image

Safari ya tatu ya Sinbad

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad

SAFARI YA TATU YA SINBAD

Siku ile ya pili Sinbad mbeba mizigo alivaa ngup zake safi alizonunua na kijipamba vyema na kuelekea kwenye kikao chao. Alipofika alikuta watu wote wamekusanyika tayari wanamdsubiri yeye. Alipofika vinywaji viliagizwa na vyakula laini. Watu wakaanza kuburudika, na baada ya muda mzee Sinbad akawasili na kuaza kusimulia safari yake ya tatu kama ifuatavyo:-

 

Basi niliamua nisafiri tena kwa mara ya tatu, nikafuatilia taarifa za kuwa jahazi linaondoka lini na wapi. Nilikusanya bidhaa za kwenda kuanza nazo na maandalizi nilikamilisha kwa muda wa wiki nzima. Siku ya safari ilipofika ndugu zang walinisaidia kupeleka mizigo baharini. Walinisaidia na kupandisha pia huku wakinishawishi nisiende. Bila ya kujuwa kitakachonikuta nilikataa ushauri wao na kujitetea kuwa kwa miezi sita sijasikia ajali yoyote iwe leo kisa mimi nimo?.

 

Tulisafiri salama katika visiwa kadhaa na safari ilikuwa ni njema kwakweli. Tulifanya biashara visiwa kadhaa na kuona faida na matunda ya biashara. Hapa nikawa najuta kwa nini sikufanya biashara kwa muda wote huo. Tulikubaliana tuendelee kidogo kufanya biashara kisha turudi nyumbani baada ya siku kadhaa. Ijapokuwa nilipenda tuendelee lakini mawazo ya wengi sikuyakatalia. Basi tukaendelea na visiwa kadhaa hata kukaelekea kwenye kisiwa cha mwisho ili tugeuze. Kwa jumla tulikuwa watu 48 wafanya biashara pamoja na manahodha na wasaidizi tulikuwa jumla ya watu 60.

 

Tulipokuwa tupo kwenye bahari tukielekea kisiwa kile ghafla nahodha alipoteza uelekeo na kutuambia amepotea na yupo kwenye kisiwa cha maharamia vibushuti. Hatukuelewa nini anazungumzia lakini alifafanua zaidi ni watu wafupi wanaotembea kwa makundi. Kazi yao ni kupora majahazi. Basi haukupita muda tukawaona wanakuja, nahodha aliongeza kuwa kupambana nao kwenye maji hatuwezi ila tukienda nchi kavu hawatakuja.

 

Nahodha alijitahidi awezavyo awahi kufika nchi kavu kwenye kisiwa kinachoonekana jirani. Hakuwahi kufanya hivyo tukavamiwa na jahazi letu likachanywa na kukatwa katwa na nanga ikakatwa. Walipora mali zetu zote na tukakimbilia kwenye kisiwa kile. Tukiwa tukihangaika nini tufanye kuondoka pale tukaona kuna jumba kubwa sana mbele yetu. Bila ya kujuwa kama ule ni mtego mwingine tukaingia kwenye jumba lile na kuanza kufanya mipango.

 

Usiku ulipofika tukaamua kujisitiri mule. Kumbe jumba lile ni mtego wa majidude yanayokula watu. Wanavizia wasafiri wanapopata matatizo na kuporwa wakiingia mule wananafungua na kuwala. Basi usiku ule likaja jitu moja kubwa sana na refu pia. Kwa urefu alonao nilimfikia magotini na upana wake lamda tujipange saba kama mimi. Ukiangalia ukubwa wa jumba lile utaamini ukubwa wa alolijenga.

 

Basi limtu lile lilipoingia likafunga mlango na kukoka moto. Tukiwa tumetulia sana hatujui tufanye nini, lile limtu likaamza kumshikamshika kila mmoja. Likamkamata nahodha mkuu na kuanza kumbanika. Kumbe lilikuwa likiangalia mtu alionenepa amle. Alimbanika nahdha wetu na kuanza kumla. Alimla wote kisha akalala fofofoi. Kila mmoja alikuwa akitetemeka na kuanza kulia na kuogopa.

