Sababu za Ugonjwa wa kifafa cha mimba.
Posti hii inahusu zaidi sababu za kifafa cha mimba, kwa kawaida mpaka sasa hakuna taarifa zozote kuhusu sababu za kuwepo kwa kifafa cha mimba ila kuna visababishi vinavyofikiliwa kama ni Dalili za kifafa cha mimba kama ifuatavyo
Sababu za kuwepo kwa kifafa cha mimba.
1. Kuwepo kwa shinikizo la damu lisilo la kawaida ambapo sio kwa sababu ya mimba ila ni kawaida ya mtu mwenye Ugonjwa huo, kwa hiyo wale wenye Tatizo la shinikizo la damu wanaweza kupata Ugonjwa huu ingawa si wote wenye shinikizo la damu kupatwa na Tatizo hili.
2.pia tatizo hili linawatokea Sana wale wanaobeba mimba za kwanza kuliko wale ambao wamebeba mimba mara nyingi, kwa hiyo wale wa mimba za kwanza wako hatarini kupata Ugonjwa huu.
3.Kwa wale wajawazito wanaopata shinikizo la damu na kiwango cha protini kuwepo kwenye mkojo wakati wa mimba ila wakijifungua tatizo hili linaisha kwa hiyo wako kwenye hatari ya kupata kifafa cha mimba mara wabebapo mimba.
4. Pengine kifafa cha mimba kinakuwepo kwenye familia fulani yaani kuna familia ambazo kila mtu akibeba mimba ni lazima apate kifafa cha mimba, kwa hiyo tunapaswa kufahamu familia zetu na kuchukua hatua mapema ipasavyo hasa kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya na kupata uangalizi wakati wa ujauzito.
5. Pia ugonjwa huu utegemea na sehemu husika kwa mfano waafrika wanapatwa sana na matatizo haya ukilinganisha na wazungu pamoja na wa hindi mpaka sasa sababu haijawahi kujulikana.
6. Huduma za afya kuwa duni sana, tunasema hivyo kwa sababu kuna wakati mwingine huduma mbaya kwa wanawake huwa chini kwa sababu unakuta wajawazito ni wengi na wahudumu ni wachache hali ambayo Usababisha wajawazito kutopata vipimo vya kutosha, kwa hiyo kama Mama ana tatizo hili ni vigumu kuligundua mapema hali ambayo Usababisha kukuta hali ishakuwa mbaya zaidi ukilinganisha na pale ingegundulika mapema.
7. Watu wenye vitambi.
Kuna utafiti uliobainika kuwa watu wenye vitambi wanapata sana Ugonjwa huu kuliko wale ambao hawana vitambi.kwa hiyo akina Mama wanaotegemea kupata watoto jitahidi kupunguza vitambi ili kuepuka tatizo hili.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Madrasa kiganjani 👉2 web hosting 👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉4 kitabu cha Simulizi 👉5 Simulizi za Hadithi Audio 👉6 Dua za Mitume na Manabii
Post zinazofanana:
siku za hatari
Hizi ni siku za hatari kupata ujauzito.Siku hizi ndio siku za kupata mimba kwa urahisi
Soma Zaidi...Maumivu ya Uke na Uume baada ya tendo la ndoa na wakati wa tendo la ndoa
Utajifunza sababu za maumivu ya uume na uke wakati wa tendo la ndoa na baada ya tendo la ndoa na matibabu yake.
Soma Zaidi...dalili za mimba changa na siku ya kupata mimba
Jifunze namna ya kuthibitisha dalili za ujauzito kuwa ni za kweli. Tambuwa namna ya kupima mimba na muda mujarabu wa kupima
Soma Zaidi...Njia za uzazi wa mpango kwa watu wenye Ukimwi
Posti hii inahusu zaidi njia za uzazi wa mpango kwa watu waliopata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
Soma Zaidi...Kazi ya homoni ya testosterone
Posti hii inahusu zaidi kazi ya homoni ya testosterone, hii homoni kwa kiwango kikubwa ukutwa kwa wanaume ndiyo homoni ambayo umfanya mwanaume aonekane jinsi alivyokuwa na sifa zake zote.
Soma Zaidi...Madhara ya sindano za kuzuia mimba kwa vijana.
Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea kwa sababu ya matumizi ya sindano za kuzuia mimba kwa vijana ambao hawajafikilia mpango wa kuanza kujifungua watoto.
Soma Zaidi...