Kutokwa na mate mengi mdomoni si ugojwa ni hali inayoweza kutokea kwa mtu yeyote. Mara nyingi hali hii haihitaji matibabu wa dawa, na huondoka yenyewe. Lakini hutokea baadhi ya nyakati ikawa mate yanatoka zaidi mdomoni. Je na wewe ni miongoni mwao? Makala
Hapa tutaangalia baadhi ya sababu zinazopelekea mdomo kujaa mate. Sababu hizi zipo nyingine ni kwa wanawake tu, pia zipo ambazo ni kwa watu wa jinsia zote. Tunatarajia baada ya kusoma makala hii utaweza kuzijuwa sababu zinazopelekea mdomo kujaa mate, pia utaweza kupata kujuwa nini unatakiwa ufanye kulingana na tatizo lako.
HUJAA KWA MATE MDOMONI NI NINI HASA?
Kitaalamu kitendo hiki cha kujaa kwa mate mdomoni hufahamika kama hypersalivation. Hiki ni kitendo cha mdomo kujaa mate na wakati mwengine hutokea mate yakatoka yenyewe kwenye midomo baada ya kujaa. Kitaalamu kitendo hiki sio ugonjwa ila ni dalili ya kuwepo kwa tatizo lakiafya ama kuwepo kwa jambo lililopelekea mabadiliko ya mwili na kiafya.
JE MATE NI NINI?
Mate ni kimiminika cheupe kinachopatikana mdomoni ambacho hutengenezwa kwenye tezi za mate zinazojulikana kama salivary glands. Mate yana vichochezi (enzymes) ambavyo hutumika katika mmeng'enyo wa chakula hasa chakula cha wanga mdomoni. Mate pia husaidia katika kulainisha chakula na kuweka mgomo katika hali ya usafi, usalama na ubichibichi.
Tafiti zinaeleza kuwa mtu wa kawaida anaweza kuzalisha mate yanayofikia lita moja na nusu kwa siku. mate huzalishwa kwa wingi mtu anapokula na uzalishaji huu hupunguwa pale anapolala.
MADHARA YA KUWA NA MATE KIDOGO
Kwa kuwa mate yana faida kubwa mwilini hivyo endapo uzalishaji wa mate hautakuwa wa kutosheleza madhara huweza kumpata mtu ni kama:-
1.mdomo kuwa mkavu
2.Mmeng’enyo wa chakula kutofanyika vyema mdomoni kwa vyakula vya wanga
3.Mtu anaweza kupata taabu wakati wa kumeza
4.Anaweza kupata vidonda vya mdomo
5.Mdomo utaweza kuathiriwa kwa urahisi na fangasi, bakteria na sumu na kemikali za kwenye vyakula
6.Hata kuzungumza kunaweza kuathiriwa endapo mtu atakosa mate ya kutosha
MADHARA GANI ATAYAPATA MTU KAMA ATAKUWA NA MATE MENGI ZAIDI?
Kama ilivyokuwa kuna hasara kwa mate kukosekana mwilini, halikadhalika endapo mate yatakuwa mengi zaidi pia hali hii itakuwa na madhara yake. Madhara hayo ni kama:-
1.Matatizo wakati wa kusema, yaani hatoweza kuema vyema kama mate yatakuwa yamejaa mdomoni
2.Itakuwa vigumu kuufunga mdomo
3.Pia mdomo utaweza kupata mashambulizi ya bakteria kwa urahisi.
4.Mtu atashindwa kujiamini na kukaa na watu kwa sababu ya mate yake.
NINI HUSABABISHA MDOMO KUJAA MATE?
Hizi ni katika sababu ambazo hupelekea mate kujaa mdomoni:-
1.Kuongezeka kwa uzalishwaji wa mate mdomoni
2.Kama mtu atakuwa na shida na kushindwa kumeza mate ama mdomo kuondoa mate yote wakati wa kutema
3.Kama mtu atakuwa na matatizo ya kutoweza kuufunga mdomo
NINI HUSABABISHA ONGEZEKO LA UZALISHAJI WA MATE MDOMONI
Kama ulivyoona hapo juu sababu za kuwa na mate mengi mdomoni ni ongezeko la uzalishwaji wa mate mdomoni. Sasa swali la msingi kuwa “ni nini husababisha hili ongezeko la uzalishwaji wa mate mdomoni” . Sababu gizo ni kama:-
1.Kichefuchefu
2.Homa ya asubuhi na ujauzito
3.Kama kuna maabukizi na mashambulizi ya bakteria na virusi kwenye koo, tonsil na meneo mengine ya mdomoni
4.Kama umeng’atwa na buibui mwenye sumu, ama umekula uyoga ama umeng’atwa na wadudu
5.Kama unatumia meno ya bandia
6.Kama hufanyi usafi wa kinywa kwa umakini
7.Kama una maambukizi ya T.B ama ugonjwa wa rabies
8.Kama una kiungulia cha mara kwa mara
9.Mipasuko kwenye taya ma amifupa ya taya kutojipanga vyema
10.Vidonda vywnyw mfumo wa mmeng’enye wa chakula kama mdomoni, kooni na tumboni
NINI HUSABABISHA KUSHINDWA KUMEZA MATE AMA KUTEMA MATE YOTE?
