaa Soma Zaidi...

Nna swali mimi nimefanya Romance na mtu ambaye sijampima kbsa sasa naogopa anaeza kuwa mgonjwa na mm nkaupata
Muulizaji anauliza he kula denda, ama kumbusu ama kufanya romance na muathirika was HIV na wewe uta ambukizwa? Soma Zaidi...

Vyanzo vya magonjwa yanayotokea kwenye sehemu za siri
Posti hii inahusu zaidi vyanzo vya magonjwa yanayotokea kwenye sehemu za siri,kwa sababu siku kwa siku kuna magonjwa mengi yanayotokea kwenye sehemu za siri ila kuna vyanzo mbalimbali ambavyo usababisha kuwepo kwa magonjwa kwenye sehemu mbalimbali za siri Soma Zaidi...

Fahamu kuhusu vitamini K na kazi zake mwilini
vitamini k ni moja katika vitamini vinavyoitajika sana mwilini. Je unazijuwa athari za upungufu wa vitamini k mwilini? Soma Zaidi...

Fahamu sifa za Ute wa siku za kupata mimba yaani ovulation day
Posti hii inahusu zaidi sifa za Ute wa ovulation, ni Ute ambao utokea siku za ovulation yaani siku ambazo ni tayari kwa kubeba mimba, yaani siku za upevishaji wa yai. Soma Zaidi...

Madhara ya gonorrhea endapo haitotibiwa
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu madhara ya gonorrhea endapo haitotibiwa Soma Zaidi...

Maanavya legacy contact katika Facebook
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maana ya legacy contact katika facebook Soma Zaidi...

PHP level 1 somo la kumi (10)
Somo la 10 mafunzo ya php level 1. Katika somo hili utajifunza kuhusu condition statement. Soma Zaidi...

Faida za vyakula vya asili
Posti hii inahusu zaidi faida za matumizi ya vyakula vya asili, kama tunavyojua kwamba mababu na mabibi zetu walitumia vyakula vya asili wakaishi miaka mingi kweli. Soma Zaidi...

Dalili za ongezeko la homoni ya estrogen
Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo mtu anaweza kupata ikiwa homoni ya estrogen imeongezeka, hizi dalili zikitokea mama anapaswa kuwahi hospital ili kuweza kupata matibabu au ushauri zaidi. Soma Zaidi...

Matibabu ya maumivu chini ya kitovu
Post hii inahusu zaidi matibabu ya kutibu ugonjwa wa maumivu chini ya kitovu. Soma Zaidi...

Dawa ya fluconazole kama dawa ya fangasi
Post hii inahusu zaidi dawa za fangasi na matumizi yake kwa kutumia dawa ya fluconazole kama dawa mojawapo ya fangasi. Soma Zaidi...