 

Lile limtu likalala pale mpaka ilipofika karibu na alfajiri likatoka na kuacha mlango wazi. Tulikaa pale ndani na baada ya muda tukatoka. Tulipofika nje tukaanza kupiga mipango ya kuondoka. Tulizunguka kisiwa kile kutafuta pa kulala lakini tulikosa. Tukiwa katika hali ilie nikapata wazo la kuwa tutengeneze mitumbwi midogomidogo. Tukaanza kufanya kazi ile hata usiku ukakaribia kuingia. Nikawashauri wenzangu kuwa tumuuwe yule mtu au tumtoboe jicho lake. Maana alikuwa najicho moja tu. Nikasisitiza kuwaambia kama tutamuuwa ndo tutaweza kuondoka hapa bila hivyo atatufuata na wenzie.

 

Tukapanga mpango wa kumuuwa na mimi nikiongoza mtego. Usiku ule tukaingia mule ndani na tukajifanya tumelala. Lile limtu likaingia na kuanza kumpapasa kila mmoja ili achukuwe alonona amle. Alimchukua nahodha mwengine alokuwa amenenepa zaidi katika sisi. Basi akambanika pale tukiwa tunamuona. Uchungu ulinishika lakini niliendelea kusubiri alale. Alipolala tu nikaweka msumari wa moto kwenye mato na ukaiva vizuri hata ukawa mwekundu sana. Baada ya muda nikawdokoa wenzangu kuwa mambo tayari

 

Nilimfata yule limtu na kumchoma na msumari ule kwenye jicho lake. Alilia sana na kuguta makelele. Alikwenda kukaa mlangoni ili atukamate. Kwakuwa alikuwa ni mrefu sana tuliweza kupita kwenye magoti yake hata bila kutupata. Tukaenda kwneye mitumbwi yetu na kuanza kuimalizia kwa msaada wa mbalamwezi. Lile limtu likaelekea sehemu huku linalia. Muda le kwa haraka zaidi tukamaliza mitumbwi yetu na tukagawana waiwi wawili kila mtumbwi.

 

Baada ya kugawana tukaanza kuingia maji kila mmoja anajitahidi kuenda kwa haraka kiasi awezavyo ili kuweza kuondoka kisiwa hiki. Basi baada ya jua kuchomoza tulikuwa mbali kidogo lakini tukashangaa tunaona weupe unakuja. Kumbe lile limtu lilikwenda kuwatafuta wenzie wengi wakiwa wamebeba mawe. Kwa urefu wao walianza kuyaingia maji na kuanza kuturushia mawe. Wenzetu walokuwa nyuma walizama kwa mawimbi ya maji baada ya kurushiwa majimawe makubwa. Mwshowe mitumbwi miwili tu iliokoka wakwetu na wawenzetu, hivyo tukawa wanne tulookoka.

 

Tulikwenda bila ya kujua wapi tutaishia, kwa bahati tukaona kisiwa kwa mbele zaidi. Tukaingia kwenye kisiwa kile na kunanza kutafuta chakula. Tukapata matunda na maji. Tuliandalanda pale na ilipofika jioni tulilala chini ya mti. Kwa ghafla usiku alikuja nyoka mbubwa sana na akamchukuwa mwenzetu aliyekuwa pembeni amelala. Tukaogopa sana maana tumeokoka kule kwenye mawatu na sasa ni nyoka. Kwa hakika usingizi haukuja tena.

 

Ilipofika asubuhi tulitafuta njia ya kurudi bila mafanikio basi nikawashauri wenzangu tutengeneze kitundu cha miiba tulale. Basi tukakusanya miiba mingi na kutengeneza kitundu.yule nyoka alipokuja usiku ule alizunguka kwenye miiba bila ya mafanikio. Baada ya muda alipata kaupenyo ka kuingia na akamchukuwa mwenetu mwingine. Pale tukabaki wawili tu. Asubuhi tukawatunajishauri la kufanya, bila mafanikio tukabahatisha kupata matunda machache ya kula tu.

 

Tukaamua kutengeneza kitundu juu ya mti na chini tuzungushe miba ili ashindewe kupanda. Tukafanya vile na ulipofika usiku alizunguka sana nyoka yule na aipate pa kuingia. Aliruka na kuivunja miba ile na kupanda juu na kumchukiwa mwenzangu pale nikabaki peke angu. Asubuhi ilipofika nikazunguka sana kisiwani pale na nikakuta sehemu kuna kimfereji cha mguu mmoja. Nikakivuka na kukutana an kisiwa kingine. Yule nyoka alishindwa kuja kule kwa sababu ya maji ya chumvi ambayo yangemuuwa kama angejaribu kuyavuka. Nilitembea huku na kule na kufika sehemu kuna kijibostani kizuuri. Nikawa nakula matunda. Kwa mbali nikaona kuna kibibi kizee kinaniita kwa ishara.

