image

SAFARI YA MUUJIZA

Post hii inahusu hadithi moja iliyotokea Kwa mama mmoja mwenye familia ya watoto watano.ambapo mama aliolewa na mwanaume mwenye maambukizi ya virus vya ukimwi na kupata watoto bila maambukizi kusambaa kutoka Kwa baba kwenda Kwa mama.

SAFARI YA MUUJIZA.

post hii inahusu Zaidi safari ya muujiza ya mama mmoja ambaye Kwa jina aliitwa bahati,kutokana na jina lake kweli maisha yake yalikuwa ya bahati, kadri ya historia yake yeye ni mtoto wa kumi , katika familia yao ya watoto kumi wa kike ni yeye mmmoja na WA kiume ni tisa, Kwa nini aliitwa bahati,Kwa sababu mama yake alijifungua watoto hao tisa sio Kwa kupenda bali Kwa sababu ya kutafuta mtoto wa kike, ukiangalia distance iliyopo kati ya mtoto wao wa tisa na kumi ni kubwa ambapo mtoto wa tisa anamzidi bahati miaka kumi na miwili.

 

 

 

 

Wakati mama bahati alipokosa mtoto wa kike baada ya kupata mtoto wa tisa ,aliamua kuachana na kujifungua Kwa hiyo akachukua mtoto wa kike kutoka kwenye kituo Cha watoto yatima na kuanzia kumlea kama mtoto wake na mtoto huyo alipendwa sana na mama bahati Kwa sababu alikuwa wa kike na mtoto Kwa jina aliitwa ya Mungu mengi, Kwa hiyo alipokelewa kwenye familia hiyo akiwa na miezi miwili Kwa hiyo haikuwa rahisi huyo mtoto kufahamu kwamba Hawa SI wazazi wake wa kweli alipokuwa mkubwa hata hakwambiwa na ukitegemea alikuwa mwenye rangi kama ya familia yaani weupe.

 

 

 

Kadri siku zilivyokwenda mtoto ya Mungu mengi alianza kuwa na tabia tofauti na ndugu zake ,Kwa sababu ndugu Hawa wa damu moja walikuwa wapole,wasikivu,wachapakazi ila ya Mungu mengi alikuwa mtundu sana, mchokozi,mtoro shuleni na mambo mengine kama hayo,basi siku moja shuleni watoto wa mama na baba mmoja walipewa zawadi shuleni Kwa sababu ya kufaulu vizuri ila ya Mungu mengi peke yake ndiye hakupewa ila alicharazwa viboko shuleni Kwa sababu ya kufanya vibaya, na mwalimu aliwaita wazazi shuleni ili wapewe zawadi ya wazazi Bora Kwa ajili ya watoto wao na pia kuonywa Kwa sababu ya mtoto aliyefanya vibaya Zaidi pale shuleni ambaye alikuwa ya Mungu mengi.

 

 

 

Kwa sababu baba na Mama wa watoto wa damu moja walipenda sifa hasa baba yao,Kwa hiyo alipofika shuleni alipokelewa na waalimu na wazazi pia waliokuwepo pale, Kwa hiyo wakanza kutoa zawadi Kwa watoto wao na pia Kwa kutoa ushauri Kwa mtoto mmoja ambaye hakufanya vizuri, baba aliumia sana Kwa sababu ya mtoto ya Mungu ni mengi na mama akapokea kawaida,basi wale wazazi wakapewa kipaza sauti ili waongee chochote,baba akampa mama kipaza sauti ili aongee kwanza, basi mama akaanza kuongea na kusema kama ifuatavyo.

tunawashukuru sana waalimu Kwa kazi njema na tunafahamu kwamba kazi ya kufundisha watoto ilivyongumu , vile vile tunawashukuru Kwa ufaulu mzuri wa watoto Hawa na pia Kwa zawadi ila sisi wazazi tunatoa mchango mdogo ila nyie waalimu ndio mnastahili zawadi Kwa sababu ni nyie mnatoa mchango mkubwa Kwa watoto wetu,Kwa hiyo mimi na baba yao tutapanga zawadi Kwa ajili ya shukrani Kwa waalimu, pia mama akatoa shukrani Kwa wanafunzi wengine akisema kwamba kuwepo kwawanafunzi na wenyewe ni mchango mkubwa Kwa sababu wangu hawajitoshelezi bila wenzao,pia mama akaendelea kusema kwamba watoto wote hawalingani kwa sababu ya Mwanangu ya Mungu mengi na yeye aendelee kusaidiwa na waalimu pamoja na wanafunzi wakishirikiana na wazazi na akasema anaamini siku moja atafanya vizuri hata ikibidi arudie darasa, waalimu walifurahi sana kwa maongezi ya Mama na msimamo wake Kwa mtoto wake ya Mungu mengi.

