Sanda ya mwanaume na namna ya kumkafini

Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

-    Sanda ya mwanamume ina vipande (majavi) vitatu.

 

  1. Weka kipande cha kwanza juu ya mkeka kisha cha pili na cha tatu na vyote kushikizwa kwa uzi katikati, na kila kipande kipakwe marashi na ubani. 

 

  1. Pasua kamba katika pembe mbili za jamvi la kwanza, moja kwa ajili ya kufungia kichwani na nyingine kwa ajili ya kufungia miguuni.

Kamba moja itachanwa kutoka jamvi la pili, ili kumfunika (kufungia) maiti katikati. Na kamba tatu zitachanwa jamvi la tatu na la pili kwa ajili ya kufungia juu ya mkeka.

 

  1. Maiti italazwa juu ya majavi yote matatu. Ichukuliwe pamba iwekwe manukato kisha iwekwe juu ya viungo vyote vya sijda; paji la uso, viganja vya mikono, magotini na vidole vya miguu. Pamba itumike pia kuziba tundu zote mwilini; mdomo, masikio, pua na makalio.

 

  1. Maiti itatizwe (ifunikwe) mwili wote, kwa kuanza kipande cha kwanza, kisha cha pili na cha tatu ukitanguliza kunjo la kushoto kisha la kulia linafuata. Zile kamba zilizochanwa zitatumika kufungia vitanzi maiti kichwani, tumboni na miguuni. Baada ya hapo maiti inaweza kuwekwa kwenye jeneza baada ya kuzungushiwa kwa mkeka tayari kwa kuswaliwa.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/01/02/Sunday - 02:43:56 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1568


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Sababu za kushuka surat al-Fiyl
Al fiyl ni neno la Kiarabu lenye maana ya tembo. Sura hii inazungumziakisa cha jeshi lenye tembo. Jeshi hili lilikuwa na nia ya kuvunja al qaaba Soma Zaidi...

Haki za viumbe na mazingira
Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: Dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Sura za makkah na madinah
Quran (EDK form 3: Dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Kumkafini (kumvisha sanda maiti)
Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Mfumo wa ulinzi na usalama katika fola ya uislamu madinah
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Umuhimu wa jihad katika kusimamisha uislamu katika jamii
Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Malezi ya mtume
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Aina za tawafu
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Lengo la kushushwa vitabu vya mwenyezi Mungu (s.w)
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Maadui wakubwa wa dola ya uislamu madinah
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Kina Cha uovu wa shirk
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Nguzo za swala.
Kipengele hiki kinaelezea nguzo mbalimbali za kuswali. Soma Zaidi...