 

Nikaenda pale nikakikuta kibibi kinataka kuvushwa kwenye mfereji. Nikakibeba, ila mara tu baada ya kukibeba kikatia makucha yake kwenye mbavu zangu na kuganda. Kikawa kinaninyonya damu. Nikikaa pia habanduki, nilijitahidi kadiri niwezanyo lakini hakutoka. Nilichoka sana na nikaanza kupoteza nguvu na kukonda zaidi. Siku ya tatu nikatengeneza pombe kwa kutumia mizabibu na ilipokkuwa tayari nilimreburebu hata akakubali kunywa. Alipolewa aliachia na kuanguaka na hapo nikamkimbia.

 

Nilizunguka sana na mida ya mchana nikaona jahazi kwa mbali, hapo nikavua shati langu na kuashiria wajeniokoa. Walipokuja nikawasimulia habari yangu. Wengi walinipa pole na wengine wakanambia bahati yangu ila ningekufilia mbali. Wakanichukuwa na kuenda nao na safari yao. Tukafika sehemu kuna kisiwa, yule nahodha akanambia shuka ukafanye kama watu wanavyofanya. Nikaendanao watu wa jahazi lile mpaka kwenye kisiwa kile. Basi wakaokota mawe mengi sana wakawa wanawapiga nyani waliopo kwenye minanzi.

 

Nikaokota mawe na kupiga na mimi, basi kila nikimpiga nyani kwa jiwe ananirudishia kwa kunipiga na nazi. Basi nachukuwa nazi ile na kuiweka kwenye mizigo yangu. Niliweza kupata nazi mia sita. Mizigo ya watu ilipoenea tukaondoka na kwenda kisiwa kingine na kuuza bidhaa zile. Nilipata faida kubwa kuliko ile ilopotea kwenye maji. Baada ya hapo nikanunua bidhaa na tukaendelea kufanya biashara visiwa kadhaa na tulipofika karibia na baghadadi nikashuka na kurudi kwetu kwa majahazi yanayokwenda Baghadadi

 

Safari hii nilipata faida kubwa lakini nilipatwa na makubwa zaidi. Nilikuta ndugu zangu wakilia pindi nilipowaelezea kilichonikuta. Nilitowa sadaka mali yangu na kuendeleza biashara zangu. Niliogopa tena kufanya biashara za majini. Ijapokuwa uwoga huu unanipata kwa muda ila huenda nikasahau. Na hivi ndivyo huwa sikio la kufa halisikii dawa. Miezi kadhaa ilipita na niliposikia msafaa wa biashara unatoka baada ya siku 12 nilijifunganya na mimi niweze kutoka safari ya nne.

Mpaka kufika hapa Sinbad wa baharini akamaliza msafara wake wa tatu na kumpatia Sinbad mbeba mizigo pesa kiasi kwa kufidia kazi zke. Akamuahidi awahi kesho maana safari ya nne alikutwa na hatari na mambo makubwa zaidi na alipata faida pia.






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Aliflela1 Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1267


Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 kitabu cha Simulizi     👉6 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Hadithi ya binti wa pili mwimba mashairi mwenye makovu
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Alif lela u lela 1
Alif lela u lela ni hadithi zilizosheheni utamu na machungu pamoja na visa vya wachawi na majinim soma sasa. Soma Zaidi...

Alif lela u lela: utangulizi
Katika nchi za China, Hindi, Uarabuni na Uajemi alikuwepo mfalme aliyefahamika na kuheshimika sana kwa uhodari wake na utawala wake mzuru. Soma Zaidi...

UFUPISHO WA ALIFU LELA ULELA KITABU CHA KWANZA
Posti hii inakwenda kukisimulia kuhusu hadithi za alifu lela ulela KITABU CHA KWANZA Soma Zaidi...

Safari ya tano ya Sinbad
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

HADITHI ZA SINBAD
Soma Zaidi...

Safari ya sita ya Sinbad
Posti hii inakwenda kukuletea muendelezo wa safari za Sinbad Soma Zaidi...

Safari ya pili ya Sinbad
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

Kisiwa cha uokozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

Ndoto ya mgonjwa, binti mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Hadithi ya binti wa kwanza na mbwa
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

alif lela u lela
Soma Zaidi...