 

 

 

Basi Kwa mda wote ambao mama alikuwa anaongea baba alikuwa amechukia Kwa sababu ya mtoto wao ya Mungu mengi kufanya vibaya kwenye mitihani, Kwa hiyo yule baba akapewa nafasi ya kuongea kuhusu watoto wake walivyofanya vizuri na pia kuhusu mtoto wao wanaomlea aliyeitwa Kwa jina ya Mungu mengi. Baba akaanza kuongea Kama ifuatavyo.

 

ndugu zangu waalimu, wazazi na wanafunzi,Mimi nimesimamishwa hapa Kwa kazi mbili ya kwanza Kwa ajili ya ufaulu wa watoto wangu na ya pili Kwa sababu ya mtoto wetu ya Mungu mengi, kwanza kabisa najiona kama li jitu li kubwa kwa kuwa na watoto wenye akili na Kila siku wanakuwa wa kwamba,hii ni Kwa sababu Huwa nawahimiza kusoma wakiwa nyumbani,Kwa sababu elimu ya shule peke yake haitoshi,kwa hiyo mimi na waalimu ni nusu Kwa nusu nadhani Kwa upande wa wanafunzi hakuna ambaye anaweza kufundisha mwanangu nyote mko chini yake , yaani watu walishangaa na kuanza kuguna.akasema hata kamakiguna ndivyo ilivyo.

 

akageukia Kwa mtoto aliyeitwa ya Mungu mengi,huyu ni mwanangu ila SI wa kuzaa,Kwa sababu ningemzaa mwenyewe angekuwa na akili kama wanangu wengine watu wakashangaa na kuanza kusikiliza Kwa hamu Kwa sababu ilikuwa ni siri kati ya Hawa wazazi,ndipo mama akamyanganya kipaza sauti ma kikishika Kwa hiyo badala ya furaha ilawa karaha, ndipo mwalimu mkuu akaingilia kati watu wakashangaa sana,napia mtoto ya Mungu mengi akafahamu kwamba Hawa SI wazazi wangu na watoto wakafahamu siri ingawa sio kivile.

 

 

 

 

Kwa hiyo baba alinyanganywa kipaza sauti na kuambiwa akae chini atulie ili mambo mengine wakalizane nyumbani kama familia,basi mtoto ya Mungu mengi akaanza kufikilia na akawa mpole Kwa ghafla, Sasa mda wa kwenda nyumbani ukafika wakaondoka ila ya Mungu mengi akaondoka kimya akiwa na mawazo,alipofika nyumbani hakusema lolote Kwa sababu alikuwa na tabia ya kuzunguka nyumbani akiwa anacheza siku hiyo hakufanya vile ,basi na wale watoto wengine wakawa na wasiwasi kuhusu mwenzao Kama sio ndugu yao au la,basi kadri siku zilivyosogea mbele na hali ya kimasomo ikaendelea kuwa mbaya na mtoto akaendelea kujitenga hata na wenzake wakaanza kumtenga hali iliyosababisha kuwepo Kwa uchungu na fikra nyingi Kwa mtoto ya Mungu mengi.

 

 

 

 

Siku moja mama alisafiri pamoja na ya Mungu mengi safari ya mbali Kwa miguu,wakawa wanaongea ndipo ya Mungu mengi akamuuliza mama yake kuhusu maisha yake na ilikuwaje,ndipo mama akaamua kumsimulia hadithi nzima kuanzia mwanzo mpaka mwisho na mtoto akaumia sana na kuanza kulia usiku na mchana akiwalilia wazazi wake na kulaani kabisa roho mbaya anayoonyeshwa na baba yake mlezi na ndugu zake akijua kwamba msaada wake umebaki Kwa mama yake mlezi tu ndiye anayemjali kidogo,Kwa hiyo mtoto alilia sana mpaka akatamani kujiua ili aondoke duniani.

