SAFARI YA NNE YA SINBAD


image


Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad


SAFARI YA NNE YA SINBAD

Basi ikafikia siku ya kuanza safari yangu ya nne ya kibiashara. Tulianza safari ile usiku hata ikafika asubuhi tukiwa katikati ya maji. Njia ya safari hii sikuwa na uzoefu nayo na niliona mambo mapy. Niliweza kuona majabali yalofanana na watu, wanyama na vitu mbalimbali. Pia tuliweza kuona mawe ya ajabu ambayo huwa hayapati maji sikuzote. Tukiwa karibu ya kuingia kwenye kisiwa chetu cha kwanza kwa ghafla tulivamiwa na majiwatu makubwa na yenye nguvu sana.

 

Watu hawa walifanikiwa kututeka sote tuliokuwa mule ndani ya jahazi lile. Walitukamata wote na kutufunga kamba na kutuziba macho yetu kwa vitambaa hata tusione wapi tunakwenda. Walitupeleka tusikokujuwa na kwa kuelewa tu niliona kama tunarudinyuma. Waliturudisha nyuma kwa muda wa takribani masaa matatu kisha tukaelekea upande wa kushoto na kukiwacha kile kisiwa tulokuwa tukikiona kuliani. Tulikwenda kwamuda wa takribani masaa sita. Nikiwa nachukuwa hisia juu ya safari ili niligunduwa kumbe wanatuzungusha tuu lakini tunatupeleka pale kwenye kisiwa kile tulichokiona.

 

Hatimaye tukawasili na wakatufungua machoyetu na hapo nikapata tena kuona ardhi nzuri yenye udongo mweupe wa kupendeza. Wale watu wakawa wanagawana kila mmoja kucukuwa watu kadhaa katika sisi. Waligombaniana watu wote na kubakia mimi. Walichelea kunichagua kwa sababu nilikuwa nimekonda sana. Basi akatokea mzee mmoja wa heshima katika wao akanichukuwa. Basi wote tuliingizwa kwenye jumba moja na kuletewa chakula kilichofanana na machicha ya nasi. Bila ya kuchelewa wenzangu wakaanza kula chakula kile ila mimi nikachelea kukila hata kikaisha.

 

Baada ya muda tukaletewa majani mithili ya majani ya miwa lakini haya yana maji mengi na ni matamu sana. Mimi sikuyala kwa kuhofia usalama wangu. Niliweza kugunduwa ladha yake kwa kuhadithiwa na wenzangu. Nilikaa na njaa kwa muda wa siku mbili hata nikakosa nguvu. Yule mzee akamiletea samaki wa kuchoma pamoja na mayai ya kasa. Nilikula sana hata nikashiba. Nilipopata nduvu ziku ya tatu nikaona mabadiliko kwa wenzangu. Walikuwa wakinenepa sana kwa ghafla kila walipokula vyakula vile. Kitu cha kushangaza wakawa wanapoteza kumbukumbu na kuwa na akili ya kinyama kinyama.

 

Hali iliendelea hivi kwa muda wa wiki tatu hata akawa mmoja kati ya wenzangu hawezi kupita kwenye mlago kwa unene. Basi wale watu wakawa wanamchukuwa mtu mmojammoja kila wiki na kuondoka nae na asirudi. Nikawa nafatilia nini kinaendelea hata nikagunduwa kuwa wanakwenda kumchinja na kumuuza nyama kwenye kisiwa kingine. Niolijaribu kuwaeleza wenzangu lakini wamekuwa wanyama hakuna walijualo zaidi ya kula tu. Mimi niliendelea kula vyakula kwa kuiba na hali yangu ikazidi kudhoofu.

 

Yule mzee akaamuwa kunitoa bandani mule kwa kuamini nikiwa huru naweza kunenepa. Hali iliendelea hivyo hata nikapewa funguo ya kuwalinda wenzangu. Waliendelea kuchinjwa hata wakabakia watu kumi na mbili. Kuna siku kulikuwa na sherehe na watu wakaondoka na kuniacha mimi na yule mzee. Basi nilitoroka pale peke angu kwani ningemhukuwa yeyote asingekubali na kwa unene na uzito alonao asingeweza kukimbia hata kidogo. Basi nilitoroka kwenda mbali zaidi.



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    2 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    3 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    4 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    5 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    6 Magonjwa na afya    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili,ambapo Mama yake na Jackie pamoja na jack wakiwa hospital na jack anaendelea kumwita Julius kila mara. Soma Zaidi...

image Hadithi iliyosimuliwa na tabibu
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

image Mwendelezo wa hadithi ya Mama mchoyo na mwehu
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Mama mchoyo na mwehu, kwa sababu mwehu alikuwa mkarimu alichukua ule mkate akawapstia watoto wa yule mama wakiwa wanatoka shule kwa hiyo tutaona kilichotokea kwa wale watoto. Soma Zaidi...

image Siri ya wageni wale inafichuka
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

image Hadithi ya chongo wa kwanza mtoto wa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Kuingia kwa wageni
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Mshenga wa aladini mbele ya mfalme kwa mara ya pili
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

image Hadithi ya mzee wa tatu na mbwa wake mwekundu
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image NIMLAUMU NANI ( sehemu ya tatu)
Post hii inahusu mwendelezo wa hadithi ya kijana Frank na Amisa pia na wapenzi wawili ambao ni James na Amina. Soma Zaidi...

image Aladini na binti wa mfalme
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya mshumaa wa ajabu Soma Zaidi...