SANDA YA MWANAMKE NA NAMNA YA KUMKAFINI


image


Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: Dhana ya elimu ya uislamu)


  • Sanda ya mwanamke na namna ya kumvika.

-    Sanda ya mwanamke ina vipande vitano; 

  • Majamvi 2
  • Shuka (Gagulo) au Underskirt 1
  • Kanzu (Blause) 1
  • Shungi (Ukaya) 1.

 

    -    Taratibu za kutayarisha sanda na kukafini:

  1. Majamvi mawili yatatandikwa moja baada ya nyingine.
  2. Kikatwe kitambaa cha ukubwa wa shuka ya kujifunga kiunoni (shuka/gagulo) na iwekwe juu ya majamvi mawili ili ije kutumika kumfungia kiunoni.

 

  1. Kisha ikatwe kanzu (blause) isiyoshonwa vizuri kwa kukunja kitambaa na kukitoboa katikati kwa ajili ya kuingizia kichwa cha maiti (kumvalisha) na kisha kushikiza pembeni kwa uzi mfano wa kanzu kata mikono na kuwekwa juu ya gagulo sehemu ya chini (kiunoni) na itakuwa juu ya majamvi 2 sehemu ya juu (kifuani).

 

  1.  Kitambaa (ukaya/shungi) ya kutosha kuweza kufunika kichwa na uso kitaingizwa ndani ya shingo ya kanzu na kunyooshwa kwa juu.

 

  1. Maiti itaanza kuvalishwa kanzu, kisha kufungwa shuka (gagulo) juu yake. Kisha maiti itawekewa pamba viungo vyote vya sijda na kuziba sehemu za matundu kama ilivyokuwa kuwa kwa maiti mwanamume. Kisha maiti itatizwa (itafungwa) na majamvi mawili, moja baada ya jingine kwa kuanza kunjo la kushoto na kumalizia la kulia juu yake, na kisha kufungwa na kamba tatu juu yake- kichwani, tumboni na miguuni na kuwa tayari kuingizwa kwenye jeneza na kuswaliwa.



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    2 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    3 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    4 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    5 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    6 Hadiythi za alif lela u lela    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Lengo la kuumbwa Mwanadamu ni lipi?
Kwenye kipengele hichi tutajifunza lengo la kuumbwa mwaanadamuengo la kuumbwa ulimwengu na viumbe vilivyomo. Soma Zaidi...

image Uandishi wa hadithi wakati wa tabiina (wafuasi wa maswahaba)
Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Matendo ya hijjah na umrah
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Nini chanzo cha elimu zote na ujuzi wote
Ninichanzo cha Elimu? (EDK form 1 Dhanaya Elimu) Soma Zaidi...

image Umuhimu wa jihad katika kusimamisha uislamu katika jamii
Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu
Faradhi kwa maiti ya muislamu (edk form 2:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Walio katika hatari ya kupata magonjwa ya ngono
Posti hii inahusu zaidi watu walio kwenye liski ya kupata magonjwa ya ngono, ni watu wanaofanya mambo yanayosababisha kupata magonjwa ya ngono. Soma Zaidi...

image Zoezi la nne mada ya fiqh.
Maswali mbalimbali kuhusu fiqh. Soma Zaidi...

image Kwanini Ni muhimu kusimamisha uislamu katika jamii
Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Taasisi za kisiasa za msingi alizotumia mtume (s.a.w) katika kuanzisha dola ya kiislamu madinah
Dola ya kiislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...