 

 

 

 

Kwa sababu mtoto ya Mungu mengi alikuwa kwenye mawazo makali bila mama yake kufahamu,Kwa hiyo aliamua kumuuliza mama yake kituo gani Cha watoto yatima walipomchukua, basi mama akamwambia kwamba ni sehemu inayoitwa ntonga,Kwa hiyo mtoto akakalili sehemu hiyo,Kwa kipindi hicho mtoto ya Mungu mengi alipokuwa kwenye maangaiko ni kama alikuwa na miaka kumi na mbili hivi Kwa sababu alikuwa anadeka sana kwa sababu alidhani yeye ni mtoto kweli wa family hiyo na ni mtoto wa pekee wa kike, Kwa hiyo baada ya kufahamu yeye ni nani kwenye familia hiyo aliamua kubadilika akaanza kusoma na kufaulu vizuri na pia akaingia kidato Cha kwanza akiwa na bidii kubwa na kufahamu kwamba yeye ni yatima ,Kwa sababu ya ufaulu wake baba yake mlezi alianza kumpenda.

 

 

 

 

Baada ya hapo alianza kufanya upelelezi kuhusu kituo Cha ntonga Kiko wapi bila mafanikio, siku moja wakiwa kidato Cha nne mtoto ya Mungu mengi alichaguliwa kuwa kiongozi wa dini Kwa hiyo aliwaamasisha watoto wenzake kuchangia michango ili kwenda kuwasalimia watoto yatima,ila akasema tupendekeze vituo wakapendekeza na mwanafunzi mmoja akapendekeza kituo Cha ntonga na ya Mungu mengi akasistiza waende huko na Kwa kuwa alikuwa anaaminiwa wote wakamkubalia na siku ikafika wakapanda gari wakaanza safari kuelekea ntonga.

 

 

 

 

 

 





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 922


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

USALITI (sehemu ya kwanza)
Post hii inahusu zaidi vijana wawili ambao ni msichana na mvulana walioingia kwenye mahusiano wakiwa sekondari na wakahaidiana kuoana ila kwa sababu mbalimbali walizokutana nazo kwenye safari yao ya mahusiano mmoja akamsaliti mwingine na kusababisha kupo Soma Zaidi...

Usichofahamu kuhusu mazoezi
Posti hii inahusu zaidi mambo muhimu ambayo hufahamu kuhusu mazoezi,ni mambo ambayo utokea au no matokeo mazuri kwa watu wanaofanya sana mazoezi. Soma Zaidi...

Hasara za wivu na kutokuwa wazi ( sehemu ya 2)
Posti hii inahusu zaidi hasara za wivu na kutokuwa wazi sehemu ya pili, sehemu hii inahusu mama Lisa anaenda kwa mama lina ili kuuliza kinachoendelea kwa mtoto wake , kwa hiyo tuona atapata jibu gani. Soma Zaidi...

Mwendelezo wa hadithi ya mahusiano ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya mahusiano ya vijana wawili baada ya kuhamia shule mpya. Soma Zaidi...

WAKATI WA KUFUMBUKA
Post hii ni mwendelezo wa hadithi inayohusu Kufumbuka ambapo , John anaonekana kama sio mtoto wa Mzee maganga kwa sababu na miungu imekili kwa sababu chakula chote kimeliwa na kuisha. Soma Zaidi...

Mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini ( sehemu ya tatu)
Post hii inahusu zaidi mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini wakipanda gari kuelekea shule kuanza maisha mapya. Soma Zaidi...

NIMLAUMU NANI part 1
Post hii inahusu hadithi Moja ya kijana maaalufu aliyeitwa Frank, ni kijana aliyekuwa mwaminifu ila amekumbana na wasichana wengi wanamasaliti ukizingatia Frank alikuwa kijana mstaalabu na mwaminifu sana ila anafikia kufanya maamuzi magumu kufuatana na ku Soma Zaidi...

NIMLAUMU NANI ( sehemu ya tatu)
Post hii inahusu mwendelezo wa hadithi ya kijana Frank na Amisa pia na wapenzi wawili ambao ni James na Amina. Soma Zaidi...

Mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya tano
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya tano, baada ya bibi kuachana na mke mdogo wa mfalme alienda kwa kijana wa kiume wa mfalme na kuona udhaifu wake kwamba anapenda sana mali. Soma Zaidi...

Mtoto wa tajiri na maskini (sehemu ya pili)
Post hii inahusu zaidi watoto wa wawili ambapo mmoja ni mtoto wa tajiri na mwingine ni mtoto wa maskini. Soma Zaidi...

Mahusiano ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi mahusiano yaliyotokea kati ya vijana wawili ila yanafika baadae mmoja akamsaliti mwenzake. Soma Zaidi...

SAFARI YA MUUJIZA
Post hii inahusu hadithi moja iliyotokea Kwa mama mmoja mwenye familia ya watoto watano.ambapo mama aliolewa na mwanaume mwenye maambukizi ya virus vya ukimwi na kupata watoto bila maambukizi kusambaa kutoka Kwa baba kwenda Kwa mama. Soma Zaidi...