Kama tulivyoona kuwa katika sababu zinazopelekea mate kujaa mdomoni ni kushindwa kuyameza yote, ama kuyatema yote. Sasa ni kitu gani husababisha hali hii?
1.Kuwa na shida ya kiafya kwenye mfumo wa fahamu
2.Kuwa na shida ya kiafyakwenye figo
SABABU NYINGINE ZINAZOPELEKEA MDOMO KUJAA MATE
1.Mpangilio mbaya wa meno
2.Majeraha kwenye mdomo
3.Hewa mbaya
4.Upungufu wa maji mwilini
5.Matatizo kwenye mfumo wa fahamu hasa katika kuhisi ladha ya chakula
6.Kama una maradhi ya pneumonia
NINI UFANYE KAMA UNA HILI TATIZO:
1.Kwa kupitia dalili zilizotajwa hapo juu, angalia ambayo huwenda ndio sababu kwako.
2.Kawaida tatizo hili halihitaji dawa, ila kama imezidi fika hospitali kwa uchunguzi zaidi.
3.Fika kituo cha afya kwa vipimo zaidi kama hali yako itaendelea kwa muda bila kurudi nyuma.
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi aina mbalimbali za Magonjwa ya moyo,kwa kawaida tunajua wazi kuwa kuna moyo mmoja lakini moyo huo unaweza kushambuliwa na magonjwa kwa kila aina kwa mfano kuna Maambukizi kwenye mishipa ya moyo,au kubadilika kwa mapigo ya moyo na m
Soma Zaidi...Post hii inahusu Zaidi watu walio kwenye hatari ya kupata usaha kwenye mapafu, pamoja na kuwepo Kwa sababu zinazopekekea kupata tatizo la kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu ila Kuna watu wenye hali Fulani wako kwenye hatari ya kupata usaha kwenye mapafu kama
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia za kuzuia kuaribika kwa figo, hizi ni njia zinazotumika ili kuweza kupunguza tatizo la kuaribika kwa figo na hasa wale ambao hawajapata tatizo hili wazitumie ili tuone kama tutaweza kupunguza tatizo hili.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi mambo yanayochangia katika makuzi ya mtoto, mtoto katika makuzi yake anahitaji kutunzwa vizuri Ili akue kwa afya nzuri bila magonjwa
Soma Zaidi...Ascariasis ni aina ya maambukizi ya minyoo mviringo. Minyoo hii ni vimelea wanaotumia mwili wako kama mwenyeji kukomaa kutoka kwa mabuu au mayai hadi minyoo wakubwa. Minyoo ya watu wazima, ambayo huzaa, inaweza kuwa zaidi ya futi (sentimita 30) kwa
Soma Zaidi...Fangasi hawa ni maarufu sana kwa mapunye ya kichwani ama kwenye ngozi mikononi ama miguuni.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo mtu anaweza kupata ikiwa Kuna maambukizi kwenye magoti, kwa sababu mbalimbali ambazo usababisha maumivu au maambukizi kwenye magoti Kuna dalili za mwanzo ambazo zinajitokeza kama tutakavyoona hapo chini
Soma Zaidi...Ni muda gani nitaanza kuona dalili za HIV na kilimo kitaonyesha kuwa nimeathirika?
Soma Zaidi...Afya ya tumbo ni ishara tosha ya umadhibuti wa afya ya mtu. Maradhi mengi wanayouguwa watu chanzo kile mti anachokula. Yapo maradhi sugu kama saratani ambayo husababishwa pia na vyakula. Post hii itakwenda kujibu swalo la muulizaji kuhusu maumivu ya tumbo
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi jinsi magonjwa yanavyosambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
Soma Zaidi...