Post hii inahusu zaidi Sababu za uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo, hali hii uwatokea sana wanawake zaidi ya wanaume, kwa kitaalamu hali hii ya kuwa na uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo huitwa cystitis.
Sababu za uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo.
1. Uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo usababishwa na bakteria ambao uingia na kushambulia sehemu za ndani za kibofu Cha mkojo, bakteria hao wanaweza kutoka sehemu mbalimbali kama vile kwenye mkojo wenyewe ikiwa mkojo umekaa kwa mda mrefu bila kutolewa nje hao bakteria wanaweza kushambulia sehemu za ndani ya kibofu Cha mkojo na hatimaye kuleta maambukizi kwenye kibofu Cha yanayoambatana na uvimbe.kwa hiyo ni lazima kukojoa tu baada ya kuhisi mkojo Ili kuepuka madhara ya kuwa na uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo.
2. Kutumia sana ngono zembe yaani kujamiiana bila kutumia kondomu.
Hii ni mojawapo ya sababu ya kuwa na uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo kwa sababu ya kuwepo kwa magonjwa ya ngono ambapo bakteria kutoka kwa mtu Mwenye maambukizi kwenda kwa mwingine ambaye Hana maambukizi na kusababisha kuwepo kwa bakteria ambao uingia kwenye kibofu Cha mkojo na kushambulia na kusababisha uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo, hasa hasa kama bakteria hawa wasipotibiwa mapema uweza kuleta madhara makubwa zaidi na kusababisha ugumba. Kwa hiyo tunapaswa kutumia kondomu wakati wa kujamiiana.
3. Kuaribika kwa sehemu za kuchuja mkojo.
Wakati mwingine Kuna kuharibika kwa sehemu mbalimbali zinazohusika na kuchuja mkojo, kama vile figo, nephroni na sehemu zote kwa hiyo hali hii usababisha bakteria kusababisha maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo kwa sababu mkojo hauwezi kutoka kwa wakati au pengine kushindwa kutoka kwenye kibofu Cha mkojo, hali ambayo usababisha bakteria kuendelea kusababisha maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo. Kwa hiyo tunapaswa kuangalia mfumo wote wa kibofu Cha mkojo.
4. Kutumia catheter kwa mda mrefu au mara kwa mara.
Hii ni sababu mojawapo ambayo ufanya kuleta uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo, kwa sababu catheter inaweza kuharibu kwenye milija wa mkojo na kusababisha bakteria kuingia na kuleta madhara makubwa ambayo yanasababisha kuleta uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo kwa hiyo inabidi catheter kuwepo kwa mda unaohitajika, mda isizidi Ili kuzuia maambukizi.kwa hiyo wataalamu wa afya wanapaswa kuhakikisha kuwa catheter unatolewa kwa mda.
5. Wanawake wanaotumia uzazi wa mpango.
Wanawake wengi wanaoweka mipira kwaenye uke illi kuzuia mimba isitungwe usababisha bakteria kupita na kuingia kwenye sehemu ya kibofu Cha mkojo na kuleta madhara makubwa zaidi ambayo yanaweza kusababisha uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo kwa sababu mipira hiyo uacha uwazi ambao usababisha bakteria kuweza kupita na kuzaliana huko na kuleta uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Tonsillitis kwa kiswahili hujulikana kama mafundomafundo ambayo hutokea pande mbili karibu na Koo na huwa na uvimbe na zikikaa kwa muda bila matibabu hutoa usaha.Dalili na dalili za ugonjwa wa tonsillitis ni pamoja na
Soma Zaidi...Saratani ya ini ni Saratani inayoanzia kwenye seli za ini lako.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali za kuweza kupambana na fangasi za ukeni ili kuweza kujiepusha na madhara mbalimbali kwenye maisha ambayo ni pamoja na ugumba na Maambukizi kwenye via vya uzazi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa macho, ni ugonjwa ambao ushambulia zaidi sehemu za nje za macho ambazo kwa kawaida uitwa conjunctiva na cornea hizi sehemu zikipata maambukizi zisipotibiwa mapema uweza kusababisha upofu kwa mgonjwa.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za uti wa mgongo, ni ugonjwa unaotokana na kuwa na maumivu kwenye uti wa mgongo, hasa hasa ugonjwa huu ushambulia watu kuanzia miaka ishilini mpaka kwenye arobaini hivi, zifuatazo ni sababu za maumivu katika uti wa mgongo.
Soma Zaidi...AINA ZA MINYOO Minyoo ambao wanaweza kuishi ndani ya mwili wa binadamu wapo aina nying, lakini hapa nitakueleza aina kuu tatu za minyoo hawa.
Soma Zaidi...KUJIANDAA KWA AJILI YA KUMUONA DAKTARI Fanya miadi na daktari wako wa kawaida ikiwa una ishara au dalili zinazokupa wasiwasi.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza namna mbalimbali za kujikinga na VVU/UKIMWI
Soma Zaidi...Kama tulivyokwisha kuona kuwa malaria inaweza kuambukizwa kwa kung'atwa na mbu aina ya anophelesi.
Soma Zaidi...