Sababu za wajawazito kupata Bawasili.
Posti hii inahusu zaidi sababu mbalimbali ambazo zinafanya wajawazito kupata ugonjwa wa Bawasili, kwa sababu tatizo hili linawapa wakina mama wajawazito, kwa hiyo tutaona kwa nini wajawazito wanapatwa na tatizo hili sana.
Sababu za kuwepo kwa ugonjwa wa Bawasili kwa wajawazito,
1. Kwanza kabisa tunapaswa kufahamu kwamba akina mama wajawazito upatwa na tatizo hili hii nikwa sababu ya kukua kwa mtoto kutoka hatua Moja kwenda nyingine na hivyo na uzito wa mtoto kuongezeka.
2. Kuwepo kwa mkandamizo au uzito kuzidi.
Kwamba tulivyotangulia kusema kwamba mwanamke Mjamzito uongezeka uzito na mgandamizo sehemu ya haja kubwa kwa sababu ya kuwepo kwa uzito wa mtoto na ukuaji wa mwili wa kizazi ( uterus) Hali hii upelekea mgandamizo sehemu ya haja kubwa na kusababisha mishipa ya damu midogo midogo kwenye sehemu mbalimbali za haja kubwa kupasuka hali inayosababisha kuota kwa vinyama au uvimbe kwenye sehemu mbalimbali za haja kubwa inayoambatana na miwasho.
3. Tatizo lingine ni ulaji wa udongo.
Tunafahamu kabisa wakati wa ujauzito akina Mama ula vitu vingi mbalimbali pamoja na udongo kwa sababu ya kukosa madini ya chuma kwa hiyo ulaji wa udongo usababisha wajawazito kupata choo kigumu hali ambayo usababisha wajawazito kutumia nguvu kubwa wakati wa kujisaidia hali inayosababisha Mishipa midogo midogo kwenye sehemu za haja kubwa kupasuka na hatimaye kuota uvimbe na vinyama kwenye sehemu mbalimbali za haja kubwa.
4. Unywaji mdogo wa maji wakati wa ujauzito.
Kwa kawaida wakati wa ujauzito akina Mama wanapaswa kunywa maji ya kutosha kwa sababu ya faida mbalimbali kwenye mwili.ila Kuna baadhi ya akina Mama wakati wa ujauzito wanabagua sana vyakula hata na maji wengine hawataki kabisa kutumia hali inayosababisha choo kuwa kigumu na katika harakati za kutoa choo unaweza kukuta mishipa ya haja kubwa kupasuka na kusababisha kuota uvimbe na vinyama kwenye sehemu mbalimbali za haja kubwa.
5. Kwa hiyo akina Mama wanapaswa kunywa maji ya kutosha pamoja na kutoa taarifa yoyote endapo wataona mabadiliko yoyote mwilini Ili kuepuka na balaa hili la bawasili na pia choo kikiwa kigumu no vizuri kabisa kutumia mboga mboga za majani na dawa Ili kurainisha choo hicho
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 kitabu cha Simulizi 👉2 Madrasa kiganjani 👉3 Kitabu cha Afya 👉4 Kitau cha Fiqh 👉5 web hosting 👉6 Bongolite - Game zone - Play free game
Post zinazofanana:
Maumivu ya tumbo wakati wa tendo la ndoa
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya tumbo wakati wa tendo la ndoa
Soma Zaidi...CHANGAMOTO ZA UJAUZITO, NA DALILI ZAKE NA NAMNA YA KUKABILIANA NAZO
Utawezaje kukabiliana na changamoto za ujauzito, je ni zipi changamoto hizo. Hapa nitakujuza.
Soma Zaidi...Namna ya kufunga kitovu cha mtoto.
Posti hii inahusu zaidi njia au namna ya kufunga kitovu cha mtoto mara tu anapozaliwa, kwa kawaida tunafahamu kwamba ili mtoto aweze kuishi akiwa tumboni anategemea sana kula na kufanya shughuli zake kwa kupitia kwenye plasenta kwa hiyo mtoto akizaliwa tu
Soma Zaidi...Siku za hatari, siku za kubeba mimba
Hizi ni siku hatari kwa mwanamke ambazo ni ahisi kwake kubeba mimba, siku nitakueleza ni zipi na ni zipi sifa zake
Soma Zaidi...Siku za kupata mimba
Nitakujulisha siku ya kupata mimba na sifa zake, na namna ya kuweza kuitafuta
Soma Zaidi...Njia za kutibu mbegu dhaifu.
Posti hii inahusu zaidi njia za kutibu mbegu dhaifu, ni njia ambazo utumika kutibu mbegu ambazo ni dhaifu ili kuweza kuondoa tatizo hili ambalo limewakumba wanaume wengi na kusababisha madhara makubwa kwenye ndoa au familia.
Soma Zaidi...